Jaji Mutungi: Rais Magufuli hajafuta mikutano ya kisiasa

Afadhali ange-endelea kukaa kimya. Sijaona kama anawatetea wapinzani kupata haki zao wanaposhughulikiwa yeye huwa kimya. Leo mjomba tumemsikia wote halafu mwenzetu anatuambia TRANSFOMA zetu ni mbovu zimemuelewa mkuu visivyo. Yaani huyu hataki kuona kinachoendelea kwa wadau wake?
 
hayo ndio madhara ya
upload_2016-6-24_23-53-53.png
hata wale hawajauna madhara ya
upload_2016-6-24_23-55-14.png
wataanza kuyaona muda si,mrefu
 
hahaha. ..aisee..huyu ndiye msajili wa vyama vya siasa ..tehtehteh
Why now? Mbona amekuwa kimya muda wote huo ambao wapinzani wamekuwa wakipambana na dola kwa ubakaji dhahiri wa demokrasia? Kwani yeye ........
Hawa wasajili wa vyama vya siasa wanajifanya kuvaa miwani nyeusi Chama cha majipu kinapobaka demokrasia. Kama huyu Jaji anajali demokrasia alipasa kukifuta chama cha majipu na ufisadi au kukipa muda wa kubadili jina. Hili jina la mapinduzi wakati nchi inafuata mfumo wa DOMOkrasi halifai kabisa. Ni lazima ajipendekeze kwa chama cha majipu? Au Bwana mitungi ameamua kufuata nyayo za NS?
 
Ha
Kwa hiyo jaji mutungi kawa msemaji wa rais au ikulu.?! Katumwa na rais?! Kwa hiyo ikulu haihitaji tamko lolote maana jaji mutungi kaishatoa kwa niaba ya rais?! Kama huyu ndiye msajili wa vyama nina wasi wasi kama tutafika salama!
Hakika huyu jaji hana tofauti na jina la mleta mada sijui hukumu zake zilikuweje maana anapindisha hotuba ya mkuu bila ridhaa yake
 
Mtungi, acha kutumika vibaya usitakase vilivyotiwa najisi mwachie aliyevitia najisi aje kuvitakasa kwa kauli yake mwenyewe.

Rais tulimsikiliza tukamwelewa na hata mtoto wa miaka 12 aliyemsikiliza ukimuuliza alielewaje atakuambia kwa jibu hilohilo tulivyoelewa sisi wakubwa.
Nimekushangaa sana ulipojitokeza kutoa tafsiri ya kauli za mkuu wa nchi pale alipolikoroga.

Tafsiri uliyotoa wewe ndiyo iliyojaa upotoshaji.

Sitashangaa utakapoambiwa kuwa unajipendekeza kwa mkubwa kutaka kutolea ufafanuzi na tafsri potofu visivyokuhusu.

Sitashangaa vijana watakapo kuona kuwa unakiherehere, ungali hujaonja pilipili.

Pia sitashangaa vijana wakikusema vibaya mfano pale watakaposema ''sasa mzee huyu anazeeka vibaya'' utakuwa umejitakia.
 


Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi amewataka wanasiasa kutoitafisri vibaya hotuba ya Rais kwamba amepiga marufuku shuguli za kisiasa na badala yake watambue kuwa alichosema Rais ni kwamba amefungua milango ya mashirikiano na wanasiasa katika kuendeleza Taifa kwa kufanya kazi na siyo muda wote kuhubiri siasa

Amesema kuwa wanasiasa wasipotoshe wito wa Rais kisiasa kwa kudai kuwaRais amefuta harakati za siasa nchini.

amesema wito wa Rais ni kuwakaribisha wanasiasa katika maswala ya maendeleo na sio siasa zisizo na tija.

source:ITV

Ni vema umefafanua!
Inasaidia sana kuweka vitu mahali pake!
 
Huyu Mtungi amekuwa msemaji wa Ikulu kuanzia lini? Au amekuwa msemaji wa ccm kuanzia lini ? Huyu naye ni jipu lililoiva haswa! Toka lini mlezi wa vyama akawa msemaji wa chama kimojawapo?
 
Ameeleza upotoshwaji unaofanywa ili kutafuta kick ya kisiasa
Amepotosha kauli ya Rais maana nina hakika sivyo alivyomaanisha. Aangalie asije akatumbuliwa kwa kujipendekeza kufafanua yasiyomhusu.
 
Magufuli alihimiza kushirikiana ili kuleta maendeleo kwani sasa si muda wa siasa bali ni kazi tu. sasa nashangaa mwasema kakataza shughuli za kisiasa.
Hiyo ya kushirikiana alichomekea tu baada ya kujishtukia. Wachambuzi wa hotuba wanaweza kukupa uchambuzi wa sentensi kwa sentensi , hoja ipi imetangulia na kwa nini. Hilo alilichomekea tu baada ya kuona sehemu kubwa ya hadhira imebaki imemtumbulia macho! Tazama tena video kwa makini.
 
Kumbe kawaalika wakanywe chai? Labda hawaelewi kiswahili vizuri
Hata bungeni anakoamini ndio mahali pa kufanyia 'siasa' (kwa maana neno 'siasa' aliyo nayo kichwani mwake, yaani kinyume cha 'kufanya kazi'), nako amewawekea kauzibe. Amemuweka kibaraka NS asiwape wapinzani nafasi ya kusiasisha hoja zao! halafu huyu jaji anajiweka kimbelembele na utetezi mfu!
 
atatue kwanza issue ya sukari na ongezeko la tozo kwenye mitandao ya simu hasa ktk huduma zakifedha kwani hili ongezeko humuathiri mwananchi moja kwa moja na hili halihitaji mpaka wapinzani wakamshaur raisi
Sukari na simu ndio demokrasia tena!? Duh! Kweli wapinzani huwa hawana hoja ya ukweli, ni kama "Nagging wife" ukimpa hiki atadai kile! Hawa ni wa kupuuzwa tu! Go, go, go Magufuli.
 
Ndo tujue umuhimu wa kuwa na katiba mpya! yaelekea hii ya sasa rais wetu haitaki maana anaisukuma pembeni! na huu utaratibu wa jaji kuteuliwa na rais ni shida! inafikia hatua tunashindwa kumtofautisha msomi wa bongo na std 7!
 
Back
Top Bottom