Jaji Mutungi: Rais Magufuli hajafuta mikutano ya kisiasa

Viongozi wa CCM kwa sasa hawaoneshi tofauti ya kusoma na exposure wote kujipendekeza kwa kwenda mbele, weledi umewekwa kando. Hajulikani mwenye PhD kama Mwakyembe, Hajulikani std 7 kama Lusinde, hajulikani jaji kama Mutungi.

Kwa mwendo huu naanza kuona wasi wasi kuwa hata huko mahakamani majaji wenyewe hawa makada kama alivyotuonyesha jaji Bomani alipokuja kugombania kuteuliwa nafasi ya Urais kwa tiketi ya CCM, sijui kwa wapinzani watapata haki, hatimaye na sisi Tanzania tumepata Museveni wetu, hongera CCM
 
Jaji anajaribu kuziba mapungufu yaliyojitokeza kwenye hotuba ya rais na hilo ni jambo la kawaida ukizingatia hiyo hoja inaangukia kwenye taasisi anayoiongaza yeye jaji
 


Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi amewataka wanasiasa kutoitafisri vibaya hotuba ya Rais kwamba amepiga marufuku shuguli za kisiasa na badala yake watambue kuwa alichosema Rais ni kwamba amefungua milango ya mashirikiano na wanasiasa katika kuendeleza Taifa kwa kufanya kazi na siyo muda wote kuhubiri siasa

Amesema kuwa wanasiasa wasipotoshe wito wa Rais kisiasa kwa kudai kuwaRais amefuta harakati za siasa nchini.

amesema wito wa Rais ni kuwakaribisha wanasiasa katika maswala ya maendeleo na sio siasa zisizo na tija.

source:ITV


Sasa atakuwa anawapangia agenda za kuzungumza? Chombo gani kipitie agenda hizo na kuzikubali ama kuzikataa ili mikutano izuiliwe ama ikubalike?

Chaso wanatakiwa wafanya nini wakati wa mahafali yao?

Agenda gani ambayo wapinzani wanayo ambayo si ya maendeleo na badala yake ni siasa isiyo tija?

Kukosoa serikali nndiyo siasa zisizo tija? Kuwapa mwanga namna Ccm inavyoua nchi siyo suala la maendeleo?

Tanzania!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!.
 
Ningefurahi kama angetoa vifungu vya sheria vinavyosimamia vyama vya siasa na majumu yao kwa kulinganisha na statement kwamba visubiri 2020 badala ya kutoa tafsiri yake binafsi.
 
Rais aliyepatikana kwa njia za kidemokrasia anapiga marufuku mikutano ya kisisa , amabayo ndio iliyomuungiza madarakani ! Anataka kutuaminisha kuwa
1. Aliingia madarakani kwa njia zisizo za kidemkrasia, ndio maana haoni kuwa vyama vya siasa vina haki hiyo kikatiba.kwa hiyo hawezi kuheshimu demokrasia?
2.Anahisi hana uhalali hivyo anatumia muda huu aliopiga marufuku mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani kujihalalisha?
3.Anataka kutumia nguvu za kijeshi kujiimarisha madarakani;?
4.Anataka kutuaminisha kwamba CCM sio chama cha siasa bali ni DOLA?
Kamwe hawezi kutunyamazisha!
 
MSAJILI wa Vyama vya Siasa Nchini, Jaji Francis Mutungi ametetea kauli ya Rais John Magufuli kuhusu kufanya siasa wakati huu na kwamba alichotaka kiongozi huyo wa nchi ni ushirikiano kutoka kwa wanasiasa wenzake ili kuwaletea maendeleo wananchi.

Alisema Rais Magufuli, katika kauli yake ile hakumaanisha kuzuia shughuli za siasa nchini isipokuwa alieleza kuwa hatakuwa tayari kuona siasa zinakwamisha mikakati ya kuwapelekea wananchi maendeleo yao.

Jaji Mutungi alisema hayo Dar es Salaam jana, alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu kauli ya Rais Magufuli ya kuwataka watu kuacha siasa za hovyo hadi mwaka 2020 utakapofanyika uchaguzi mkuu mwingine, ili muda uliopo wautumie kuijenga nchi.

“Watu wametafsiri tofauti kauli ya Rais, lakini ni kwamba alikuwa akiomba ushirikiano wa wanasiasa wenzake na wadau wote wa siasa kuleta maendeleo… kwa hiyo kabla ya kukosoa kauli ni vyema ukafanya utafiti siyo kuibeba na kuitafsiri kwa mrengo tofauti,” alisema .

Alisema siyo kwamba Rais anapinga siasa isipokuwa anapingana na wanasiasa ambao ni pingamizi katika kuleta maendeleo na muda wote wamejikita katika siasa bila kuangalia namna ya kutekeleza ahadi zao kwa wananchi.

Alisema wapo watu walioitafsiri tofauti hotuba aliyoitoa juzi Rais Magufuli, hivyo wananchi wanapaswa kuwa watafiti na kuweka maslahi ya nchi huku akiwataka wanasiasa kuwa wavumilivu na kutumia muda wao kutafakari jambo kabla ya kuzungumza.

“Rais alikuwa akijaribu kuwasihi wanasiasa kuangalia namna ya kujikita kwenye siasa ya maendeleo ya jamii kwa ujumla na kuachana na siasa za kupinga maendeleo,” alisema.

Alisema dhamira ya Rais ni kuwaletea maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla na vyama vinapaswa kufuata utaratibu wa kuwasilisha taarifa kwa msajili na si kusubiri hadi vyombo vya habari kutoa taarifa.

Mutungi alisema vyama vya siasa vimekuwa vikitaka demokrasia nchini, hivyo kabla ya vyama kufikiria demokrasia kitaifa, hivyo viongozi wake waanze kuangalia suala hilo kwenye vyama vyao na si kuimba, kwani wapo wanaofanya ndivyo sivyo.

Alisema mtu anapotetea jambo, kwanza anapaswa kulitekeleza kwa vitendo huku akibainisha demokrasia kutotokea nchini endapo demokrasia ndani ya vyama vya siasa kuwa ni shida.

Jaji huyo alisema bado kuna kazi kubwa huku akibainisha yapo mambo mengi yanayotokea nchini huku akitegemea ushirikiano wao na kuwataka wanasiasa kuwekeza katika kufanya upembuzi wa mambo kabla ya kutamka au kuyatenda.

Naye Msajili Msaidizi, Kitengo cha gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma, Piencia Kiure alisema ni vyama vitatu tu kati ya 22 ndivyo vimewasilisha taarifa ya gharama za Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana.

Mwisho wa kuwasilisha gharama hizo ni leo. Alivitaja vyama vilivyowasilisha gharama za uchaguzi kuwa ni Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT-Wazalendo na Chama cha Wananchi (CUF).

Alifafanua kuwa, mgombea atakayeshindwa kuwasilisha gharama za uchaguzi utahukumiwa kifungo kisichozidi mwaka mmoja au faini isiyozidi Sh milioni mbili au vyote kwa pamoja.

Aidha, chama kitakachoshindwa kuwasilisha gharama za uchaguzi katika kipindi kilichowekwa adhabu yake ni faini isiyozidi Sh milioni tatu na kutoruhusiwa kushiriki uchaguzi hadi watakapofanya marejesho

Maoni yangu

Faiani ya milioni tatu kwa chama kitakachoshindwa kuwasilisha gharama za uchaguzi ni ndogo sana ikiwa kweli tuna nia ya kupambana na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya ya fedha katika chaguzi zetu, mamlaka zinazohusika zinapaswa kuangalia adhabu nyingine na kali zaidi ili kuvifanta vyama vyetu viiogope hii sheria badala ilivyo sasa wanaidharau kwa kuwa gharama ya faini yake ni kiasi kidogo sana
 
Rais aliyepatikana kwa njia za kidemokrasia anapiga marufuku mikutano ya kisisa , amabayo ndio iliyomuungiza madarakani ! Anataka kutuaminisha kuwa
1. Aliingia madarakani kwa njia zisizo za kidemkrasia, ndio maana haoni kuwa vyama vya siasa vina haki hiyo kikatiba.kwa hiyo hawezi kuheshimu demokrasia?
2.Anahisi hana uhalali hivyo anatumia muda huu aliopiga marufuku mikutano ya siasa ya vyama vya upinzani kujihalalisha?
3.Anataka kutumia nguvu za kijeshi kujiimarisha madarakani;?
4.Anataka kutuaminisha kwamba CCM sio chama cha siasa bali ni DOLA?
Kamwe hawezi kutunyamazisha!

Kama we mwanaume wa siasa itisha mkutano...tuone kama hajaongezeka mjane na yatima...
 
Mfalme
Hakosei
Hakosolewi
Ni mjuvi wa kila nyanja
Anajua anapotupeleka hata kama sisi hatujui
Ni Alpha na Omega
Hata akiwa uchi tunatakiwa tusifie uzuri wa nguo zake
 
Naamini kuwa hata wapinzani walitoa ahadi kwenye majimbo yao pia, hivyo wanahitaji muda kutekeleza ahadi hizo,
There is no way you can separate politics from our normal routine of life!
Work and politics are inseparable, they are identical twins.
We need to understand this, unless we are out of our mind.
 
There is no way you can separate politics from our normal routine of life!
Work and politics are inseparable, they are identical twins.
We need to understand this, unless we are out of our mind.
Hata waingereza wanaweza kutofautisha siasa na maslahi ya nchi!
 
Common folks! Come back to your senses! You should learn to listen, it's a big task. Avoid over
Critisizing!
 
Hivi hata msajiri wa vyama vya siasa anawajibika kwa chama tawala?
Kweli hapa kasi tu.!!
 
Back
Top Bottom