Uchaguzi 2020 Jaji Mkuu: Ni marufuku kwa Jaji, Msajili wa Mahakama na Hakimu kujiunga na Chama cha Siasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,976
Jaji mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jaji wa Mahakama Kuu, Msajili wa Mahakama na Mahakimu kujiunga na Chama cha Siasa.

Profesa Ibrahim Juma amesema watumishi hao wa Mahakama wanabaki na haki moja tu ya kupiga kura waliyopewa katika Ibara namba 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: ITV Habari

=====


JAJI MKUU AWATAKA MAJAJI KUSOMA KANUNI ZA UCHAGUZI ILI KUTOA MAAMUZI KWA WELEDI NA KUTENDA HAKI

WhatsApp%2BImage%2B2020-08-17%2Bat%2B2.58.33%2BPM.jpeg


Jaji Mkuu Prof. Ibrahimu Juma akizungumza na maafisa wa mahakama takribani 282 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa maafisa wa mahakama kuelekea Uchaguzi.

WhatsApp%2BImage%2B2020-08-17%2Bat%2B2.59.12%2BPM.jpeg


Jopo la majaji wa Tanzania wakiwa na Jaji Mkuu Prof. Ibrahimu Juma kwenye mafunzo ya namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa maafisa wa mahakama takribani 282 nchi nzima.

WhatsApp%2BImage%2B2020-08-17%2Bat%2B3.00.07%2BPM.jpeg


Jaji kiongozi mahakama kuu ya Tanzania dkt. Elieza Feleshi akizingumza kwenye ufunguzi wa namna bora ya uendeshaji wa mashauri ya uchaguzi kwa maafisa wa mahakama takribani 282.

JAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amewataka Majaji na Mahakimu kusoma sheria na kanuni zote za Uchaguzi Mkuu, ili kutoa maamuzi ya mashauri ya uchaguzi kwa weledi na kutenda haki.

Jaji Prof. Juma, aliyasema hayo jijini Dodoma wakati alipokuwa akifungua mafunzo ya namna bora ya uendeshaiji wa mashauri ya uchaguzi kwa maafisa wa Mahakama wapatao 282.

Alisema kuwa, Majaji pamoja na wote watako pata nafasi ya kusikiliza mashauri ya uchaguzi mkuu 2020, wanatakiwa kuwa na uelewa mpana juu ya sheria pamoja na kanuni zitakazo tumika ili kutenda haki.

Pia, alisema maafisa wote wa Mahakama ambao watapata nafasi ya kuskiliza mashauri ya uchaguzi mwaka huu, wanatakiwa kutumia muda wao hivi sasa kuzisoma sheria pamoja na kanuni ili kujiongezea uelewa.

“Tunatakiwa kutenda haki kwa mashauri yote yatakayoletwa kwetu na kuyafanyia kazi ili kutoa maamuzi kwa weledi na kuzingatia haki kwa wale watakao onewa katika mchakato wa uchaguzi mkuu mwaka huu”alisema Jaji Prof. Juma

Alieleza kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo maofisa wa mahakama kutoa maamuzi kwa weledi na haki kwa wakati.

“Mahakama isionekane kupendelea upande fulani wa uchaguzi, bali Mahakama iisaidie Tume ya taiafa ya uchaguzi NEC, kuwapatia wananchi uchaguzi huru na wa haki, pia Majaji wajikite katika kusoma vifungu ambavyo vitawasaidia kutoa maamuzi yote ya mashauri ya uchaguzi kwa wakati”alieleza.

Vile vile, aliwataka maafisa wa Mahakama kushughulikia mashauri ya jinai wakati wa kamapeni, katika uchagumzi mkuu 2020.

“Makosa ya jinai ambayo mnatakiwa kuyashugulikia ni yale ya wakati wa kampeni pamoja na wakati wa kupiga kura makosa hayo ni kama vile kujiandikisha maeneo zaidi ya moja, kupiga kura katika kituo zaidi ya kimoja, kudanganya kitambulisho na mengine mengi.”Alibainisha

Aidha, aliwataka Majaji na Mahakimu, kuhakikisha kuwa hukumu za kesi zao wanazozitoa zinaandikwa kwa lugha nyepesi ili wanachi wazielewe.

Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Dk. Elieza Feleshi, alisema mafunzo hayo yameandaliwa na Mahakama ya Tanzania kwa kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa mahakama Lushoto (IJA).

Jaji Feleshi, alisema kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo maafisa wa Mahakama na kuwaandaa kutoa haki kwenye mashauri ya Uchaguzi Mkuu ujao wa Rais, Wabunge, na Madiwani.

“Duru ya kwanza ya mafunzo hayo inawahusisha waheshimiwa Majaji wa Mahakama kuu, Wasajili na Naibu Wasajili, Mahakimu Wakazi Wafawidhi wa Makahakam za Hakimu Mkazi”Alisema

Kadhalika awamu ya pili itawahususha Majaji wa Mahakama ya rufaa na yatafanyika Septemba 2 hadi 4 mwaka huu, mkoani Morogoro, Mahakimu wakazi Wafawidhi wa Mahakama za wilaya watapata mafunzo hayo baadaye katika chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto Tanga.
 
Ongeza wanajeshi,Polisi, usalama wa taifa, walimu, Nwa watumishi wote wa Umma hawatakuwi kufanya kazi kwa mlengo wa kisiasa ila wanabaki na Haki ya kupiga Kula

Hongera JWTZ na Mahakama kwa kujitenga na CCM mwaka huu.
Wanajeshi na Askari

Watumishi wengine ruksa isipokuwa wakati wa kazi kuwa neutral kutoa huduma
 
Jaji mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jaji wa Mahakama Kuu, Msajili wa Mahakama na Mahakimu kujiunga na chama cha siasa.

Profesa Ibrahim Juma amesema watumishi hao wa Mahakama wanabaki na haki moja tu ya kupiga kura waliyopewa katika Ibara namba 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: ITV Habari
simjui ila naona kasema vizuri na watakao jaribu wapigwe chini kama ambavyo niliwai sema watumishi walioenda kutia nia majimboni nao wapigwe chini wakatumikie siasa sawasawa maana mwaka huu wamezidi na haijawai tokea
 
Jaji mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jaji wa Mahakama Kuu, Msajili wa Mahakama na Mahakimu kujiunga na chama cha siasa.

Profesa Ibrahim Juma amesema watumishi hao wa Mahakama wanabaki na haki moja tu ya kupiga kura waliyopewa katika Ibara namba 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: ITV Habari

Je yeye ni mwanachama wa chama gani? Ha wa majaji si ndo wanateuliwa kuwaviongozi wa tume ya uchaguzi na kuibeba ccm?
 
Jaji mkuu Profesa Ibrahim Juma amesema ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jaji wa Mahakama Kuu, Msajili wa Mahakama na Mahakimu kujiunga na chama cha siasa.

Profesa Ibrahim Juma amesema watumishi hao wa Mahakama wanabaki na haki moja tu ya kupiga kura waliyopewa katika Ibara namba 5 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Chanzo: ITV Habari
Hizi ni Sarakasi zile zile..alitakiwa kuwaagiza wajivue uanachama kutoka vyama vya siasa kwani zaidi ya 50% ya Majaji&Mahakimu wa nchi hii wana kadi za CCM.Watakuja kujitetea baadae kuwa walioambiwa ni wale ambao hawajajiunga na sio kwa wale ambao tayari ni wanachama. Jaji Mkuu awe wazi kuwa wajivue uanachama kuanzia lea na akianzia na Hakimu Simba anayepewaga kesi za upinzani...
 
Back
Top Bottom