Chanzo cha taarifa ya Jaji huyo hakiwezi kuwa Chuo kikuu peke yake, hata shule ya msingi alikosoma zipo, shule ya sekondari, High school kote unaweza kupata taarifa hizo. Mtoa uzi kama angekuwa makini asingeishia chuo kikuu kitivo cha sheria peke yake.
Chanzo cha taarifa ya Jaji huyo hakiwezi kuwa Chuo kikuu peke yake, hata shule ya msingi alikosoma zipo, shule ya sekondari, High school kote unaweza kupata taarifa hizo. Mtoa uzi kama angekuwa makini asingeishia chuo kikuu kitivo cha sheria peke yake.
. Uzi sio wangu na sipendi na sina kawaida ya kudandia kazi ya mtu. Kama ameamua kutoa taarifa anapaswa kutoa taarifa iliyokamilika bila ya kuacha kipengere chochote. Tusizungumzie ushabiki, tuzungumzie uchambuzi unavyopaswa kuwa. Tusitoe maada yenye mapengo tukitumainia watu wengine kuziba. Mchango wangu katika maada ni kumwonyesha mtoa maada vyanzo vingine vya taarifa anakoweza kutoa ili kuikamilisha maada kiutafiti zaidi. Mtu anayedhani kuwa hizi ni lawama hajangalia kwa maana ya academic criticism anachukulia kama personal attack jambo ambalo sio sahihi. Sitoki nyumbani kwa Jaji Chande Omari wala sijasoma naye lakini pia sikuwa na nia yoyote ya kufuatilia maisha yake. Maadam mtoa maada kaitoa humu jamvini nimevutiwa nayo ndiyo maana nikamshauri atafute taarifa zaidi kutoka kwenye vyanzo vingine ili kuipa uzito, mvuto na ukweli zaidi bila ya kuacha nafasi kwa msomaji ya kuhoji au kupendekeza jambo lolote. Nimependekeza kwa sababu Uzi wake unatoa mwanya wa kufanya nilivyofanya. Ugomvi unatoka wapi? Nadhani mtoa uzi na waungaji mkono wa uzi huu walitegemea kila mtu apokee taarifa hii pasi na kuhoji kama walivyoipokea wao. HapanaYeye kwa uwezo wake amefika chuo kikuu, kama unaweza kufuatilia shule ya msingi, sekondari na a level itakuwa vizuri kuliko kumtwisha lawama zisizo na msingi wowote.
Asungwile Mwaifunga, tunapoleta mjadala kwenye JF, tunategemea wewe kama unatoka Kijiji alichosoma Jaji Mkuu, au kama upo mahalai alipozaliwa unasaidiwa watanzania wengine kujua.
Huu utaratibu wa kufikiri kuwa mpaka mtu aende kila mahali unakuwa hauna maana, nimeenda UDSMA, HAKUNA, WEWE ULIYEKO KIJIJI ALIKOZALIWA, AU WEWE ULIYESOMA NAYE AMBAYE HABARI ZENU SASA NI SIRI, NJO jamvini waambie watanzania Jins Jaji Mkuu alivyoanza darasa la kwanza akiwa na miaka 4, je kwa nyakat zile iliwezekana.
Hapo ndo huwa namkubali JK. Anakupa cheo huku anajua unanuka mavi, ukimzingua tu anakuanzishia soo..! Hapo ni nidhamu mwanzo mwisho..! Aliweza kum-set EL sembuse jaji mkuu..?