Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,067
- 22,760
Naam, ni kweli. Jaji Mkuu hakuweza kuendelea kuvumilia tuhuma zinazotolewa na Rais wa nchi dhidi ya majaji akihoji hukumu zinazotolewa katika kesi zinazofunguliwa dhidi yake. Kila mara Rais huyo amekuwa akiziponda hukumu hizo akidai zinatolewa na majaji walioteuliwa na Rais waliomtangulia ambao walikuwa na misimamo tofauti katika kutekeleza majukumu yao.
Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi anapata ujeuri wa kuingilia uhuru wa mahakama ambayo ni mhimili huru na kuhusisha hukumu zinazotolewa akihoji itikadi na uzalendo wa majaji hao. Jaji Mkuu amemtahadharisha Rais kwamba majaji wanatimiza majukumu yao kulingana na Katiba ya nchi inayolinda uhuru wa mhimili huo na kumtaka Rais azingatie hilo.
Kwa habari kamili bonyeza hapa: Chief Justice Roberts rebukes President Trump