Jaji Mkuu amkemea Rais na kumuonya kutoingilia uhuru na utendaji wa Mahakama!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,064
22,757
Naam, ni kweli. Jaji Mkuu hakuweza kuendelea kuvumilia tuhuma zinazotolewa na Rais wa nchi dhidi ya majaji akihoji hukumu zinazotolewa katika kesi zinazofunguliwa dhidi yake. Kila mara Rais huyo amekuwa akiziponda hukumu hizo akidai zinatolewa na majaji walioteuliwa na Rais waliomtangulia ambao walikuwa na misimamo tofauti katika kutekeleza majukumu yao.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi anapata ujeuri wa kuingilia uhuru wa mahakama ambayo ni mhimili huru na kuhusisha hukumu zinazotolewa akihoji itikadi na uzalendo wa majaji hao. Jaji Mkuu amemtahadharisha Rais kwamba majaji wanatimiza majukumu yao kulingana na Katiba ya nchi inayolinda uhuru wa mhimili huo na kumtaka Rais azingatie hilo.

Kwa habari kamili bonyeza hapa: Chief Justice Roberts rebukes President Trump
 
Naam, ni kweli. Jaji Mkuu hakuweza kuendelea kuvumilia tuhuma zinazotolewa na Rais wa nchi dhidi ya majaji akihoji hukumu zinazotolewa katika kesi zinazofunguliwa dhidi yake. Kila mara Rais huyo amekuwa akiziponda hukumu hizo akidai zinatolewa na majaji walioteuliwa na Rais waliomtangulia ambao walikuwa na misimamo tofauti katika kutekeleza majukumu yao.

Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni wapi anapata ujeuri wa kuingilia uhuru wa mahakama ambayo ni mhimili mwingine na kuhusisha hukumu zinazotolewa akihoji itikadi na uzalendo wa majaji hao. Jaji Mkuu amemtahadharisha Rais kwamba majaji wanatimiza majukumu yao kulingana na Katiba ya nchi inayolinda uhuru wa mhimili huo na kumtaka Rais azingatie hilo.

Kwa habari kamili bonyeza hapa: Chief Justice Roberts rebukes President Trump

Naona umejaribu kufanya ' Localization ' Mkuu.
 
Si useme ni Marekani. Sasa kwa kuificha ficha habari ili ionekane ni ya hapa nchini wakati unajua sivyo utakua umesaidia nini?

Unamlaumu mleta mada kwa matatizo yako!

Hakuna sehemu aliyoficha kwa sababu kama wewe ni msomaji mzuri basi unatakiwa kuisoma habari yote.

Hii thread inanifundisha kuna watu wanasoma heading halafu wanaanza kutoa comment. Hili ni tatizo kubwa sana nchini.
 
Nina uhakika bashite na jiwe wameingia kichwa kichwa kwenye uzi huu
 
Back
Top Bottom