don-oba
JF-Expert Member
- Dec 8, 2011
- 1,387
- 677
Minong'ono na wasiwasi vimetanda katika jiji la Arusha juu ya jarada la hukumu kupinga ubunge wa Lema kuvujishwa. Inasemekana mh Lema ubunge wake utatenguliwa hapo kesho pindi hukumu yake itakaposomwa. Jambo la kujiuliza, je imekuaje taarifa hii kuvuja? Tunafahamu miiko na taratibu za kimahakama, mojawapo ni weledi na ufanisi katika kutoa haki pasi kuangalia kipato cha mtu. Mwenendo wa kesi hii ulivyokuwa kwa sisi na kila mwanazuoni wa fani ya sheria tayari imetoa mwangaza wa hukumu yenyewe itakavyokuwa. Sitaki kuingilia uhuru wa mahakama bali tofauti na hapo, itaibua mjadala mkali katika mhimili huu muhimu. Mungu bariki mahakama zetu, mungu bariki Tanzania.