Jaji kesi ya Lema Arusha kashikishwa kitu na mafisadi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji kesi ya Lema Arusha kashikishwa kitu na mafisadi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Naloli, Apr 3, 2012.

 1. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Leo nimebahatika kutembelea Arusha mjini katika sehemu moja mitaa ya Mihanzini nilikuwa na jamaa zangu tukipata vinywaji na kutafakari mambo tofauti. Katika maongezi yetu tulijadili kwa muda mrefu USHINDI wa NASARI huko Arumeru East. Maongezi yetu yalivuta watu wa meza za jirani pia.

  Katika kujadiliana kwetu kuna jamaa wa meza ya jirani akaingia katika maongezi yetu katika kujadili kwake akaingiza jambo lililo nistua na kunigusa, Alisema, " EL na timu yake uhakika wa 90% kuwa Mpambanaji GODBLESS LEMA anang'olewa ktk UBUNGE kupitia hukumu ya kesi iliyopo mahakamani.

  Mdau huyo aliendelea kueleza kuwa taarifa hizo kazipata kwa jamaa yake(ndugu yake) wa UVCCM Arusha aliyekaribu na MILLYA, kuwa wameshamuweka Jaji sawa hivyo "Jogoo awike asiwike lazima kutakucha tu" yaani lazima LEMA ang'olewe.

  Nilishangaa kuona watu wengi wakiwemo na wenzangu wanazifahamu taarifa hizo na wanazungumza kwa uhakika na kuniambia wewe subiri HUKUMU ndipo utakapo amini tukisemacho. Wengine wakasema kuna sherehe imeshaandaliwa ya kujipongeza kwa kumng'oa LEMA. Na eti katika mashtaka dhidi ya LEMA walalamikaji wwameomba ikiwa mahakama itamuona LEMA ana HATIA afungiwe kushiriki siasa kwa miaka mitano. Hivyo katika uchaguzi mdogo CDM bila LEMA wamekwisha hivyo mtu wa EL atachukua JIMBO.

  Naomba nieleweke si lengo langu kuingilia UHURU wa mahakama au kumshinikiza jaji atoe matokeo yatakayo wafurahisha CDM au wananchi wanao muunga mkono LEMA hata kama alipotoka ktk kampeni.

  Je taarifa hizi Makamanda wa CDM hawana? kama wanazo wamejipanga vp? ni kweli wao wana PESA na sisi tuna MUNGU. Lakini inapobidi MAKAMANDA yapasa kutumia NGUVU YA UMMA kutoa HUKUMU kwa watumishi wanaopewa dhamana ya kutoa HAKI lakini wao wanaangalia MASLAHI ya KISHETANI.Si hamasishi machafuko au CDM wamtende vibaya Jaji akitoa Hukumu kinyume chao, lakini kama msingi wa hukumu ni fedha za EL, NGUVU YA UMMA IKIMUANGUKIA mimi nitaona sawa tu.

  MAANA SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU
   
 2. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii habari ilikuwepo tangu asubuhi ni tetesi ni kweli JAJI AMEKULA RUSHWA ILI LEMA, G ashindwe!
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  habari za baa zinafikaje jf?
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Kwa sababu zipi?
   
 5. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,781
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Kama suala ni hilo,mbona hata Arumeru walijihakikishia hvyo,lakini wameangukia pua?
   
 6. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 470
  Trophy Points: 180
  Kama ni kweli na huyo jaji akapindisha sheria kwa ajili ya pesa. Basi katika maisha yake yote yeye na familia yake awe na ulinzi kuliko hata wa rais Obama. Kwasababu atakuwa amewaumiza raia wengi wa Arusha kwa tamaa yake ya pesa hivyo lazima nae alipe.
   
 7. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Habari za baa na kupima upepo huwa hazina mashiko, kawaambie waliokutuma hukuwakuta wenyeji.
   
 8. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Kwa rushwa ya Tanzania sitashangaa. Watu wanashindwa kuheshimu profession zao na kukubali kudanganywa. Kazi hipo
   
 9. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  leteni vithibitisho jamvini, other wise its all ****, yaleyale ya cdm ikishinda najinyonga, tupunguze conspicuous theories, tusubiri hukumu! period.
   
 10. G

  George Katembo Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muosha huoshwa, lakini naamini ukweli utabaki palepale. Yule aliyeipigania arumeru east ndiye ataipigania arusha.
   
 11. MD25

  MD25 JF-Expert Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 3,078
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  P.umba tu hizi. Naona kilichowapata arumeru bado hakijawatosha.
   
 12. R

  Rugumisa Ben Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 31
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hello!
   
 13. t

  true JF-Expert Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 496
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  hizi habari ni za kweli mkuu! Zimetapakaa karibia Ars nzima.
  Jana asbh nilikuwa police upande wa ofc ya RPC, imagine maaskari wenyewe wanaliondelea hilo!!
  Na mmoja akawa anasema ni bora haya matukio yangejitokeza kwa cku moja. Yaani ushindi wa Joshua na hukumu ya Godless Lema.
  Na akasema hiyo alhamis kunawatu watakimbia mji! Mmoja wa askari akambana na kumuuliza ni kweli jamaa atapigwa chini? Huyo askari akastuka na kuniangalia na kusema mi sijui ww subiria hiyo alhamis.
   
 14. F

  Froida JF-Expert Member

  #14
  Apr 3, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Atajiabisha sana huyo Jaji kwa sababu hiyo kesi hata asiye kuwa Jaji anajua hakukuwa na kesi yeyote kwa sababu ushaidi ulipishana mno kati ya mashaidi hakuna hata mmoja aliyethibitisha yale waliodai
  Juzi nilikuwa kwa rafiki yangu kiongozi wa juu sana serikalini akanihakikishia kwamba Tundu Lissu,Mnyika,na Godbless watapigwa chini
   
 15. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #15
  Apr 3, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Toeni ujinga kesi yenyewe iko wapi au wewe hukuifuatilia nini.
   
 16. C

  Chinga boy JF-Expert Member

  #16
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hata mm kuna mshkaji wangu yupo Arsh alinijuza hiyo kitu na yule mama ashaitwa toka Kenya
   
 17. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Hiki chote ni kimbunga cha juzi mtaweweseka sana na bado.
   
 18. m

  mashimbamang'oma Member

  #18
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ila CCM watambue ya kuwa Hata Chadema ikimsimamisha dogo janja aliyerup siku ya kufunga kampen za Joshua na wao wakamsimamisha yule mama Chadema itashinda kwa kishindo Arusha... So kukwepa gharama zote watakazozitumia ni heri wajipange kwa ajili ya 2015 na sio kutumia plan B. Watu wa kaskazin hawadanganyiki tena na Magamba kifo chao kimeshafika hawana ujanja wala pakutokea....
   
 19. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nyie watu wa ccm jifurahisheni maana si tumesha wapiga kwenye uchaguzi arumeru sads mmegeukia maswala msyoyajua: nawaambieni sasa hata mahakamani tutaibuka kidedea, watu zaidi elf 57 waliomchagua Lema siyo wajinga, eti wafutiwe mbunge wao kwa issue za kihuni, huyo jaji athubutu aone!
   
 20. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lema, Mnyika na Lisu .........hawa wote wakipigwa chini nitajua kuwa kweli Tanzania haina demokrasia na nchi imo mikononi mwa wachache na hatutakuja tuendelaa hadi damu imwagike sana ndio watafurahia au hadi waaibike kama bagbo ndio watatuia akili ila bila hivyo wataendelea kujiona kuwa wapo juu ya sheria na wana nguvu kuliko umma
   
Loading...