Jaji kesi ya Lema Arusha kashikishwa kitu na mafisadi?

wangekuwa na akili wasingefikiria, japo kufikiria tu, kutengue ubunge wa kiongozi wa watu wa arusha. kuna sehemu wanaweza kufanya upuuzi huo na wakaachwa tu, cyo sehemu kama Arusha.

hawa jamaa hawajifunzi kabisa inaelekea.
wamuconsult Mr. Trasias Kagenzi awaambie ubaya wa wanachokusudia kukifanya
 
Minong'ono na wasiwasi vimetanda katika jiji la Arusha juu ya jarada la hukumu kupinga ubunge wa Lema kuvujishwa. Inasemekana mh Lema ubunge wake utatenguliwa hapo kesho pindi hukumu yake itakaposomwa. Jambo la kujiuliza, je imekuaje taarifa hii kuvuja? Tunafahamu miiko na taratibu za kimahakama, mojawapo ni weledi na ufanisi katika kutoa haki pasi kuangalia kipato cha mtu. Mwenendo wa kesi hii ulivyokuwa kwa sisi na kila mwanazuoni wa fani ya sheria tayari imetoa mwangaza wa hukumu yenyewe itakavyokuwa. Sitaki kuingilia uhuru wa mahakama bali tofauti na hapo, itaibua mjadala mkali katika mhimili huu muhimu. Mungu bariki mahakama zetu, mungu bariki Tanzania.


Kesho Mahakama itatoa hukumu ya haki, na kwamba Kamanda Lema ataendelea na ubunge bila maneno. Siyo kwamba tunaingilia uhuru wa mahakama, bali mwenendo wa kesi ulivyokuwa.
Ninachoweza kusema ni kwamba mara baada ya kutoka mahakamani kesho wapenzi wote wa CDM tutakutana NMC kufurahia ushindi wa kesi dhidi Dhuluma.
NMC patakuwa hapatoshi.
Musa Mkhanga na wenzake wajiandae kulipa gharama za kesi, maana walimsababishia Lema badala ya kuwatumikia wananchi akawa anahudhuria kesi ya Kipumbavu isiyokuwa na maana yoyote.
 
Sawa (CCM) wafanye tu wao si wenye dola na hela.....sisi (CHADEMA) tuna Mungu tuone mwisho
 
Hata kama jaji kapokea rushwa lakin kwa sababu tulianza na Mungu na tutamaliza na Mungu, ushindi u kati yetu kwa maana kama Mungu yupo upande wetu ni nani atakayetushinda. Hukumu kinyume na matarajio ya nguvu ya umma itabadilisha jina la jaji.
 
Leo nimebahatika kutembelea Arusha mjini katika sehemu moja mitaa ya Mihanzini nilikuwa na jamaa zangu tukipata vinywaji na kutafakari mambo tofauti. Katika maongezi yetu tulijadili kwa muda mrefu USHINDI wa NASARI huko Arumeru East. Maongezi yetu yalivuta watu wa meza za jirani pia.

Katika kujadiliana kwetu kuna jamaa wa meza ya jirani akaingia katika maongezi yetu katika kujadili kwake akaingiza jambo lililo nistua na kunigusa, Alisema, " EL na timu yake uhakika wa 90% kuwa Mpambanaji GODBLESS LEMA anang'olewa ktk UBUNGE kupitia hukumu ya kesi iliyopo mahakamani.

Mdau huyo aliendelea kueleza kuwa taarifa hizo kazipata kwa jamaa yake(ndugu yake) wa UVCCM Arusha aliyekaribu na MILLYA, kuwa wameshamuweka Jaji sawa hivyo "Jogoo awike asiwike lazima kutakucha tu" yaani lazima LEMA ang'olewe.

Nilishangaa kuona watu wengi wakiwemo na wenzangu wanazifahamu taarifa hizo na wanazungumza kwa uhakika na kuniambia wewe subiri HUKUMU ndipo utakapo amini tukisemacho. Wengine wakasema kuna sherehe imeshaandaliwa ya kujipongeza kwa kumng'oa LEMA. Na eti katika mashtaka dhidi ya LEMA walalamikaji wwameomba ikiwa mahakama itamuona LEMA ana HATIA afungiwe kushiriki siasa kwa miaka mitano. Hivyo katika uchaguzi mdogo CDM bila LEMA wamekwisha hivyo mtu wa EL atachukua JIMBO.

Naomba nieleweke si lengo langu kuingilia UHURU wa mahakama au kumshinikiza jaji atoe matokeo yatakayo wafurahisha CDM au wananchi wanao muunga mkono LEMA hata kama alipotoka ktk kampeni.

Je taarifa hizi Makamanda wa CDM hawana? kama wanazo wamejipanga vp? ni kweli wao wana PESA na sisi tuna MUNGU. Lakini inapobidi MAKAMANDA yapasa kutumia NGUVU YA UMMA kutoa HUKUMU kwa watumishi wanaopewa dhamana ya kutoa HAKI lakini wao wanaangalia MASLAHI ya KISHETANI.Si hamasishi machafuko au CDM wamtende vibaya Jaji akitoa Hukumu kinyume chao, lakini kama msingi wa hukumu ni fedha za EL, NGUVU YA UMMA IKIMUANGUKIA mimi nitaona sawa tu.

MAANA SAUTI YA WENGI NI SAUTI YA MUNGU



Basi itakuwa miujiza kama kwa mwendo huu hapo chini Lissu atashindwa:-Kesi ya kupinga matokeo ya Lissu yaibua mambo mazito.
Chiligati atajwa kuhusika kuandaa ushahidi,
Mrema na mwanae watumika kusaidia CCM kumpinga Lissu,
Mashahidi waingia tena mitini, jaji aamuru walipe gharama.
Josephat isango- Singida.
Kesi ya kupinga matokeo ya Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya CHADEMA jana iliibua mambo mapya, baada ya mshitakiwa Tundu Lissu kutoa waraka Mahakamani ulioandikwa na John Chiligati kuomba ufafanuzi namna TLP ilivyoshiriki katika uchaguzi Mkuu wa 2010.
Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo Tanzania daima inayo, yenye kumbukumbu namba CCM/OND/559 Vol.II/10, ya tarehe 23/03/2011. John Chiligati aliomba kujua kama kweli TLP iliweka mawakala katika Jimbo la uchaguzi wa singida mashariki, au kama mihuri iliyotumika ya TLP ilikuwa ni sahihi au ni ya kughushi,

Kufuatia barua hiyo, barua nyingine ya majibu kwa Chiligati, iliyotolewa mahakamani hapo na Tundu Lissu ilitoka kwa Hamadi R. Tao, aliyekuwa naibu katibu Mkuu TLP, yenye kumbukumbu Namba TLP/HQ/HAB/VOL.V/165, Ilisema Ni kweli mawakala wa TLP hawakuteuliwa au kama waliteuliwa utaratibu wa uteuzi haukufuata taratibu za Chama. Barua hiyo ya TLP ilipingana vikali sana na barua ya Mwenyekiti wa TLP, wilaya ya singida, iliyoandikwa kumjibu Katibu wa taifa wa TLP, ya tarehe 12/04/2011, ilisema kuwa Chama cha TLP kiliweka mawakala kusimamia katika uchaguzi Mkuu bila malipo.
Hata hivyo mjadala wa mahakamani ulikuwa Mkubwa, baada ya Shahidi wa 19, Bw. John Madindilo, ambaye ni Mwenyekiti wa TLP Mkoa wa singida kukubaliana na hoja zote za Lissu, na alimtaja Mtoto wa Augustino Mrema, anayeitwa Michael Mrema kuwa alitumwa singida kama afisa wa Chama kwenda kufuatilia suala hili, na alipopewa taarifa hiyo, hakuridhika nayo badala yake aliwalelekeza wale viongozi wa Singida, kuandika barua kwa Katibu Mkuu kadiri itakavyompendeza Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema.
Baadhi ya mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo: Baina ya tundu Lissu na SHAHIDI, JOHN MADINDILO
T/L Ni kweli au si kweli kuwa ulikasimu madaraka kwa Mwenyekiti wa TLP wa wilaya ya Singida, kwa kuwa wewe ulikuwa Mgombea, na Mwenyekitji wa Wilaya ya singida, ulimwamini, kwa uwezo wake na uadilifu , na uzoefu wake?
P/W:NDIYO NILIFANYA HIVYO LAKINI YEYE PIA YUPO MAKAO MAKUU YA MKOA HAPA MJINI.
T/L Ni kweli au si kweli kuwa mliweka mawakala kulinda maslahi ya Chama,
P/W NI kweli,
T/L Ni sahihi au siyo sahihi, mnapokuwa na Mgombea urais, huwa mnaweka mawakala?
P/W NI KWELI, pale ambapo mawakala wanakuwa tayari kujitolea.
T/L Ni kweli au si kweli kuwa kwa mujibu wa barua ulizo nazo, kesi hii ipo kwa maslahi ya Chiligati na Mrema?
P/W Ni kweli kwa mahusiano ya barua hizi walizoandikiana.
T/L Kama nimekusikia vizuri uliiambia mahakama hii kuwa kuna Afisa wa Chama anakuja toka Mkao makuu, umpokee na umpe ushirikiano?
P/W NI kweli.
T/L Je huyo afisa wa chama alikuwa anaitwa nani?
P/W: Siruhusiwi kumtaja
JAJI: Kama umemtaja Augustino Mrema, Mwenyekiti wa TLP Taifa ni Afisa gani unashindwa kumtaja
P/W: ni Mikaeli Mrema.
T/L. Mikaeli Mrema ambaye ni mtoto wa Augustino Mrema?
W/P.NDIYO
T/L. Mikaeli Mrema alisema nini?
P/w; alisema kuwa kulikuwa na mawakala hewa wa TLP waliwekwa Singida mashariki?
T/L. Hukushangaa kupokea taarifa ya Malalamiko toka makao makuu wakati wewe Mwenyekiti wa Mkoa huna taarifa yeyote?
P/W: NILISHANGAA SANA lakini nilipokea kwa kuwa inatoka kwa Mkubwa wangu wa Kazi.
T/L: Nimeshtakiwa hapa, kwa mujibu wa barua mbalimbali ulizosoma, wanaitaka Mahakam itengue matokeo ya uchaguzi, kwa mujibu wa ufahamu wako, unasemahe juu ya hili?
P/W: watakuwa wanakuonea.
Kesi hiyo haikuendelea mchana, baada ya upande wa walalamikaji kushindwa kuleta Mashahidi mahakamani, kitendo kilichopelekea jaji kuwapiga faini ya kulipa nusu gharama ya siku katika kesi hiyo:
Na mahojiano yalikuwa hivi:
Wakili wa walalamikaji; Mheshimiwa jaji, naiomba Mahakama iahirishe kesi hii hadi kesho kwa kuwa shahidi wetu hajaja, na amefunga simu,
JAJI: Ulichukua hatua kuleta shahidi mmoja tu?
Wakili: huwa tunachelewa kutoka mahakamani, hivyo inakuwa vigumu kuwatafuta kwa siku inayofuata. Hata hivyo kazi ya kutafuta mashahidi sio yangu ni ya wateja wangu.
TUNDU LISSU: Mheshimiwa jaji, uchelewashaji unaofanywa kwa makusudi unaniathiri mimi, kwanza kiuchumi kwa kuwa nakaa hotelini, pili ninashindwa kushiriki kazi za kibunge, na ninashindwa kuwatumikia wanachi wangu walionichagua. Siku nyingine ulinionya nisidai gharama, leo mheshimiwa jaji, naomba upande wa walalamikaji walipe gharama,
Jaji: Mlalamikaji naomba usimame, unajua kuwa katika kesi hii mimi nalipwa na serikali, na hawa wanasheria watatu wa serikali, na katibu wangu?
MLALAMIKAJI: NDIO,
JAJI: mbona hampo ‘serious’ . Kuna uzembe mkubwa unatokea na leo hii sitaki kukubali kirahisi uzembe huu. Kuna uzembe unafanywa na walalamikaji, na tayari nilionya hili tangu mwanzo. Mtumzembe hukumbushwa na leo naamuru mtalipa nusu gharama ya ahirisho la kesi leo kwa uzembe wenu ili mjitume na mjue wajibu wenu sio kutupotezea muda hapa.
 
hivi mambo ya rushwa bado yana nafasi arusha? mbona naona kama njia mbala ya rushwa ambayo inakemewa na watu wote haina mashiko tena

na kama itatokea basi chama tawala kinajiweka ktk wakati mgumu sana

huwezi mlazimisha punda kunywa maji
 
Wanabodi,
Kesho Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ndio inatoa hukumu ya shauri la madai inayoomba Lema avuliwe ubunge.

Katika shauri hilo linalotarajiwa kuvuta hisia za wengi, Lema anadaiwa kutoa lugha za matusi, kafsha na udhalilishaji dhidi ya Dr Batilda.

Wadai hao wameita mashahidi 14 kuthibitisha tuhuma zao mbele ya Jaji Gabriel Rwakibarila.

Katika hoja zao za majumuisho yaliyowasilishwa na mawakili wao wamesisitiza maombi ya kuvuliwa ubunge Lema na wao kulipwa gharama za shauri hilo na malipo mengine yatakayoamriwa na na mahakama.
 
Hatima ya lema imeshajulikana kilichobaki ni modality tu, lema alimdhalilisha sana yule dada wa watu, avuliwe ubunge ili CCM irudishe heshima iliyopotea ARUMERU.
 
Inavyoonekana hakuna hata mmoja wenu aliekoment anyejua uhuru wa mahakama nini, mahakama haihukumu kishabiki, wala usitegemee unachokiwaza pekee kitendeke ndio uone kuwa haki imetendeka. Mimi binafsi nilikuwa nahudhuria mikutano ya uchaguzi ya Lema, hakuna kampeni za kipuuzi na kihuni kama zake. This guy hafai kuongoza hata kundi la machizi. Tokea kaingia madarakani what did he do mpaka sasa, kuna kilichoongezeka hapo mjini arusha zaidi ya kupungua kwa watalii kutokana na siasa chafu alizoziendesha yeye, hakuna haja ya kukumbatia watu kama yeye wanaotuletea hasara badala ya faida, uhuni hauna nafasi kwa nchi ya wastaarabu kama hii. Wote tunapenda mabadiliko lakini si katika hali ya kihuni, tufuate utaratibu na kufanya siasa safi sio CDM au CCM au CUF. Tunahitaji sera na si uhuni. Sitashangaa Lema akishinda au akishindwa kwani moja wapo kati ya hayo lazima yatokee na mahakama itakuwa imetenda haki. Kusema kuwa Jaji kapokea rusha this statement is baseless and ungrounded..huwezi niambia jaji kama huyu mwenye uzoefu apokee rushwa kwa kesi kama hiii ambayo jamii nzima wanasubiri matokeo yake, judiciary pia kabla ya kuteua majaji wanaangalia sifa za jaji na uzito wa kesi. Stori za baa hazina nafasi mahali hapa, kaongeeni na walevi wenzenu huko baa.

What did he do????mkuu Watanzania wengi wanajua uhuru wa mahakama na umuhimu wa vyombo vya dola,tatizo hizi taasisi zimekua zikifanya kazi kwa maelekezo zaidi na si kutokana na matakwa ya taaluma husika!kuna Mtanzania hasiyejua kua polisi au mahakamani pananuka rushwa?mpaka mkuu wa nchi mwenyewe anayajua hayo na uwa anakemea!sasa wewe utalazimisha vipi kuwalisha ujinga Watanzania kua mahakama zetu za Tanzania ziko fair sana katika maamuzi yake!unapowa aminisha watu kua eti jaji kama huyu ni mzoefu na hawezi pindisha sheria huo ni uongo na upofu uliotukuka,unakumbuka aliyekua Judge mkuu wa nchi Mh .A Ramadhani alisema nini baada ya kustaafu?kuna baadhi ya kesi alikua anapindisha sheria kutokana na maelekezo ya wakubwa,na alikiri wazi hiko ni kitu kitakacho muumiza sana maishani mwake kwa kua hakuitendea haki taaluma yake!na baada ya kauli hiyo serikali ilichukia na kumnyang'anya ulinzi judge huyu kama wanavyopewa majaji wakuu wengine wastaafu mpaka wadau walipopiga kelele sana,kwa aibu ikabidi wamrudishie ulinzi,suala la Lema kutukana mimi sijui maana sikuwahi kuudhuria mikutano yake,na wala sikua kuona video/clip yoyote juu ya ilo kama nilivyoiona ya Lusinde!kuhusu watalii kupungua,nafikiri wewe na waziri mkuu mstaafu mnataka kuwaaminisha Watanzania ujinga,au ninyi wenyewe ni wavivu wa kuhusisha vichwa/akili katika kufikiri na kuyajua yanayoendelea duniani!hv ni nani hasiye jua kua sekta ya utalii iliyumba sana duniani kote kutokana na mtikisiko wa uchumi duniani?hata wizara ya maliasili imelisema ilo mara kadhaa!Arusha ni vurugu gani iliyotokea eti mpaka iathiri utalii wa Arusha?unanichekesha sana mkuu,kama wewe ni kijana!jaribu kushirikisha zaidi ubongo katika hoja zako kwa jamihi,kuliko hisia zako!otherwise ndio tunarudi kwenye kauli kua we should thank a stupid person for their contribution,maana without a stupidy people we would have no one to laugh at!
 
Hatima ya lema imeshajulikana kilichobaki ni modality tu, lema alimdhalilisha sana yule dada wa watu, avuliwe ubunge ili CCM irudishe heshima iliyopotea ARUMERU.

Ya arumeru mashariki haijawafunza, tafuteni by election arusha mpate aibu ya karne!!!!!
 
Magamba bana!! Mtatumia nguvu nyingi kusaka madaraka, baadae mkipata mnavimbiwa na mnajisahau...yule mama si keshapewa ubarozi kenya...ameshaenda?? Kuvuliwa ubunge Lema ni sawa na Ritz kupenya kwenye ncha ya komeo!!
 
Huyo jaji namfahamu si mtu wa rushwa ila binadamu hawatabiriki. Kwa vyovyote wakipigwa chini waende mahakama ya rufaa kwa kuwa wanakaa majaji watatu itakuwa ngumu sana kwa CCM wale wazee wa court of appeal hawahongeki
 
ni rahisi sana kutengua ubunge wa mwenyekiti wa CDM mh. mbowe kuliko kutengua ubunge wa Mh. G.lema.
 
Huyo dada aliyedhalilishwa yuko wapi katika kesi hii?
Acha kuongea kwa hisia, hata mashahidi walioletwa mahakamani walishindwa kuthibitisha tuhuma dhidi ya Lema.
Lema ni Mbunge wa Arusha na ataendelea kuwa Mbunge wa Arusha Mjini na Waziri kivuli wa Mambo ya Ndani.
Kesho tunasherehekea ushindi amini maneno yangu. Mahakimu/majaji wamechoka kuingiliwa uhuru wao na washenzi, sasa wameamua kutoa hukumu ya haki.
Mungu ibariki Tanzania
Mungu Ibariki CHADEMA
Mungu Ibariki Arusha
Hatima ya lema imeshajulikana kilichobaki ni modality tu, lema alimdhalilisha sana yule dada wa watu, avuliwe ubunge ili CCM irudishe heshima iliyopotea ARUMERU.
 
Wanabodi,
Kesho Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ndio inatoa hukumu ya shauri la madai inayoomba Lema avuliwe ubunge.

Katika shauri hilo linalotarajiwa kuvuta hisia za wengi, Lema anadaiwa kutoa lugha za matusi, kafsha na udhalilishaji dhidi ya Dr Batilda.

Wadai hao wameita mashahidi 14 kuthibitisha tuhuma zao mbele ya Jaji Gabriel Rwakibarila.

Katika hoja zao za majumuisho yaliyowasilishwa na mawakili wao wamesisitiza maombi ya kuvuliwa ubunge Lema na wao kulipwa gharama za shauri hilo na malipo mengine yatakayoamriwa na na mahakama.

Kama hata ndoa ameshindwa kukidhi vigezo hadi kutwangwa talaka tatu!!!!! unataka kutuambia batilda buriani anaheshima gani kwa jamii, umepaswa kujua kuwa huyu mama ni muhuni, kama vipi nenda zenji kaulize.
 
Back
Top Bottom