Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 638
- 1,771
Akijibu swali la mwandishi kuhusu uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Stergomena Tax, kujiunga na tume ya kuchunguza yaliyotokea wakati wa uchaguzi pamoja na kuwepo kwa tuhuma kwamba Jeshi analolisimamia lilihusishwa na mauaji ya waandamanaji, mwenyekiti wa tume hiyo Jaji mkuu mstaafu othman Chande ameeleza kuwa mamlaka ya kuteua wajumbe wa tume ni ya Rais kisheria. Kwa msingi huo, Rais ndiye mwenye uwezo wa kufanya maamuzi na kuzingatia vigezo anavyoona vinafaa katika uteuzi huo.