CHADEMA Haina Mtu Anayeweza Kushindana na Rais Samia katika Sanduku la Kura uchaguzi Ujao

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,327
9,748
Ndugu zangu watanzania,

Huo ni ukweli japo unaweza kuwa mchungu kwa mashabiki na wafuasi wa chama hicho kilichopoteza ushawishi, nguvu, muelekeo, Dira, uungwaji mkono na imani kutoka kwa mamilioni ya watanzania.Hakuna mtu au kiongozi ndani ya chadema mwenye Ubavu au uwezo wa kushindana na Rais samia katika sanduku la kura.

Kwa Akili Timamu za watanzania ni nani anayetosha kupewa u Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama wa Taifa letu kutoka Chadema.

Nani na kiongozi gani ndani ya Chadema mwenye kifua cha uongozi,haiba ya urais,mdomo wa urais anayeweza kuzungumza na watanzania wakamsikiliza ,kumtii na kumuunga mkono? Nani kutoka ndani ya chadema anayeweza kuungwa mkono na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama? Nani anayeweza kulinda amani na utulivu wa Taifa letu? Nani kutoka Chadema mwenye uwezo wa kuwaunganisha watanzania bila kujali itikadi za kisiasa, Dini, kabila, jinsia au kanda?

Nani kutoka Chadema anayeweza kuwaongoza watanzania na kuwapenda na kuwatumikia wote kwa usawa wote waliomchagua na ambao hawajamchagua na kujuwa wote ni wananchi wake wanaohitaji huduma sawa na Haki sawa? Nani anayeweza kuungwa mkono na akakubalika na kuungwa mkono na watanzania wa Dini zote, kanda zote, makabila yote, rika zote, jinsia zote na makundi yote?

Ni nani huyo? Yupo wapi kwa sasa? Nani kutoka Chadema mwenye kujuwa kuchunga ulimi na mdomo wake na kujuwa athari za matamshi yake kama mkuu wa nchi? Ikumbukwe ya kuwa kuongea sana kwa kuropoka na kukurupuka hakukupi sifa ya kuwa Rais wa nchi ,kwa Kuwa urais unahitaji mtu mtulivu,mwenye busara,hekima, unyenyekevu, utu, jasiri, shupavu, madhubuti, imara, mwenye misimamo,maono na akili kubwa ya kuweza kuwaza na kuona na kuwa mbele ya wakati na kutazama mbele ya wale unaowaongoza,mwenye uwezo wa kuvumilia na uvumilivu wa mambo magumu na mazito, mwenye kujuwa wakati gani uzungumze na wapi akae kimya,wapi atoe tamko na wapi anyamaze, afanye nini na wakati gani? Nani mwenye uwezo huo kutoka Chadema?

Mara ngapi mmesikia Lissu akiropoka,kutukana ,kuwagawa watu kwa misingi ya ukabila, u vyama,Udini,ukanda na hata jinsia? Mara ngapi mmesikia akisema maccm au mapoliccm? Sasa nani wa kumuunga mkono mtu wa namna hii? Mara ngapi amewatusi na kuwatukana wale asio kubaliana nao mitizamo juu ya jambo fulani? Sasa vipi ataongoza Taifa lenye watu wa mitizamo ya aina mbalimbali na Elimu tofauti tofauti?

Urais unahitaji kifua cha utunzaji wa siri,Nani ndani ya chadema mwenye uwezo wa kutunza siri za Taifa pasipo kupasuka kifua? Ikumbukwe mkuu wa nchi ni mtu anayekuwa anajuwa siri nyingi na mambo mengi ya taifa letu, sasa nani mwenye uwezo wa kubeba mambo mazito katika kifua chake kutoka ndani ya chadema? Nani mwenye maono ya uongozi kutoka ndani ya chadema? Nje ya katiba ni lini umewahi kumsikia Lissu akiongea na kuonyesha falsafa yake ya masuala ya kiuchumi na vipi atakuza uchumi au ni vipi atajenga uchumi jumuishi unaogusa maisha ya watanzania wengi?

Mtu gani ndani ya chadema mwenye haiba au hadhi ya kumpeleka white house Marekani akafanye mazungumzo na Joe Bideni au Kamala Harris au Emmanuel macron au kwenda kuzungumza na wawekezaji na makampuni ya kitalii kutoka Marekani yaje kuwekeza nchini na kuleta watalii? Hivi kweli kwa akili za kawaida inaingia akilini kuwa Salumu mwalimu ndio angekuwa kweli makamu wetu wa Rais? Inaingia akili kweli hii? Hivi kweli chadema wapo sirias Kweli? Au wanadimba dimba tu?

Chadema ifute na kuondoa kabisa wazo la kuweka mgombea urais uchaguzi ujao na badala yake ijikite katika kutafuta idadi ya wabunge na madiwani tu,nje ya hapo itakuwa inapoteza muda wake tu kuweka mgombea Urais, maana ataishia kuwa sinema majukwaani na kituko cha mtaa,kwa kuwa hakuna mwenye akili Timamu awezaye kuwapa kura ya Urais chadema. Hilo lipo wazi kabisa mkubali au kuukataa ukweli huu lakini bado itabakia kuwa ndio ukweli wenyewe, kuwa hakuna mwenye ubavu wa kushindana na Rais samia na CCM Katika sanduku la kura katika nafasi ya Urais wa Taifa letu.

Kama hamtaki na mkashupaza vichwa vyenu mjue ya kuwa mtaishia kukatika tu shingo zenu na kuvuna aibu ya karne.ninyi bado ni wachanga na hamjawa na safu yenye kuleta matumaini na kuaminika mbele za watanzania.ndio maana unaona akina Dr Slaa leo Hawapo tena nanyi wala akina mh lowassa au sumaye. maana Bado hamjakomaa na kuiva kiuongozi na hakuna anayeweza kuja kuwa meza moja na watu kama akina Mdude nyagali ambaye akifungua mdomo na kinywa chake mpaka unaona aibu unaye msikiliza maana unakuwa huelewi kama kavuta bangi au kuna mahali kichwani pamelegea.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa,kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Hata wewe na bila chama unaweza shindana na wanakijani na ukawaondosha kwa ko tena round ya kwanza tu😂😂😂
 
Ndugu zangu watanzania,

Huo ni ukweli japo unaweza kuwa mchungu kwa mashabiki na wafuasi wa chama hicho kilichopoteza ushawishi ,nguvu,muelekeo ,Dira ,uungwaji mkono na imani kutoka kwa mamilioni ya watanzania.Hakuna mtu au kiongozi ndani ya
Nani kakwambia atagombea?

HATOGOMBEA!!
 
Back
Top Bottom