Ivory Coast hiyoooo Nusu Fainali AFCON kwa kuifunga Mali magoli 2-1

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Licha ya Timu ya Taifa ya Ivory Coast kucheza pungufu kuanzia kipindi cha kwanza dhidi ya Mali katika Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, bado hiyo haikuwa kikwazo cha kuingia Nusu Fainali kwa kushinda magoli 2-1, Februari 3, 2024.

Ivory Coast ilimpoteza Odilon Kossounou aliyepata kadi nyekundu dakika ya 43, kisha Nene Dorgeles akaipatia Mali goli dakika ya 71, wenyeji wakasawazisha dakika ya 90 kupitia kwa Simon Adingta, baada ya hapo Oumar Diakite akafunga la pili katika dakika za 30 nyongeza (120).

Hivyo, Ivory Coast itacheza dhidi ya DR Congo katika Nusu Fainali, Februari 7, 2024.
 
Mali wamekosa mentality ya kudeal na wapinzani , mpinzanij yupo pungufu na anakupeleka mchaka mchaka na wewe unakubali badala ya kutuliza mpira, icho ndo kimewagharim, mana wamecheza mpira anao taka mpinzani
 
Tanzania vs Zambia au umejizima data?
 
Back
Top Bottom