AFCON: Senegal yaingia Hatua ya 16 Bora wa kuipiga Cameroon magoli 3-1

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Timu ya Taifa ya Senegal imefanikiwa kuingia Hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), leo Januari 19, 2024 kwa kuifunga Cameroon magoli 3-1, hivyo kufikisha pointi 6 katika Kundi C ikiwa imesaliwa na mchezo mmoja.

Magoli ya Senegal yamewekwa wavuni na Ismaila Sarr, Habib Diallo na Sadio Mane wakati lile la Cameroon likifungwa na Jean-Charles Castelletto.

Michezo ya mwisho Hatua ya Makundi kwa timu hizo, Senegal itacheza na Guinea huku Cameroon yenye pointi moja ikitarajiwa kucheza dhidi ya Gambia.
 
Ikitokea egypt amekutana na hawa miamba sioni ni namna gani atatoboa
 
Rigobert Song kaishiwa mbinu ifike mahali Cameron Ibadilishe mwalimu. Hata word cup jamaa walikuwa tia maji tia maji.
 
Back
Top Bottom