Ivona Kamntu - Mtangazaji anayemiliki vyema kamera

Miwatamu

JF-Expert Member
Oct 2, 2012
1,450
487
wana Jamvi habari,

Nimeamua kuandika thread hii baada ya kukutana na lalamiko la mwana jamvi mwenzetu akimlalamikia mtangazaji huyu kuwa anajiona awapo kwenye kazi yake ya utangazaji.

Ukweli ni kuwa; mbali ya pozi zake awapo mbele ya kamera, lakini ni mtangazaji kati ya wachache tulionao hapa nchini anayeweza kutengeneza sentensi na kujua jinsi ya kuifikishwa kwa jamii na kila mtu akaelewa kile anachokisema. kwa maana nyingine, ni kuwa huyu ni mtangazaji mahiri sdana katika fani hii.

Labda kwako wewe unayekereka na aina ya utangazaji wake, nitakuongezea watangazaji wengine wa aina yake kwa uchache;

Salim Kikeke - BBC
Samadu Hassan - Star

Kwa ufafanuzi huu naomba niseme kuwa hoja ya ndugu yangu hapa chini haina mashiko.

By. Mtazamaji huru.

TV Huyu mtangazaji Wa star tv


Wanajamvi,Leo natoa dukuduku langu hasa kwa mtangazaji VYONA KAMUNTU Wa star Tv,apunguze malingo na kujisikia pale anapokuwa Anatangaza pale Luninga ya star Tv,kwani anajibinuabinua utadhani kuna Mtu Ana mlingishia sura yake,Ajirekebishe ,mbona watangazaji wenzake wanatangaza vema?au anajiona kuwa yeye ni mrembo zaidi?Anakera sana huyu Dada,
 
ni kwel anajua kutangaza na anamvuto akiwa anatangaza. ila kuna mishebeduo flani inazidi kipimo apunguze,jamaa aliyelalamika yuko sahihi
 
Kusema kwel kama mnamsema vibaya ni kwa roho mbaya zenu ila mim namkubali sana Ivona na nampa big up akiendelea hivyo atafika mbali sana
 
Jamani watanzania na chuki binafsi tumezidi. mdada anaipenda kazi yake na anaifanya ipasavyo na hicho ndo kinatakiwa. lazima mtu uwe mbunifu katika kazi ili ufike mbali. basi wasemeni na akina salim kikeke, kasim kayila wa bbc bila kumsahau lee yung xinhua wa CCTV. BIG up kwa Ivona K!!
 
Mimi aliniudhi jana, alivyomwambia mnyika eti asimseme ndugai kwa kuwa hayupo studio, pia kuwasema waz waz mafundi mitambo wake kwa nn hawarekebishi sauti....huku akikunja ndita...binafsi naona apunguze kujisikia.
 
Ni kadada kazuri njooni kwao ukonga hapo ndo mtajua kuwa anaringa ama vip mm naona yuko kawaida tu
 
Ebwana kuna dada flani alikuwepo star tv miaka ya 2006 hadi 2009 mrembo kweli alikuwa ana kipindi cha urembo na pia alikuwa anatangaza taarifa za habari simuoni siku hz kaenda wapi? Ana rangi ya chocolate na macho kama kala kungu.
=====================
Ukipata Ujumbe wa chuki matusi futa delete kabisa
=====================
 
mimi huwa naona havai mavazi ya kike, anavaa mashati na ana posi za kiume. sisemi kuwa ni msagaji lakini posi zake ni za kiana fulani hivi, halafu anaongea polepole sana haongei harakaharaka ili kusevu muda wa tv, anapoteza muda kutoa mimacho na kujifanya anaongea point kumbe anaboa. ukimwangalia kwa makini, anaweza kuwa alikulia kwenye familia ya watoto 5 wa kiume na wakike akiwa peke yake, ana element fulani hivi ambazo huwa zinanitia kichefuchefu. huo ndio ukweli toka moyoni mwangu. si unajua mimi nachukia sana wasagaji na mashoga...
 
Ni kweli mtoa mada yuko sahihi aache kujishebedua anapotangaza ananikera anavyotingisha bich!wa na hiyo mimacho.hapo cio mahali pake. Asubiri Miss Tanzania ijayo kama ana jeuri asitukere tunapemda habari
 
Ni mtangazaji anayetamka neno kwa neno kwa ufasaha mkubwa sana.
Tuwatieni moyo watangazaji wetu mahili kama huyu ili vijana wetu
wengine waige mfano wake.

Zaidi ya hapo itakuwa ni wivu na chuki binafsi kwa binti mrembo kama yule,
pengine labda ni jinsi tu anavyoongea vema bila wasiwasi wala hofu.

Binafsi nampongeza na kumtakia kila la heri katika kazi yake.
 
Back
Top Bottom