I've Reached the End of the Road

I've Reached the End of the Road

Addiction ya gambling/kamari ilinifanya nichukue risk kubwa sana.

Guys kuazia 2020 niliingia kwenye uraibu mkubwa sana wa kamari.

Mwaka 2022 nilifika kwenye peak mbaya sana ya uraibu nikafukuzwa kazi,nilikua nafanya kazi as tour operator huko northern Tz. Ilitokeaje mpaka nikafukuzwa ni stori nyingine.

Sasa si nikafukuzwa kazi with zero balance,sikua hata na pesa yoyote zote nilikua nimezisondeka kwa mhindi hata ndugu zangu wa karibu nilikua siwatumii chochote visingizio tu natoa.
Licha ya kuwa nilikua na mshahara mzuri tu na posho nilikua na madeni mengi sana kwa marafiki zangu wote wa karibu wote kwahiyo sikua na wakumueleza hata anisitiri.

Sasa sikutaka ndugu jamaa na marafiki wajue kabisa kwamba Mimi nimefukuzwa kazi na nipo juu ya mawe nikasema nipo tayari kufa na tai shingoni nikaamua kuingia Arusha mjini,hapo Mimi nyumbani ni Dar.

Niliuza assets zote nilizotoka nazo kazini,PC, binoculars,simu nk lakini havikusaidia maana mzimu wa aviator ulikua umenishika balaa sikutoboa week nikadata kabisa.
Heh kamari aieee hua nasikia tu huu uraibu pole bro na hongera kuchomoka huko
Hapo sasa ndipo nilipoona nimegonga mwamba kabisa nikaaza kumchukua risky yoyote ni survive nikaaza kutarget wanawake wazungu mjini na wanawake watu wazima corporate.


Aaghhh nimechoka kuandika ila tu risky niliyochukua ni kuwa nimekuwa kwenye mahusiano na mwanamke wa miaka 48 mwenye maambukizi ya ukimwi kwa miaka miwili.

Hapo ndio nilipata turning point na break through.

Am -ve though

Gambling ni mbaya
I'm shocked 😲
Huyo mama uli date nae ulikua unajua kabisa ni positive?
 
Mawazo yetu huumba uhalisia wa maisha kupitia maamuzi tunayofanya.

Maneno unayotamka huimarisha mawazo hayo na kuashiria kwenye ubongo wako kile kinachowezekana.

Ukisema umefika mwisho wa barabara, unaweza kuuhadaa ubongo wako uache kabisa kutafuta suluhisho.

.Sababu za Maneno Kuumba Uhalisia

Mabadiliko ya Ubongo (Neuroplasticity):
Ubongo hubadilika na kujirekebisha kimuundo kulingana na mawazo unayoyakariri kila mara.

Mfumo wa Kuchuja Taarifa (RAS): Sehemu hii ya ubongo huangazia na kukuvutia kwenye fursa zinazoendana na kile unachokiwazia zaidi.

Utabiri Unaojitimizia: Kutangaza kushindwa hubadilisha matendo yako, na kufanya kushindwa huko kuwa ukweli usioepukika

Mabadiliko ya Tabia:
Sentensi hasi hufanya mwili ukose nguvu na kuzuia ari yako ya kupiga hatua.

Maneno Mbadala ya Kutumia Wakati wa Changamoto

Badala ya kufunga njia kabisa, tumia misemo inayogeuza kikwazo hicho kuwa sehemu ya mpito:

"Ninaingia kwenye ukurasa mpya wa maisha

""Njia hii inabadilisha uelekeo.

""Ninasaka njia mbadala ya mzunguko.

""Njia hii imeisha, na mpya inafunguka."
Kaka Mshana Jr hapa Umetoka elimu kubwa Sana
 
Safari Yangu Kutoka Lilongwe Hadi Dar es Salaam: Je, Umewahi Kuwa na Imani Kali Kiasi Hiki? 😂 Noma sana

Mwaka fulani nilikuwa Malawi, mjini Lilongwe Wakati huo nilikuwa na miaka 14, naelekea kutimiza 15

Nilikuwa nimeenda likizo, ikafika muda wa kurudi Tanzania

Mama akanipa nauli na kuniambia:

Shika hii pesa vizuri, nenda ukate tiketi.
Kwa nini hakunisindikiza sitasema leo. 😅

Basi nikachukua begi langu lenye nguo chache na mkoba mdogo uliokuwa na pesa za nauli, pesa ya kula, pamoja na kibari changu cha kusafiria Malawi

Nikafika stand ya Lilongwe ambapo magari ya Dar es Salaam yalikuwa yanapatikana

Kipindi hicho kulikuwa na kampuni moja maarufu sana, Taqwa
Sasa sijui ilikuwa bahati mbaya, uzembe sielewi mpka leo nilipochunguza mkoba wangu nikakuta umepotea 😭

Pesa zote zimeenda
Kibari kimeenda
Nauli imeenda
Kila kitu kimepotea

Aisee nilichanganyikiwa vibaya sana. Nikalia mpaka macho yakachoka
Lakini jambo moja nililokuwa na uhakika nalo ni hili

Sirudi nyumbani
Na hii ni hata leo nikisema hapana ni hapana

Kwa sababu mama yangu alikuwa mkali sana
Nilijiona nikirudi kumwambia nimepoteza nauli basi hakuna rangi ningeacha kuona

Nikajiwaza🤔

Kati ya kukutana na mama au kuvuka mipaka bila pesa, bora nijaribu bahati yangu

Nikajikaza nikamfuata dereva
Nikamsalimia kwa heshima zote za dunia
Shikamoo

Akanijibu
Marahaba binti, unasemaje?

Hapo ndipo nilipoanzisha filamu yangu ya kwanza ya maisha Uongooo pro 🤣
Nikaanza
Mimi nilikuja Malawi kufanya kazi za ndani : Astghafirullah 🙌

Dereva aliposikia hivyo akasema
Hebu njoo huku kidogo
Tukakaa pembeni

Sasa hapo nikaanza kusuka hadithi ya uongo kwa kasi ambayo hata nikikumbuka nachoka maana uongo sio tabia yangu mtu muongo na mnafiki hawajaachana mbali

Nikamuambia bosi wangu ananitesa sana, nimeamua kukimbia na kurudi Tanzania lakini sina hata senti

Dereva akaniangalia, akaangalia sura yangu ya mtoto mtulivu, akasikitika

Akamwita konda

Wakakubaliana kunibeba bure.
Mimi ndani ya moyo nikasema:
Asante Mungu, operation usirudi kwa mama imeanza rasmi🤣
Safari ikaanza

Usiku ulivyoingia, konda naye akaingia kwenye shughuli zake akanisahau kabisa kuhusu chakula
😭
Lakini Mungu alikuwa mbele
Nilikaa karibu na kaka mmoja ambaye kila alichonunua alikuwa ananipa sehemu bila kuniuliza hata MashaAllah 😍

Nilikuwa nakula kama nimepewa huduma ya full board😂

Tulipofika Karonga polisi wa Malawi walikuwa wanakagua
Konda akaniambia
Shuka ujifiche kwanza he kasheshe
Nikashuka

Ukaguzi ukaisha
Yaani simple tu ikawa imeisha hiyoo
Nikapanda tena

Mpaka leo nikiikumbuka najiona kama nilikuwa kwenye mission ya siri 🤣
Lakini ni kasheshe la kweli lilikuwa
Linaendela nahisi ningefaa kwa ujasusi🤪
Konda akasema shuka
Sisi tutapita hapa rasmi, wewe shuka upande ule vuka kwa mtumbwi 🙄
Nikabaki namtazama

Mtumbwi? Mimi ambaye hata kuangalia maji kwa muda mrefu naogopa? 😭

Akanipa hela kidogo ya kuvukia
Nikakuta mzee wa mtumbwi yupo tayari kazini Inaonekana ni michongo yake
Nikapanda

Tukiwa katikati ya mto nikaanza kuona mbele polisi kama anatusubiri kabisa 😂😂😂 heh

Moyo ukaanza kwenda mbio kuliko mtumbwi

Nilipofika upande wa pili, kweli polisi akaniita
Umetoka wapi?
Malawi
Ulikuwa unafanya nini?
Hapo nikarudia script ile ile akili mtu wangu 🤭

Nilikuwa nafanya kazi za ndani, bosi ananitesa, nimekimbia 🤣
Akauliza kitambulisho
Hakuna
Kibari
Hakuna
Simu
Hakuna
Kila kitu kilikuwa hakuna😂
Yule polisi akaniangalia halafu akasema
Wewe mtoto una ujanja sana
Akaandika namba yake kwenye karatasi na kuniambia

Ukifika Dar nitafute🤣😒
Mimi nikasema sawa, lakini kichwani nilikuwa nawaza basi lisiniondokee tu
🤣
Nikakimbia mpaka sehemu niliyoelekezwa

Baada ya muda gari likafika
Nikapanda
Safari ikaendelea mpaka Dar es Salaam

Leo nikikumbuka hii safari, najiuliza nilikuwa na ujasiri au nilikuwa na hofu ya mama yangu? 😂😂😂

Mom S 🥹🙌

Kwa sababu uongo wote huo, mipango yote hiyo, kuvuka mipaka, mtumbwi, polisi na hatari zote hizo tena mtoto wakike mdogo baso sijakomaa sura katika ya majangili (wanaume jokes)

chanzo chake kilikuwa kimoja tu

Mama yangu alikuwa mkali mno! 😭😭
Lakini pamoja na yote

Mama, nakupenda sana ❤️ ila ukweli ni kwamba ulikuwa mkali mnoooo!
You're a brave girl, you acted out of faith and not sight. Ila wazazi wakali Huwa hawajui baadae wanashape mtu wa namna gani
 
Mawazo yetu huumba uhalisia wa maisha kupitia maamuzi tunayofanya.

Maneno unayotamka huimarisha mawazo hayo na kuashiria kwenye ubongo wako kile kinachowezekana.

Ukisema umefika mwisho wa barabara, unaweza kuuhadaa ubongo wako uache kabisa kutafuta suluhisho.

.Sababu za Maneno Kuumba Uhalisia

Mabadiliko ya Ubongo (Neuroplasticity):
Ubongo hubadilika na kujirekebisha kimuundo kulingana na mawazo unayoyakariri kila mara.

Mfumo wa Kuchuja Taarifa (RAS): Sehemu hii ya ubongo huangazia na kukuvutia kwenye fursa zinazoendana na kile unachokiwazia zaidi.

Utabiri Unaojitimizia: Kutangaza kushindwa hubadilisha matendo yako, na kufanya kushindwa huko kuwa ukweli usioepukika

Mabadiliko ya Tabia:
Sentensi hasi hufanya mwili ukose nguvu na kuzuia ari yako ya kupiga hatua.

Maneno Mbadala ya Kutumia Wakati wa Changamoto

Badala ya kufunga njia kabisa, tumia misemo inayogeuza kikwazo hicho kuwa sehemu ya mpito:

"Ninaingia kwenye ukurasa mpya wa maisha

""Njia hii inabadilisha uelekeo.

""Ninasaka njia mbadala ya mzunguko.

""Njia hii imeisha, na mpya inafunguka."

Kwa kusoma hivi ni rahisi sana

Kawaida mtu akiwa na msongo au na kiwewe cha jambo fulani
na hasa akiwa anapokea presha kutoka kwa watu au mazingira sio rahisi kuamua sawa sawa hapo ndio linakuja neno maamzi magumu

Kumbuka ile story ya majuzi boda boda kujirusha kwenye roli alikua na msongo na akashindwa kuzibiti hofu yake

Na hii ni wasababu alikua anahofia jambo fulani

Mimi ku take risk hivyo ni kwa sababu ya mama angu alikua mkali niliogopa nikafanya maamzi magumu

But now najifunza namna ya kuendea mambo japo ubinadamu unabaki pale pale hofu na mfadhaiko
 
You're a brave girl, you acted out of faith and not sight. Ila wazazi wakali Huwa hawajui baadae wanashape mtu wa namna gani
Asante kaka mama angu alikua mkali walau saivi anazeeka
But kwa jinsi alivyo nimejifunza vingi japo kwa njia ngumu

Moja ya kitu nilichojifunza ni kua na msimamo nikisema hapana ni hivyo ndio ni hivyo
 
Asante kaka mama angu alikua mkali walau saivi anazeeka
But kwa jinsi alivyo nimejifunza vingi japo kwa njia ngumu

Moja ya kitu nilichojifunza ni kua na msimamo nikisema hapana ni hivyo ndio ni hivyo
Mahusiano yako na mama ni mazuri?
Daah Huwa na feel sympathy kubwa sana Kwa mtu alie kuwa na mzazi mkali. I was victim too,
 
Heh kamari aieee hua nasikia tu huu uraibu pole bro na hongera kuchomoka huko

I'm shocked 😲
Huyo mama uli date nae ulikua unajua kabisa ni positive?
Aliniambia kabisa before,Mimi ndio nilikubali na kurisk kwasababu nilijua Kuna sehemu atanifikisha.
Yes sio haba mambo yalienda ila kwa gharama kubwa
 
Aliniambia kabisa before,Mimi ndio nilikubali na kurisk kwasababu nilijua Kuna sehemu atanifikisha.
Yes sio haba mambo yalienda ila kwa gharama kubwa
Aisee wewe kweli uli take risk 🥹
Siwezi kukulaumu kaka
From now ishi maisha yako ❤️
 
Akasimulie bahari,?? Nothing will work... Ili hiyo Siri I dissolve anahitaji human interaction asikilizwe aeleweke then ajue it was not his/her fault
Sasa yeye hataki

Tumpe mda akiwa tayali atasema hata isipokua humu

na nina muelewa sana unamshirikisha jambo mtu kesho inakua breaking news kila sehemu
 
Back
Top Bottom