ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

Takwimu za hivi karibuni zinazoonesha kituo cha televishen cha Clouds kikiwa kinaongoza kutazamwa na watazamaji wengi kimepeleka shockwaves na kilio kwa kituo ambacho kilikuwa kinaongoza kutazamwa kwa mda mrefu cha ITV.
Hali hii inahatarisha pia wazamini wa vipindi ambao wamekuwa wakinunua airtime ya matangazo kwa kipindi kirefu...
Just imagine wewe ndio muuzaji wa bidhaa fulani mathalani sabuni na unataka uitangaze alafu takwimu zinasema kuwa kituo fulani kinatazamwa zaidi, unadhani utajisumbua kupeleka matangazo yako ITV? Iwapo utayapeleka ITV definitely utataka utozwe pesa kidogo kuliko rates ambazo utapewa clouds.

Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma.
Kuhaha kwingine kumeonekana baada ya ITV kulegeza msimamo wao na 'kuachia bure' matangazo yao kwa njia ya mtandao. yani sasa ukiwa na ile app yao, unaweza kuangalia matangazo ya ITV bure kupitia njia ya mtandao...
Jitihada zao zimekuja when it was too little too late... Ikumbukwe kuwa ITV ndicho kilikuwa kituo chenye watangazaji mahiri na wenye mvuto kama kina Kitenge ila wakati wanajiondoa ITV ilionesha kutowashobokea, kitu ambacho kimewafanya kupoteza watangazaji ambao walikuwa wanahamasisha watazamaji.
Pia wakati ving'amuzi kama star times wakati vinaingia, ITV ilionesha kugoma kujiunga na ving'amuzi hivyo, wakijiona kuwa wao ndio kituo bora na keki ya taifa.
Hiki kiliwafanya wale wasioweza kuipata ITV kwenye ving'amuzi kikimbilia kuangalia channel nyingine na kuifuta ITV kwenye akili zao.
ITV iliendelea kulala usingizi wa pono na kujidanganya kuwa wao ni super brand na kuzidisha fomarlity kwenye vipindi vyao hivyo kuvifanya vipoteze mvuto ihali TV kama clouds zinazoonesha vipindi vya kiswazi kama kile cha SHILAWADU wakizidi kujipatia umaarufu...
Kwa sasa ITV wana kibarua kizito sana kupambana na TV zinazoibukia na wasipojiangalia wanaweza wakazidi kupotezwa kwenye soko la watazamaji wa TV za nyumbani...
Nimeghairi kuendelea kusoma huu uzi wako...hapo ulipofika kwenye SHILAWADU...sijui nini...
 
Lazima Clouds iwazidi ITV maana inapigiwa promo na profesa John Peter Mahenge.
 
ITV wakiweka kipindi vizuri mda wote mtashindwa kufanya Kazi mgande kwenye TV tu mda wote... Ila mtoa Mada kaongea neno ITV wajipange vizuri. Me local channels nilishaacha tizama hadi nisikie jirani kuongeza sauti kubwa muda Wa habari. Na pia TCRA wanachangia kupungua Wa viewers Wa local channel kwa kutowakaripia makampuni yenye decoder kuziachia free kifurushi kinapoisha... Imagine ulipie kifurushi and then utizame free channels its crazy thing mtu hawezi fanya. ITV wana picture quality tofauti na uchafu unaonekana kwenye channel zingine local first time nilidhani TV yangu imeharibika TBC,clouds,star TV na zinginezo
 
Cclouds tv? Hiv Wana nini cha maana?
 
Watoto ndo mnakaa mnaangalia clouds. Vipindi havieleweki, vipindi vya kujisifia tu, vipindi havinigusi kiujumla. Ntabaki na ITV DAIMA
 
yaani ujinga mtupu....!!!clouds kabisa halafu wanashangaa kufeli DSM mitihani ya form four...

yaani siipendi hiyo chaneli
ujinga mtupu
Mkuu kama huipendi hiyo redio au channel basi isiwe kigezo cha kushirikisha na issue zingine zisizohusiana,binafsi nimeacha kusikiliza clouds muda mrefu sana lakini nilikuwa mdau kipindi changu chote cha masomo o'level.Na sijaona inachangia vipi watoto kufeli.Mtoto anapofeli mnaanza kusingizia hata issue zisizochangia kama hiyo..Watoto wa dar Kikubwa malezi ya baba na mama zao ni mabovu...na vishawishi ni vingi lakini siyo ulichokisema
 
We wa isidingo tupo hapa kinachonifurahisha kwenye isidingo unaweza usiifuatilie hata miezi sita ila siku ukiifuma ndo Kama unaendelea ulipoachia Jana [HASHTAG]#isidingo[/HASHTAG] the need
asee tena nkikosa isidingo naumwa kabisa naanzaje kumkosa pastor Gabriel.....
 
Je hii ina uhusiano na utendaji mbovu wa serikali ya JPM? Nauliza hivi kwa sababu ITV iliposhindwa kulipa mishahara ilionekana kusababishwa na utendaji wa serikali ya JPM unaodaiwa kuporomosha uchumi.
 
Kwa habari za ukweli angalia Azam...sijaangalia ITV mwaka sasa...
Azam watakufanya ukae chini kuanzia saa 2 hadi 3...huwa nawalaani sana ...maana wananiharibia ratiba yangu ya usiku...siwezi kukosa habari zao ...kuna jamaa yangu alikuwa mbishi (maana ni mkabila hatari) sasa hivi kanunua king'amuzi cha Azam na yeye sasa anapiga saluti

Yani wanafanya homework yao...ni wajanja...hawaweki habari muhimu mwanzo na zisizo na umuhimu mwisho...wanazi spread ili kukufanya usubiri hadi mwisho...
Huwa mfano nikiwa nimechelewa nasikiliza habari redioni nalazimika kuweka radio one...kuna jamaa anaongea na kibesi yani hata sisikii anatangaza nini...sijui ni sauti yake au redio yao...afu habari zao sasa...muda mfupi zimeisha na in most case wala hakuna real 'news'...wako too formal and structured....wanaanza kitaifa kimataifa michezo bai....wajiongeze sio kuwa vile vile toka mwaka 47...

Ila inawezekana mleta mada akawa sahihi...maana kila nikirudi home nakuta HG wangu ametune Clouds...probably vijana wanaikubali na hiyo inaleta ukweli kuwa Clouds wana viewers wemgi...BUT nadhani suala la viewers linaweza kuwa traced si kwa opinion ni kwa facts and figures
 
mimi nilikuwa naipenda ITV wakati ule bado haijatekwa na sisiem ila kwa sasa sins kituo nachoangalia zaidi ya BBC dila ya dunia, clouds ndio sitaki hata kuisikia
BBC dila ya dunia =BBC Dira ya dunia
 
Jamani kwani Hyo Shilowadu inakua lini maana...
 
sasa clouds unaangalia nn au hilo likipindi la kipuuzi lashilawadu??mwenye akil hawez angalia clouds hataa kidgo labda km utakuwa na element za upunga.ni station ya mabek tatu na watoto
 
Takwimu za hivi karibuni zinazoonesha kituo cha televishen cha Clouds kikiwa kinaongoza kutazamwa na watazamaji wengi kimepeleka shockwaves na kilio kwa kituo ambacho kilikuwa kinaongoza kutazamwa kwa mda mrefu cha ITV.
Hali hii inahatarisha pia wazamini wa vipindi ambao wamekuwa wakinunua airtime ya matangazo kwa kipindi kirefu...
Just imagine wewe ndio muuzaji wa bidhaa fulani mathalani sabuni na unataka uitangaze alafu takwimu zinasema kuwa kituo fulani kinatazamwa zaidi, unadhani utajisumbua kupeleka matangazo yako ITV? Iwapo utayapeleka ITV definitely utataka utozwe pesa kidogo kuliko rates ambazo utapewa clouds.

Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma.
Kuhaha kwingine kumeonekana baada ya ITV kulegeza msimamo wao na 'kuachia bure' matangazo yao kwa njia ya mtandao. yani sasa ukiwa na ile app yao, unaweza kuangalia matangazo ya ITV bure kupitia njia ya mtandao...
Jitihada zao zimekuja when it was too little too late... Ikumbukwe kuwa ITV ndicho kilikuwa kituo chenye watangazaji mahiri na wenye mvuto kama kina Kitenge ila wakati wanajiondoa ITV ilionesha kutowashobokea, kitu ambacho kimewafanya kupoteza watangazaji ambao walikuwa wanahamasisha watazamaji.
Pia wakati ving'amuzi kama star times wakati vinaingia, ITV ilionesha kugoma kujiunga na ving'amuzi hivyo, wakijiona kuwa wao ndio kituo bora na keki ya taifa.
Hiki kiliwafanya wale wasioweza kuipata ITV kwenye ving'amuzi kikimbilia kuangalia channel nyingine na kuifuta ITV kwenye akili zao.
ITV iliendelea kulala usingizi wa pono na kujidanganya kuwa wao ni super brand na kuzidisha fomarlity kwenye vipindi vyao hivyo kuvifanya vipoteze mvuto ihali TV kama clouds zinazoonesha vipindi vya kiswazi kama kile cha SHILAWADU wakizidi kujipatia umaarufu...
Kwa sasa ITV wana kibarua kizito sana kupambana na TV zinazoibukia na wasipojiangalia wanaweza wakazidi kupotezwa kwenye soko la watazamaji wa TV za nyumbani...
Very good analysis..
 
Back
Top Bottom