ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

Takwimu za hivi karibuni zinazoonesha kituo cha televishen cha Clouds kikiwa kinaongoza kutazamwa na watazamaji wengi kimepeleka shockwaves na kilio kwa kituo ambacho kilikuwa kinaongoza kutazamwa kwa mda mrefu cha ITV.
Hali hii inahatarisha pia wazamini wa vipindi ambao wamekuwa wakinunua airtime ya matangazo kwa kipindi kirefu...
Just imagine wewe ndio muuzaji wa bidhaa fulani mathalani sabuni na unataka uitangaze alafu takwimu zinasema kuwa kituo fulani kinatazamwa zaidi, unadhani utajisumbua kupeleka matangazo yako ITV? Iwapo utayapeleka ITV definitely utataka utozwe pesa kidogo kuliko rates ambazo utapewa clouds.

Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma.
Kuhaha kwingine kumeonekana baada ya ITV kulegeza msimamo wao na 'kuachia bure' matangazo yao kwa njia ya mtandao. yani sasa ukiwa na ile app yao, unaweza kuangalia matangazo ya ITV bure kupitia njia ya mtandao...
Jitihada zao zimekuja when it was too little too late... Ikumbukwe kuwa ITV ndicho kilikuwa kituo chenye watangazaji mahiri na wenye mvuto kama kina Kitenge ila wakati wanajiondoa ITV ilionesha kutowashobokea, kitu ambacho kimewafanya kupoteza watangazaji ambao walikuwa wanahamasisha watazamaji.
Pia wakati ving'amuzi kama star times wakati vinaingia, ITV ilionesha kugoma kujiunga na ving'amuzi hivyo, wakijiona kuwa wao ndio kituo bora na keki ya taifa.
Hiki kiliwafanya wale wasioweza kuipata ITV kwenye ving'amuzi kikimbilia kuangalia channel nyingine na kuifuta ITV kwenye akili zao.
ITV iliendelea kulala usingizi wa pono na kujidanganya kuwa wao ni super brand na kuzidisha fomarlity kwenye vipindi vyao hivyo kuvifanya vipoteze mvuto ihali TV kama clouds zinazoonesha vipindi vya kiswazi kama kile cha SHILAWADU wakizidi kujipatia umaarufu...
Kwa sasa ITV wana kibarua kizito sana kupambana na TV zinazoibukia na wasipojiangalia wanaweza wakazidi kupotezwa kwenye soko la watazamaji wa TV za nyumbani...

Utafiti uchwara uliojaa uchumia tumbo na kujikomba
 
nilipenda sana kuangalia ITV nikiwa tz,but majuzi nimerudi nikakuta vipindi havina mvuto kabisa.I think wanatakiwa wabafilike,mfano Isidingo sidhani kama inawagazamaji wengi.Nadhani inabadilika sasa na kua TV ya wazee.
... Hee Isidingo imefanyaje??.. Yaani saa 1.30 hunibandui kwenye Isidingo...
 
Labda shilawadu...
watanzania wengi wanapenda abali za umbea na majungu ndiyo maanamagazati ya udaku yanauza sana kuliko majarida/gazeti yatoayo elimu ya maisha au habari za msingi, hii upelekea kuendelea kuwa na taifa la waongeAJI SANA KULIKO MATENDO mfano katika elimu , siasa na uchumi.
 
Makampuni ya IPPMedia yamekuwa yakichelewesha mishahara na kulipa watu mishahara isiyostahili kwa miaka mingi tu, zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Ukiandika "Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma." inaonekana ama huijui ITV, ama huijui miaka ya nyuma, pengine huvijui vyote.
utakua haris kapiga ww
 
Kuna habari ya azam kupewa tuzo, sasa inanichanganya na hii
 
Anaengalia hio claus mchunguze atakua ana matatizo yaakili lazma, kituo cha kupromot mashoga!!
 
Hivi kweli Azam HD sport inaingia kwenye other?
hao ni wapishi wa propaganda za mitandao kwa ajili ya kibiashara; eti hadi tbc2 ipo above azam two ;
kwa hali hii tanzania ya vi-wonder inakucha9in gwajima voice)
 
Nimesikia kwenye radio tangazo moja eti mapenzi mubashara, yaani nimejisikia vibaya sana tangazo chafu liko uchi, yaani kama uko na wazazi au watoto,!!! Utajisikia vibay Lazima
 
mimi nilikuwa naipenda ITV wakati ule bado haijatekwa na sisiem ila kwa sasa sins kituo nachoangalia zaidi ya BBC dila ya dunia, clouds ndio sitaki hata kuisikia
Washaurini na ukawa wateke baadhi ya TV!
 
nilipenda sana kuangalia ITV nikiwa tz,but majuzi nimerudi nikakuta vipindi havina mvuto kabisa.I think wanatakiwa wabafilike,mfano Isidingo sidhani kama inawagazamaji wengi.Nadhani inabadilika sasa na kua TV ya wazee.
Wat Isidingo? Mkuu hicho ni kipindi bora kabisa na wateja tupo.
 
KIJANA mkubwa hivyo unakaa na kuishindanisha ITV Super brand na CLAUZI shilawadu????


Ama kweli hii ni Tanzania ya viwanda.
 
Back
Top Bottom