Nichumu Nibebike
JF-Expert Member
- Aug 28, 2016
- 8,658
- 15,784
Takwimu za hivi karibuni zinazoonesha kituo cha televishen cha Clouds kikiwa kinaongoza kutazamwa na watazamaji wengi kimepeleka shockwaves na kilio kwa kituo ambacho kilikuwa kinaongoza kutazamwa kwa mda mrefu cha ITV.
Hali hii inahatarisha pia wazamini wa vipindi ambao wamekuwa wakinunua airtime ya matangazo kwa kipindi kirefu.
Just imagine wewe ndio muuzaji wa bidhaa fulani mathalani sabuni na unataka uitangaze alafu takwimu zinasema kuwa kituo fulani kinatazamwa zaidi, unadhani utajisumbua kupeleka matangazo yako ITV? Iwapo utayapeleka ITV definitely utataka utozwe pesa kidogo kuliko rates ambazo utapewa clouds.
Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma.
Kuhaha kwingine kumeonekana baada ya ITV kulegeza msimamo wao na 'kuachia bure' matangazo yao kwa njia ya mtandao. yani sasa ukiwa na ile app yao, unaweza kuangalia matangazo ya ITV bure kupitia njia ya mtandao.
Jitihada zao zimekuja when it was too little too late... Ikumbukwe kuwa ITV ndicho kilikuwa kituo chenye watangazaji mahiri na wenye mvuto kama kina Kitenge ila wakati wanajiondoa ITV ilionesha kutowashobokea, kitu ambacho kimewafanya kupoteza watangazaji ambao walikuwa wanahamasisha watazamaji.
Pia wakati ving'amuzi kama star times wakati vinaingia, ITV ilionesha kugoma kujiunga na ving'amuzi hivyo, wakijiona kuwa wao ndio kituo bora na keki ya taifa.
Hiki kiliwafanya wale wasioweza kuipata ITV kwenye ving'amuzi kikimbilia kuangalia channel nyingine na kuifuta ITV kwenye akili zao.
ITV iliendelea kulala usingizi wa pono na kujidanganya kuwa wao ni super brand na kuzidisha fomarlity kwenye vipindi vyao hivyo kuvifanya vipoteze mvuto ihali TV kama clouds zinazoonesha vipindi vya kiswazi kama kile cha SHILAWADU wakizidi kujipatia umaarufu...
Kwa sasa ITV wana kibarua kizito sana kupambana na TV zinazoibukia na wasipojiangalia wanaweza wakazidi kupotezwa kwenye soko la watazamaji wa TV za nyumbani...