ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

Mi nadhani kati ya EATV na Clouds FM mojawapo itakuwa inaongoza, kwa maana kuna vipindi vingi vya kuangalia vya burudani tofauti na ITV ambayo inategemea taarifa ya habari tu kidogo na kipindi cha Mizengwe, vipindi vingine ni wachache huviangalia hasa wazee
 
Makampuni ya IPPMedia yamekuwa yakichelewesha mishahara na kulipa watu mishahara isiyostahili kwa miaka mingi tu, zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Ukiandika "Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma." inaonekana ama huijui ITV, ama huijui miaka ya nyuma, pengine huvijui vyote.
Marehemu Rehema Mwakangale katangaza zaidi ya miaka 5 bila mkataba, IPP ni majizi
 
Takwimu za hivi karibuni zinazoonesha kituo cha televishen cha Clouds kikiwa kinaongoza kutazamwa na watazamaji wengi kimepeleka shockwaves na kilio kwa kituo ambacho kilikuwa kinaongoza kutazamwa kwa mda mrefu cha ITV.
Hali hii inahatarisha pia wazamini wa vipindi ambao wamekuwa wakinunua airtime ya matangazo kwa kipindi kirefu.

Just imagine wewe ndio muuzaji wa bidhaa fulani mathalani sabuni na unataka uitangaze alafu takwimu zinasema kuwa kituo fulani kinatazamwa zaidi, unadhani utajisumbua kupeleka matangazo yako ITV? Iwapo utayapeleka ITV definitely utataka utozwe pesa kidogo kuliko rates ambazo utapewa clouds.

Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma.
Kuhaha kwingine kumeonekana baada ya ITV kulegeza msimamo wao na 'kuachia bure' matangazo yao kwa njia ya mtandao. yani sasa ukiwa na ile app yao, unaweza kuangalia matangazo ya ITV bure kupitia njia ya mtandao.

Jitihada zao zimekuja when it was too little too late... Ikumbukwe kuwa ITV ndicho kilikuwa kituo chenye watangazaji mahiri na wenye mvuto kama kina Kitenge ila wakati wanajiondoa ITV ilionesha kutowashobokea, kitu ambacho kimewafanya kupoteza watangazaji ambao walikuwa wanahamasisha watazamaji.
Pia wakati ving'amuzi kama star times wakati vinaingia, ITV ilionesha kugoma kujiunga na ving'amuzi hivyo, wakijiona kuwa wao ndio kituo bora na keki ya taifa.

Hiki kiliwafanya wale wasioweza kuipata ITV kwenye ving'amuzi kikimbilia kuangalia channel nyingine na kuifuta ITV kwenye akili zao.

ITV iliendelea kulala usingizi wa pono na kujidanganya kuwa wao ni super brand na kuzidisha fomarlity kwenye vipindi vyao hivyo kuvifanya vipoteze mvuto ihali TV kama clouds zinazoonesha vipindi vya kiswazi kama kile cha SHILAWADU wakizidi kujipatia umaarufu...

Kwa sasa ITV wana kibarua kizito sana kupambana na TV zinazoibukia na wasipojiangalia wanaweza wakazidi kupotezwa kwenye soko la watazamaji wa TV za nyumbani...
Ni king"amuzi gani ITV haipatikani? hivi kweli unaifananisha ITV na Clouds Tv? unajua utofauti wa Kuwa super brand na kupata views wengi? Clouds amepata views robo ya nne ya mwisho wa mwaka 2016 na hiyo haiwafanyi kuwa super brand.
Hivi kweli kwa akili yako ITV inaweza kukosa matangazo?
 
katk TV station mbovu kabisa Tanzania ni TBC 2 clouds Tv na Chanel 10, hawana guiding programs, muonekano mbaya, sauti ndio ovyo kabisa.

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
Mi nadhani kati ya EATV na Clouds FM mojawapo itakuwa inaongoza, kwa maana kuna vipindi vingi vya kuangalia vya burudani tofauti na ITV ambayo inategemea taarifa ya habari tu kidogo na kipindi cha Mizengwe, vipindi vingine ni wachache huviangalia hasa wazee
kweli we ni screpa

Sent from my INFINIX-X551 using JamiiForums mobile app
 
ITV kipindi kinachoangaliwa ni taarifa ya habari tu labda kidogo na dakika 45 zaidi ya hapo ni uozo mtupu
 
hizi tv za tanzania michosho yaani hakuna hata tv moja ambayo imeweza kuonyesha mashindano ya afrika halafu mnazungumzia kuvutia watazamaji
 
aiseehh!hivi mtu makini ataangalia clouds kweli

hii nchi wajinga wengi utakuta jitu zima linaangalia shilawadu daahhh!!

halafu mnataka Tanzania ya viwanda...
Mmmmhhhh jaman kuna muda wa viwanda na muda wa kuanhalia mambo yanayoifuraisha akil.
 
Kuna wakati Itv walikuwa wakisoma magazeti hata jina la gazeti hawalisema wala kulionesha
 
Kwa watu wenye akili zao bado vituo kama itv na tbc1 ni suala mtambuka
 
Back
Top Bottom