ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

ITV 'Yahaha' baada ya viewers kupungua...

Makampuni ya IPPMedia yamekuwa yakichelewesha mishahara na kulipa watu mishahara isiyostahili kwa miaka mingi tu, zaidi ya miaka 15 iliyopita.

Ukiandika "Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma." inaonekana ama huijui ITV, ama huijui miaka ya nyuma, pengine huvijui vyote.
 
ITV wako vizuri Kwenye taarifa ya habari japo
Hawajimbui kama zaman sasa sijajua kwasababu
Wamepata promo ya watangazaji wake kwenda kufanya kazi Ikuru ndo maana wanashindwa kufanya kama mwanzo

VITUO BORA NA VYENYE MPANGILIO MZURI WA VIPINDI, UBORA WA PICHA NK, NI AZAM IKIFUATIWA NA ITV, HIVI VINGINE VIPO VIPO TU. HATA HIVYO MSIJALI NI MTAZAMO WANGU SIHITAJI MALUMBANO
 
nilipenda sana kuangalia ITV nikiwa tz,but majuzi nimerudi nikakuta vipindi havina mvuto kabisa.I think wanatakiwa wabafilike,mfano Isidingo sidhani kama inawagazamaji wengi.Nadhani inabadilika sasa na kua TV ya wazee.
We wa isidingo tupo hapa kinachonifurahisha kwenye isidingo unaweza usiifuatilie hata miezi sita ila siku ukiifuma ndo Kama unaendelea ulipoachia Jana [HASHTAG]#isidingo[/HASHTAG] the need
 
Hiyo kilauzi imeipita AITIVI mida ya saa moja mpaka mbili tu baada ya Hapo ni AITIVII...
 
Unajichanganya kweli mleta mada, utafiti huo umeufanya lin na wapi toa total no ya watazamaji wa ITV vs CLOUDS tuone. Hivi umewahi kuangalia taarifa ya habari ya clouds kwel? Kuna jamaa mmoja huwa anatangaz kama anajifunza yaan anaboa mpaka kero ,huwez nishawish kuangalia habar za clouds. Kwangu mm habari za kitaifa huwa naangalia ITV, za kimataifa na michezo nacheki star T.V then namalizia na BBC Swahili maana Kikeke plus zuhura yunus ni mwisho wa kaz
 
Wengi wa waliofeli form4 ni mateja wa vipindi vya kilauz, vile vya kina fina mango.
 
Isidingo ilikua ina watazamaji wengi tatizo itv maringo saba wanairudia rudia bila kutoa sababu,kuna kipindi matangazo yalizidi mpaka kero.
Twakimu za kupikwa hizo Cloudz over ITV yaani Isidingo imekosa kabisa watazamaji?
 
Naona hapa wachangiaji wote mpo dar, ukiwa ndani ya kanda ya ziwa ni star times tu marufuku channel nyingine, ukiona mtu yupo kanda ya ziwa anajadili tv nyingine tofauti na star huyo ni wakuja.
 
Kuanzia mtoa Post na upikaji wa hizo takwimu wote mimba ya kifipa inawasumbua
 
Hizo takwimu wanazitoa wapi? Lazima waelewe kuna wateja na watazamaji, utafiti wao umehusisha wateja au watazamaji? Maana utakuta kuna sehemu kuna tv moja tu inaangaliwa na watu elfu moja, hapo inakuaje?
 
usifananishe ITV na vitu vya kijinha jinga.
 
aiseehh!hivi mtu makini ataangalia clouds kweli

hii nchi wajinga wengi utakuta jitu zima linaangalia shilawadu daahhh!!

halafu mnataka Tanzania ya viwanda...
Kwa hiyo uncle anavyopiga mpaka cm unamuonaje?
 
Takwimu za hivi karibuni zinazoonesha kituo cha televishen cha Clouds kikiwa kinaongoza kutazamwa na watazamaji wengi kimepeleka shockwaves na kilio kwa kituo ambacho kilikuwa kinaongoza kutazamwa kwa mda mrefu cha ITV.
Hali hii inahatarisha pia wazamini wa vipindi ambao wamekuwa wakinunua airtime ya matangazo kwa kipindi kirefu...
Just imagine wewe ndio muuzaji wa bidhaa fulani mathalani sabuni na unataka uitangaze alafu takwimu zinasema kuwa kituo fulani kinatazamwa zaidi, unadhani utajisumbua kupeleka matangazo yako ITV? Iwapo utayapeleka ITV definitely utataka utozwe pesa kidogo kuliko rates ambazo utapewa clouds.

Hali hii imethibitishwa na taarifa za kucheleweshwa kwa mshahara zilizotolewa na ITV, kitu ambacho kilikuwa hakijawahi kusikika kwa miaka ya nyuma.
Kuhaha kwingine kumeonekana baada ya ITV kulegeza msimamo wao na 'kuachia bure' matangazo yao kwa njia ya mtandao. yani sasa ukiwa na ile app yao, unaweza kuangalia matangazo ya ITV bure kupitia njia ya mtandao...
Jitihada zao zimekuja when it was too little too late... Ikumbukwe kuwa ITV ndicho kilikuwa kituo chenye watangazaji mahiri na wenye mvuto kama kina Kitenge ila wakati wanajiondoa ITV ilionesha kutowashobokea, kitu ambacho kimewafanya kupoteza watangazaji ambao walikuwa wanahamasisha watazamaji.
Pia wakati ving'amuzi kama star times wakati vinaingia, ITV ilionesha kugoma kujiunga na ving'amuzi hivyo, wakijiona kuwa wao ndio kituo bora na keki ya taifa.
Hiki kiliwafanya wale wasioweza kuipata ITV kwenye ving'amuzi kikimbilia kuangalia channel nyingine na kuifuta ITV kwenye akili zao.
ITV iliendelea kulala usingizi wa pono na kujidanganya kuwa wao ni super brand na kuzidisha fomarlity kwenye vipindi vyao hivyo kuvifanya vipoteze mvuto ihali TV kama clouds zinazoonesha vipindi vya kiswazi kama kile cha SHILAWADU wakizidi kujipatia umaarufu...
Kwa sasa ITV wana kibarua kizito sana kupambana na TV zinazoibukia na wasipojiangalia wanaweza wakazidi kupotezwa kwenye soko la watazamaji wa TV za nyumbani...
Wewe sio mjinga wewe ni MPUMBAVU
 
Back
Top Bottom