Mkuu sio tangazo hii ni habari ambayo husomwa katika taarifa ya habari ya saa 2 kwenye Habari za Africa Mashariki kila siku kuanzia tarehe 29.09.2013 jitahidi kuwa unasoma habari yote kabla ya kucoment kitu chochote
mi mwenyewe nimeshangaa na itv wanavyokomaa na hiyo habari katika kipindi hiki cha mpito.
Kwanza wapo kibiashara hivyo kama ina maslahi kwao hamna anaewakataza kuirudia hata mwezi mzima. Pili wanasema ya ukweli na kwa silka yetu Tz hatupendi kuambiwa ukweli, mara nyingi tunafurahia sifa za kijinga au kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
aaah bw Nyabinghi sijui ni wa kule Jamaika au..leo sipo pamoja na wewe.Ukweli ni ukweli na humuweka mtu huru kwani hakuna haja ya propaganda hapo.Usidhanie kwa kuwekeza Rwanda watakaofaidika ni wao tuu hata mwekezaji ambaye anaweza akawa mtanzania pia.Wanatoa taarifa zitakazosaidia wenye kutaka maendeleo,mbona CRDB bank wapo kule kama kusipokuwa na taarifa kama hizi ingekuwaje??Kwani hata wamarekani walikuwa wanatangaza habari za Osama pia,ingawaje sisi na Rwanda hatuna uadui bali viongozi ndo wagombanao kwa mambo yao ambayo hatukuwatuma ila kwa utashi wao wenyewe!
Tena hata mie ningekuwa na mtaji mkubwa ningeenda kuwekeza Rwanda, jamaa wapo serious na uwekezaji.
Nakumbuka Marehemu Musiba aliwahi kusema kuwa aliomba kiwanja Sumbawanga mjini ili ajenge hotel, ilipita miaka 3 bila kupata (wakati anasema alikuwa hajapata) lakini alienda Rwanda kwenye mkutano wa uwekezaji. Wajumbe waliohudhuria yeye akiwa mmojawapo waliulizwa wanataka kuwekeza katika nini, Musiba akasema anataka kujenga hotel Kigali. Siku ya pili Waziri wa uwekezaji, Meya wa Kigali na Afisa Ardhi walikua mkutanoni kumchukua na kumpeleka kwenye viwanja, alioneshwa viwanja 5, achague kimojawapo. Alipewa miezi 6 kuanza kukiendeleza, na baada ya hapo kama hakukiendeleza, kiwanja kinarudishwa serikalini.
Huyo Kagame pamoja na matatizo mengine lakini hana longolongo kama wa kwetu, ana uchu wa maendeleo.
ITV hawajasema uongo, Ni kweli Rwanda wako juu sana kiuchumi and I wish tanzania tungepata Rais kama Kagame, tungesonga mbele fasta. Tuache porojo za mswahili wetu Mkwer.e na tulifanya kosa kubwa sana kumpa nchi hii Mkwer.e.
Fikra zako zimeenda sambamba na mawazo yangu mkuuMimi ningependa wasome kila siku kwa mwaka mzima maana hiyo ndiyo habari ya muhimu. Kila tunaposikia hivyo, tuweze kujiuliza, 'INAKUWAJE KANCHI KADOGO KASIKO NA RASILIMALI NYINGI, KALIKOTOKA KWENYE VITA, NA KAPO KWENYE VITA KILA SIKU, LANDLOCKED, KAWE KANA MAENDELEO MAKUBWA KIASI HICHO WAKATI TANZANIA TUNA LINCHI KUBWA, LENYE RASILIMALI KIBAO, WATU WENGI, LINAENDELEA KUWA KATI YA NCHI MASKINI NA ZENYE MAZINGIRA HOVYO YA UWEKEZAJI?'
Hiyo taarifa ya habari ya ITV ni ujumbe tosha kwa watanzania kuwa msipoteze muda wenu mwingi kujadili mambo yasiyo na maana, jadili kuhusu maendeleo ya uchumi ya nchi yenu.
ONENI madudu ya viongozi wenu mulinganishe na majembe .Kama tukiacha mahaba ..ingekuwa ni bora Kagame atutawale pia ili tuweze kufikia malengo ya kiuchumi.
Ona hapa chini kwenye mkazo (Bold)mlinganishe na huyo wenu mnaemsifu
Habari wakuu
Kuna taarifa inayohusu Rwanda kuwa nchi iliyo na mazingira mazuri ya uwekezaji na inayokuwa kwa kasi kiuchumi na kupunguza mfumuko wa bei kwa kasi na ni nchi ya 7 kati ya nchi 180 zilizofanyiwa utafiti na benki ya dunia, Naandika hili kwa sababu nina mshangao kwani taarifa hii ilisomwa katika taarifa ya habari ITV saa 2 tarehe 29/8/2013 kinachonishaza taarifa hii imesomwa siku tano mfululizo yaani tarehe 29/8 hadi jana 3/9 sasa najiuliza kuna nini hasa kinachofanya ITV waisome taarifa hii kila siku je ni kuifanyia promo Rwanda kwa wawekezaji au ni kutuumbua Watanzania ambao kila kukicha tunaikashfu Rwanda na hasa Rais wao? au kuna kitu kingine kilichojificha juu ya hili.
Watanzania tuna matatizo mengi. Kwetu sisi wawekezaji ni maadui wakati nchi zote Duniani zinahangaika kuvutia wawekezaji. Siku hizi wawekezaji hawatafuti pakuwekeza bali wanafuatwa na kubembelezwa ili wakawekeze. Tanzania tunapowachukia na kuwafukuza kwa vitendo vyetu wengine wanawaita.
Kwetu sisi, wawekezaji wa madini, wanatuibia madini yetu. Wawekezaji wa gas wanatuibia gas yetu. Wawekezaji wa kilimo, wanatunyang'anya ardhi yetu. Sasa tunataka nini? Dunia nzima hata wale wajamaa wa zamani wanahangaika kutafuta wawekezaji. Leo hii wawekezaji wakubwa nchini China ni makampuni ya Marekani na Ujerumani. Huko Urusi, wanavutia wawekezaji wa Kimarekani.
Sisi tunapowachukia wawekezaji wa nje na kuwaona maadui, tujifunze kutoka kwa mataifa ya Korea Kaskazini (kusiko na wawekezaji wa kigeni) na Korea Kusini (walikojaa wawekezaji wa Kimarekani).
Siasa za ujamaa zilituua fikra. Katika ulimwengu wa leo, mwekezaji mkubwa ni muhimu kuliko kiongozi wa kisiasa. Kinachopimwa ni athari yake kwa jamii. Fikiria leo hii Mengi akifunga biashara zake zote kutatokea nini, linganisha na JK akaacha kuwa Rais, kutakuwa na athari gani kwa jamii? Ndiyo utajua ni nani muhimu zaidi. Wenzetu nchi nyingine kama Malaysia na Singapore mwekezaji mkubwa wa kuanzia mtaji wa U$100 million anapoingia nchini anatandikiwa red carpet, na hupokelewa na waziri anayeshughulika na uwekezaji. Na hawa ni watu walioendelea siyo sisi maskini wa kutupwa, wanafanya hivyo! Halafu sisi tunaendelea na siasa za maskini jeuri.
hAMCHELEWI KUSEMA 'MKE WA mENGI NI mNYARWANDA!
kuna watu wengine wapuuzi kweli kama inakuuma anzisha tv yako halafu utangaze za wabakaji wenzako..Rwanda juu juu zaidi..