ITV na Taarifa hii Kuhusu Rwanda kuna nini ndani yake?

ITV na Taarifa hii Kuhusu Rwanda kuna nini ndani yake?

Mkuu unayosema ni sahihi kabisa. Lakini ITV kama chombo cha habari kipo kibiashara na katika kipindi kama hiki wanajaribu kuonyesha kwa warwanda kama wapo bila kufungana na upande wowote. Japo baada ya maelezo yote sijaona sababu ya ITV kurudia tarifa ya habari moja kila mda wa habari za biashara au africa mashariki. Mbona hawakurudia ushindi wa cheka kuchukua mkanda wa dunia? Kama kuongoza ndiyo sababu.
 
Tushichanganye mambo Watz. ITV walikuwa wanazungumza performance ya uchumi wa Rwanda. Tusichanganye na kuzorota kwa uhusiano kati yao na TZ.

Ni ukweli mtupu kuwa Uchumi wa Rwanda ni Mzuri kuliko wa TZ hata kama tunakaona kanchi kadogo, wanachota madini DRC na mengineyo tutakayotaka kusema. soma hapa:
https://www.cia.gov/library/publications/the-world-factbook/geos/rw.html.
Sisi na marasilimali yetu eneo la ardhi, madini, gesi, chuma, Tanzanite, Almasi, Bandari kibao nk tujifunze kwa hilo.

Pengine ndicho chanzo cha hasira kwa TZ tunawaharibia maslahi ya kiuchumi wa nchi yao kule DRC. wangekuwa navyo hivi tulivyonavyo WaTZ nilivyoorodhesha hapo juu Rwanda isingekamatika

Baniani mbaya lakini kiatu chake ni..... .....
...Ni kweli mkuu. JK hawezi kumfikia huyu jamaa katika kusimamia interest za nchi yake, tena JK hahitaji kwenda kuiba Kongo chochote, tungeweza kukuza uchumi wetu kitakatifu kabisa. Kagame ni dikteta lakini yupo makini kwenye national interest na ni stategist mzuri katika kufikia goals zake, hateui mawaziri kishkaji ndio maana waziri akiharibu anamtosa bila aibu. Sisi wa kwetu - waziri kaibiwa laptop tatu gesti na kukutwa na SMG ambayo kisheria haruhusiwi kumiliki na hatujui alikuwa anaitumia kwenye nini. Rais wetu anavunja baraza la mawaziri halafu anamteua upya?. akina Dr DeoMtasiwa wametimuliwa MoHSW kwa kusababisha mgomo wa madaktari leo karudishwa ofisi ya waziri mkuu eti kushughulikia maswala ya afya. shame!
....Nadhani Rais wetu anadaiwa kitu na hawa jamaa, maana katika nchi ya watu milioni zaidi ya 40 unafanya uteuzi controversial namna hii halafu utegemee tutamfikia Kagame ni ndoto.
 
Kwani wanachosema ITV ni uongo? Rwanda is a shining star in Africa, everyone knows this.
 
Huenda wamepiga kelele na viongozi wetu kurekebisha hali ilivyo hawasikiii na sasa wanawaonyesha Rwanda inavyosonga mbele labda nao wataamka na kuchukua hatua! ITV ni wazalendo sana jamani.

But Nchi ya rushwa hata siku moja ni ngumu kusonga mbele kwa kasi.
 
Kwanza wapo kibiashara hivyo kama ina maslahi kwao hamna anaewakataza kuirudia hata mwezi mzima. Pili wanasema ya ukweli na kwa silka yetu Tz hatupendi kuambiwa ukweli, mara nyingi tunafurahia sifa za kijinga au kupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

ni kweli mkuu tunaridhika sana tunapopewa sifa za uwongo na tusizostahili.
 
yani watanzania mnalifanya swala la kagame na jk kama ugomvi. yani mnataka kulifanya liwe ugomvi wa kudumu na ikiwezekana vita?

huu ni ujinga kupoteza muda kwenye ugomvi,na kwanza Tanzania haina ugomvi na rwanda sema kuna watu mnatamani hata vita itokee sijui mnavichwa gani.

Kwanza na wapongeza ITV kwa kuonesha hiyo habari hili kudhihirisha kuwa hatuna ugomvi na Rwanda.

Ina maana ulitaka habari za rwanda zisioneshwe au kurudiwa ili kitokee nini?ina maana unataka itv waache kutangaza habari za Rwanda ili wachochee kuni?

TUJIFUNZE KUFIKIRI KWA KINA.
 
ila mm nimependa sana,huwezi kujifanya ww bingwa wakushauri wengine wakati ww mambo hayo hayo yanakushinda,acheni watu watangaze hata mwaka mzima ili tz tujifunze zaidi!gd itv carry on.....
 
Tena hata mie ningekuwa na mtaji mkubwa ningeenda kuwekeza Rwanda, jamaa wapo serious na uwekezaji.

Nakumbuka Marehemu Musiba aliwahi kusema kuwa aliomba kiwanja Sumbawanga mjini ili ajenge hotel, ilipita miaka 3 bila kupata (wakati anasema alikuwa hajapata) lakini alienda Rwanda kwenye mkutano wa uwekezaji. Wajumbe waliohudhuria yeye akiwa mmojawapo waliulizwa wanataka kuwekeza katika nini, Musiba akasema anataka kujenga hotel Kigali. Siku ya pili Waziri wa uwekezaji, Meya wa Kigali na Afisa Ardhi walikua mkutanoni kumchukua na kumpeleka kwenye viwanja, alioneshwa viwanja 5, achague kimojawapo. Alipewa miezi 6 kuanza kukiendeleza, na baada ya hapo kama hakukiendeleza, kiwanja kinarudishwa serikalini.

Huyo Kagame pamoja na matatizo mengine lakini hana longolongo kama wa kwetu, ana uchu wa maendeleo.

..kwenye kuchangamkia wawekezaji/wahamishaji toka nje tumewazidi Rwanda, tena kwa kiasi kikubwa.

..umesahau jinsi waziri wetu wa madini alivyochangamka ktk kusaini mkataba wa mgodi wa dhahabu wa Buzwagi??

..waziri alimfuata muwekezaji London, wakasaini mkataba hotelini!! sijui ilikuwa chumbani, au kwenye lobby area.

NB:

..serikali yetu haipendi WAZAWA.
 
Ukweli ndiyo huo. Hivi kuna ugimvo kati yawananchi wa Rwanda na Tanzania au kati ya viongozi waliopo kutokana na mitazamo yao binafsi? Kwanza Rwanda kuyazuia magari ya kutokea Tanzania kuingia Rwanda kwa wananchi wa kawaida linatuhusu nini. Malori hayo ni kweli yanajaza uzito kupita kiasi kutokana na mfumo wa upimaji uzito uliopo kwenye vituo vya kupimia mizigo kutokana na hongo na zaidi magari ya wakubwa hayawezi kusumbuliwa hata yangezidisha uzito mara 10 ya kiwango stahili. Tukumbuke mwanzoni mwa miaka ya 80 tanzania ilizuia malori ya mizigo kutokea Kenya kwa kisingizio kuwa yana uzito kupita kiasi jambo ambalo linachangia kuharibu barabara zetu na kuyapachika jina kuwa yanamilikiwa na Manyangau. Je leo magari ya mizigo ya Tanzania nayo yanamilikiwa na Manyangau?.
 
Back
Top Bottom