Itv mwaonyesha picha chafu - kipindi kilichoishia saa 4.15 usiku

Inasikitisha ITV yenye hadhi kama ITV kuruhusu vipindi vichafu kama hivyo (Siri ya mtungi). Tuna fundisha maadili gani kwa watoto wetu.Halafu tunasema watoto wa siku hizi wameharibika. Tena inatia kinyaa wakati mtanzania anavyojaribu kuiga tabia ambazo hazikuzoeleka hapa kwetu. Shame on you ITV

Lalamikia umasikini wako kwa kuwa na Video moja kwa hiyo wasituoneshe maisha kisa kuna watoto wanunulie tv watoto zako iwe chumbani kwao na uwawekee CD za kitoto.We dini gani kwanza mbona mlalamishi hivyo?
 
Ukionesha mwanaume na mwanamke wamelala kimahaba kitandani utakuwa unakosea kwa audince ya watz, bila shaka hata kwako wewe yaweza shida kuangalia ukiwa na wazazi/watoto etc. Zipo namna nyingi za kufikisha ujumbe wowote bila kukwaza 'wateja', hiyo sinema haikutengenezwa ili itazamwe na hao unaowaita wafadhili sijui watu gani. Imeletwa kutazamwa na watu kama mleta mada.

Pia sio lazima kumjua muandaaji au mfadhili wa kipindi ili kujua kama ni kizuri au kibaya. Nakubaliana na wewe kuwa watanzania bado tuna safari ndefu.

Naungana na hoja ya mleta mada

Ile tamthilia inaelezea kuhusu maswala ya ukimwi na magonjwa rafiki wa ukimwi yanayotokana na ngono zembe na kwa dunia ya sasa kila kiti lazima kiwe wazi ili watoto wetu wajue

Ukimya na kuficha ficha ndio ulitufikisha hapa....

Na ndio maana sasa hivi darasa la tatu mtoto shuleni anafundishwa namna mwanamke anavyopata mimba mtoto anajua kazi ya korodani ni nini...

Ni lazima waonyeshwe kwa vitendo matendo yanaambukiza ukimwi

Ili mradi tu matendo hayo yasiwe katika mfumo wa pornographic

Baba na mama wamelala kitandani laini sana hiyo sio ya kupigia kelele...,

Hata french kiss baadhi ya channel wanaacha....

So longas sio nude... there is nothing to hide.....

Tuna safari ndefu ila tutafika kwani zamani ukiwa ukisikia tangazo la kondom ulikuwa unabadilisha chanel ili mtoto asisikie...

Ila siku hizi...

Nisimalizie sana ila watanzania tuna safari ndefu mno
 
Umemaliza kilakitu,
 
Inasikitisha ITV yenye hadhi kama ITV kuruhusu vipindi vichafu kama hivyo (Siri ya mtungi). Tuna fundisha maadili gani kwa watoto wetu.Halafu tunasema watoto wa siku hizi wameharibika. Tena inatia kinyaa wakati mtanzania anavyojaribu kuiga tabia ambazo hazikuzoeleka hapa kwetu. Shame on you ITV

ITV yenye hadhi kama ITV!? aint i gotta a sober mind ..!???
 
Hebu fafanua huo uchafu mkuu maana tokea wakate dijitali wengine tunaendelea na DSTV...hizi locals tushaanza kuzisahau
 
Inasikitisha ITV yenye hadhi kama ITV kuruhusu vipindi vichafu kama hivyo (Siri ya mtungi). Tuna fundisha maadili gani kwa watoto wetu.Halafu tunasema watoto wa siku hizi wameharibika. Tena inatia kinyaa wakati mtanzania anavyojaribu kuiga tabia ambazo hazikuzoeleka hapa kwetu. Shame on you ITV

Wewe avcha kupotosha vipindi vilivyoenda shule.....
Kakika picha za kibongo zilizo kaa vema hii ni namba1..!!

Taja maeneo unayoona ni machafu? usiongelee kiujumla...ndio tutajua kama kweli unazo, au unahoma ya kulalamika!!

Kuna eneo kwa mfano jamaa kamtoa dogo chumbani kisa yeye yuko na girl friend wake...then baada ya kuingia dogo anaonekana anawaangalia(wao hawaonekani) zinasikika busu busu kianina basi hakuna kilichoonyeshwa!! sema wapi pachafu?
 
mida hiyo watoto wako macho wansubiri nini na wewe???

kuwaweka macho hadi saa nne usiku ni mbaya kuliko kuangalia vitafunio

Kwani imeandikwa under 18 hawaruhusiwi ili watu wawaandae watoto? Na je hakinaga marudio nyakati za mchana kweli kama mfanyavyo vipindi vingine?
 
Mkuu nina maswali 6 nataka kukuiliza
Unajua maana ya picha chafu ?
wameonesha nude videos ?
Unajua project ya siri ya mtungi inahusu nini?
Unawajua kwanini siri ya mtungi inaonyeshwa itv na eatv?
Unawajua wafadhili wa siri ya mtungi?
Unajua kwanini wameonesha hizo picha wewe unazoziita chafu kwa makusudi?

Watanzania tuna safari ndefu sana mkui,..

umemuuliza maswali ya msingi safi sana mkuu. Heshima yako.
 
Wazo langu,
kimtazamo hapa si mahali pa kutukanana au kuwa majibizano ambayo hayana lengo ya kufundisha au kusaidia. Mleta mada kaleta hoja, wazo na hisia zake juu ya nn amekiona huo usiku kwa ITV. Sasa sawa hajatuambia ni nn hasa alichokiona ili tuweze kumsaidia ipasavyo!
Tasfiri ya yeye na watoto kuwa macho hio sa nne, kuwafahamu waigizaji, wapi ilipoigiziwa, wafadhili sidhani kama itatusaidia kitu. Mimi nawafahamu na mmoja nipo naye hapa Ubungo msewe na ni mhusika mkubwa tu japo sikuona hio movie huo usiku lakini sipati shida kutaka kujua yote haya, niwaombe tu wana JF kusaidiana kimawazo hii itaweza tujenga na kufahamiana vizuri na wengi kuwa msaada kwa wengine hapa. Mimi naamin kabisa wengi hamfahamiani, kutoweka majina yenu halisi na picha zenu haiwafanyi mzozane. Mimi nawaambieni na ndio naamini hivi kuwa wengi wenye mahitaji hapahapa JF wapo ambao ni suluhisho au msaada kwako! Tufikiri kwa urefu na si kwa saizi ya Zakayo
Kama kuna mtu nimemkwaza naomba anisamehe
Mungu awabariki sana
 
Lalamikia umasikini wako kwa kuwa na Video moja kwa hiyo wasituoneshe maisha kisa kuna watoto wanunulie tv watoto zako iwe chumbani kwao na uwawekee CD za kitoto.We dini gani kwanza mbona mlalamishi hivyo?

Mshukuru sana Mungu aliyekupa wewe uwezo wa kuwa na TV zaidi ya moja na Moyo wa kumdharau mwenzio kwa umaskini wake. Naamini ipo siku Mungu huyu atatenda kwako pia.
 
Watoto usiku wa manane wanafanya nini mkuu? Ndiyo maadili hayo pia?
Inasikitisha ITV yenye hadhi kama ITV kuruhusu vipindi vichafu kama hivyo (Siri ya mtungi). Tuna fundisha maadili gani kwa watoto wetu.Halafu tunasema watoto wa siku hizi wameharibika. Tena inatia kinyaa wakati mtanzania anavyojaribu kuiga tabia ambazo hazikuzoeleka hapa kwetu. Shame on you ITV
 
Nafikiri Sio jambo la busara kuacha watoto wadogo mpaka saa 4 usiku hawajalala! Secondly utakuwa kuwa mwendawazimu kwa dunia ya sasa Kama utafikiri malezi/maadili ya watoto wako yatajengwa na jamii dunia ya sasa imeharibika sana kuwa responsible na watoto wako kumbuka watoto wako wakiharibikiwa ni wewe Kama mzazi umeshindwa Hakuna atakaye kuelewa ukiilaumu jamii japokuwa inaweza kuhusika!
 
Inasikitisha ITV yenye hadhi kama ITV kuruhusu vipindi vichafu kama hivyo (Siri ya mtungi). Tuna fundisha maadili gani kwa watoto wetu.Halafu tunasema watoto wa siku hizi wameharibika. Tena inatia kinyaa wakati mtanzania anavyojaribu kuiga tabia ambazo hazikuzoeleka hapa kwetu. Shame on you ITV
Kama vp uza hyo tv ili watoto wasiangalie
teh teh teh!
 
Back
Top Bottom