ITV Live: Lipumba anamshukia Kikwete ESCROW

ITV Live: Lipumba anamshukia Kikwete ESCROW

Wewe ni Mpuuzi kabisa. Hata kama mtu ni adui yako, anaposema ukweli ni lazima aungwe mkono. Tunajua kazi yenu CCM ni kujaribu kutugawa ili tusiwe na nguvu yakuwaelimisha wananchi ili wawabwage. Safari hii mtakoma, Hamuwezi kutugawanya. Tumeshawashtukia. Jaribuni kuwa na akili. Nchi hii ni ya watoto wetu wote na siyo ya Mafisadi tu. Lipumba ni mtu makini kuliko yeyote ndani ya CCM. Mtakoma Waka huu, mapka kieleweke.
 
usiniambie wakati wa nyerere sikuwepo
mimi nimeshuhudia ccm ikila nchi bila huruma huku wananchi wake wakiwa na hali mbaya

na wakati wa nyerere mapato yatokanayo na kodi hayakua makubwa kama siku hizi
kulikuwa hakuna wizi wa bilion 300 kama siku hizi ila wa benja na kikwete yote tumeyashuhudia bora mwinyi alijitahidi kwa kiwango chake


Huo wizi wa kufikirika na kujilisha na kujijaza ujinga. Mlitaka umeme wa bure.

CCM wanakula nchi, chadema wanakula michango ya chama. fuso mbili chakavu kwa millioni 600.

Nyerere kilimshinda nini kuyafanya mapato yawe makubwa? ni ujamaa wake ulioididimiza nchi, aliikuta inauza mazao nje kuliko nchi yoyote katika Afrika na laiti angaliiweka misingi mizuri na si ile ya ujamaa, leo hii Tanzania ingekuwa hakuna kulipa kodi au ingekuwa ndogo sana. Kumbuka hilo, kuharibu ni rahisi kuliko kutengeneza.
 
Ha ha ha FF! Hukumbuki kwa jinsi alivyokuwa anaichukia rushwa kidogo Chief Fundikira alambwe Hamsa wa Ishirini akiwa waziri wa sheria kwa kupokea rushwa? Siku hizi siku hizi mpokea rushwa ndio mjanja.

Kuna anaeichukia rushwa zaidi ya Kikwete? tunaoona kaiunda TAKUKURU na leo inazagaa wilaya zote, tumeona mpaka mawaziri wakiswekwa jela na Kikwete, nani wa kabla yake alithubutu hayo?
 
Nasikitika sana unavyomtetea jk ccm ni walewale, hakuna kipindi ambacho watz wengi wameuawa na serikali kama cha jk, arusha nadhani unakumbuka, mtwara huko nako ndo usiseme ndo maana uchaguzi serikali za mitaa tandahimba ccm hamujapata ujumbe, wala kiti chochote na hiyo ni salamu

Hukuwepo wakati wa Nyerere, uliza kina Hanga wako wapi? waliouliwa vijiji vya ujamaa pekee ni kwa maelfu kama si malaki.

Msome Ludovick Kaijage.
 
Leo magwanda mnamuona Lipumba mzuri si mlikuwa mnamtukana huyo, mmesahau?

Amma kweli baniani mbaya kiatu chake dawa. Nawashauri chadema muwe mnamuabudu Lipumba mumfanye mungu wenu, ndiyo aliwasaidia mlipokuwa ICU.

Imekuwaje ndugu mbona unachangia kwa jaziba sana? Tulia ujadili hoja.Mleta hoja anazungumzia Lipumba na alichokieleza leo sasa hapo CDM inaingiaje? TULIA KIKUINGIE DADA.VUMILIA TU UTAMU UTAMU UTAUSIKILIZIA U KARIBU.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kuna anaeichukia rushwa zaidi ya Kikwete? tunaoona kaiunda TAKUKURU na leo inazagaa wilaya zote, tumeona mpaka mawaziri wakiswekwa jela na Kikwete, nani wa kabla yake alithubutu hayo?

Usichefue watu hapa. Nani kakuambia kuwa kikwete anchukia Rushwa??? Ndivyo mnavyojidanganya nakujiaminisha ndani ya chama chenu? Wapi alishawahi kukemea rushwa? Unadhani kuunda takukuru ndiyo kuichukia rushwa? Hiyo Takukuru imemgusa nani mkubwa? au nikwaajili ya machinga tu? Mlarushwa hawezi kuchukia rushwa hatakidogo? Msifikiri watanzania hawaelewi upuuzi mnaoufanya wa kulindana. Jitahidini tu kuwa na shingo ngumu kwani muda wenu unafika ghafla kama gharika. Jifunzeni basi hata kwa alama za nyakati.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Good morning FF, naona una mzio mbaya kabisa na Nyerere RIP lakini kumbuka kipindi hicho unachozungumzia wewe nchi ilikuwa imetoka vitani na Uganda na kilikuwa ni kipindi cha mpito
Nyerere aliweza kuibeba nchi vilivyo hata katika kipindi kigumu kabisa na kwakweli alikuwa imara kwenye maamuzi yake nafikiri unakumbuka operesheni ya wahujumu uchumi mwaka 1984 iliyoongozwa na E.M. Sokoine RIP, JK na Pinda hawawezi kufanya hata robo ya yale yaliyofanywa na NYERERE na Sokoine
personality ya JK ni practice of leniency, na dull actions kitu ambacho hakifai hata kwa familia achilia mbali Taifa

Personality ya JK sio ya kuchukua maamuzi magumu hata kidogo na anapofanya hivyo huchukua muda mrefu na kujishauri kwingi na kusitasita sana! Hii pia sio sifa nzuri kwa kiongozi wa nchi

Personality ya JK ni kutaka kumridhisha kila mmoja kitu ambacho ni hatari mno! Lazima uwe na msimamo thabiti kwenye lolote lile usiwe kinyonga huyu unamwambia hivi yule unamwambia vile ni hatari kwa Taifa

RIP kisha kufa? RIP inatakiwa ukiwa hai. Oh you who believe enter into peace. Siyo ku rest in peace, itamsaidia nini kama uhai wake alikuwa hayuko kwenye peace?

Jakaya hafanyi vitu kwa kukurupuka, hufanya vitu vyake kiumakini mkubwa sana.
 
Huo wizi wa kufikirika na kujilisha na kujijaza ujinga. Mlitaka umeme wa bure.

CCM wanakula nchi, chadema wanakula michango ya chama. fuso mbili chakavu kwa millioni 600.

Nyerere kilimshinda nini kuyafanya mapato yawe makubwa? ni ujamaa wake ulioididimiza nchi, aliikuta inauza mazao nje kuliko nchi yoyote katika Afrika na laiti angaliiweka misingi mizuri na si ile ya ujamaa, leo hii Tanzania ingekuwa hakuna kulipa kodi au ingekuwa ndogo sana. Kumbuka hilo, kuharibu ni rahisi kuliko kutengeneza.

Mshukuru nyerere alituunganisha ila miccm mnatugaw nyerere alifanya kwa nafasi yake kwa kipindi chake hakutaka umugabe au ughadaffi ila nyie mnataka ufalme kabisa ni ziro kuona unashabikia majizi kama unatetea majizi kuanzi leo nakuita mwizi tu potelea mbali hizo ban nizile

wewe FaizaFoxy ni mwizi ni fisadi
 
Last edited by a moderator:
Hayo yalikuwa wakati wa Nkapa, wala alikuwa hajali Wazanzibari wakiuwana, ana uchungu nao upi? lakini mwenye uchungu nao alipoingia madarakani, tukaona amani imeingia Zanzibar, waliokuwa wanauwana na kuwekeana mavi sasa wanaongoza Zanzibar kwa pamoja, raha mustarehe.

Au huyajuwi hayo?
haa haa we binti/ajuza ni mbaguzi sana. Mwanaccm makini hawezi kuunga hoja zako kichwakichwa tu.
 
huyu mseja naye tumemchoka

Uko peke yako lakini unajipa nafsi ya wingi. Wewe sema 'Nimemchoka, sio tumemchoka'.
Usijitie kimbelembele cha kutaka kuwasemea watu, jisemee mwenyewe.
Ova
 
Mshukuru nyerere alituunganisha ila miccm mnatugaw nyerere alifanya kwa nafasi yake kwa kipindi chake hakutaka umugabe au ughadaffi ila nyie mnataka ufalme kabisa ni ziro kuona unashabikia majizi kama unatetea majizi kuanzi leo nakuita mwizi tu potelea mbali hizo ban nizile

wewe FaizaFoxy ni mwizi ni fisadi

Alikuunganisha ulikuwa umefarakana na nani?

Nyerere mwenyewe alipokuja Dar alipokewa, kauta watu wako bukweri kabisa.

Hii nchi ilikuwa ni kitovu cha amani na ndiyo maana ikaitwa Dr Es Salaam, imo kwenye Qur'an hiyo.

Toka Zanzibar mpaka Kongo ilikuwa shwari kabisa na watu wakifanya biashara zao bila uvunjifu wa amani.

Dar ndiyo kabisa, tulikuwa hatuna kufuli za milango kabla ya Uhuru.
 
Back
Top Bottom