Itel Yaanzisha maktaba Shule ya Msingi Ubungo NHC

Mar 5, 2020
18
28
Mwishoni mwa juma lililopita tulitembelea shule ya Msingi Ubungo NHC kwaajili ya kuweka nguvu zaidi ya kuendeleza elimu, sote tunafahamu serikali inafanya jitihada kubwa sana kuendeleza miundombinu ya elimu ikiwemo kujenga madarasa kutokana na ongezeko la idadi kubwa ya watoto. Hivyo nasi tumeona tuunge mkono jitihada za serikali kwa kutoa vifaa vya masomo.
View attachment IMG_9007.jpg
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya msingi Ubungo NHC

Lakini kwa kifupi ni kwamba Itel ilianzisha kampeni ya CSR yenye kaulimbiu ya ‘Love Always On’ yaani Upendo Usiozima tangu mwaka 2003 ikilenga kurudisha fadhila kwa jamii kwa kuwasaidia wanafunzi /watoto kuwa na mazingira mazuri ya kusomea au vitendea kazi vya shuleni.

Hakuna asiyefahamu kuwa Watoto ni hazina na ni taifa lijalo, hivyo sisi itel kwa kutumia kaulimbiu yetu ya “Enjoy Better Life” tunahakikisha tunatengeneza mazingira mazuri kwaajili ya kutimiza azma yetu ya kuwasaidia watoto kufurahia maisha bora. Programu hii kwa sasa inatekelezwa nchi zote za Afrika ambazo itel inapatikana.
IMG_9142.jpg

Sehemu ya maktaba iliyotolewa na itel
Kwa upande wa Tanzania tayari itel imeshafanya matukio ya kurudisha fadhila kwa jamii yaani CSR mara kadhaa katika shule na vituo vya watoto Yatima tangu mwaka 2016 mpaka sasa.

Pia tumeanzisha Mradi wa maktaba unaojulikana kama ‘Wandering Libraries Project’ tangu 2021 na huu utakuwa mradi wa muda mrefu wa CSR wa itel. Lengo ni kuchangia maktaba ndogo zaidi ya 10,000 kote barani Afrika katika miaka 3 ijayo.

Hivyo basi kama ilivyoelezwa hapo awali, leo tumetembelea shule hii na Lengo la kutembelea shule hii ni pamoja na kuwasaidia watoto wanaotoka mazingira magumu au familia zenye kipato cha chini ya mstari kwa kuwapatia vifaa vya masomo yakiwemo mabegi, madaftari, kalamu, chupa za maji na miamvuli kwa kipindi hiki cha mvua.
IMG_9168.jpg
IMG_9102.jpg
Meneja Mahusiano wa itel Bw. Fernando Wolle akizungumza na vyombo vya habari na picha ya pili akiwa na wanafunzi

Pamoja na msaada huu kwa watoto hawa wanaotoka mazingira magumu, pia itel mobile Limited tumeipatia Shule ya Msingi Ubungo NHC Shelfu 20 za kuhifadhia vitabu pamoja na Vitabu vya kiada 217 (mia mbili kumi na saba) kwa masomo ya Sayansi, Hesabu na Kiingereza kwa darasa la tatu, la nne na la tano. Msaada huu kwa pamoja una thamani ya shilingi za kitanzania milioni 5.
IMG_9218.jpg


IMG_20220429_113346_960.jpg

Meneja Mahusiano wa itel Bw. Fernando Wolle akikabidhi vitabu vya maktaba hiyo kwa Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ubungo NHC Bw. Paulo Mdachi.
Zoezi hili ni endelevu hivyo tunawakaribisha wadau wengine kushirikiana nasi katika kuendeleza elimu Tanzania.
 
Back
Top Bottom