Itambue thamani ya uliyenae

Itambue thamani ya uliyenae

Hahahaaaaaa!! Sasa si mada inaongelea mapenzi ya tabia mbaya? Ila huwa namshukuru sana Mungu aisee, basi tu!
Mmh em funguka cha ukorofi wewe, "hapo basi tu" kuna kijistory amazing teh teh
 
​asalaam aliyekhum wana mmu,

nipo hapa mbele yenu kuwakumbusha kitu kimoja muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku hasa yale ya kimahusiano.

Najua wote tunajua thamani ya mapenzi na pia tunafahamu ni jinsi gani mapenzi yanatesa, yanaumiza na wakati mwingine kuua. Wengi tunafahamu jinsi mapenzi yalivyoleta umoja, undugu na urafiki ambao haukutarajiwa katika maisha yetu lakini kutokana na huyu kuoa yule na yule kuolewa na huyu tumejikuta tukiunganishwa na jambo hilo.

Licha ya kujua thamani ya mapenzi na maumivu yake lakini tumeshindwa kuilinda thamani na kuyapuuza maamuvi yake. Tumekuwa wakosaji wakubwa sana kwa wenza wetu tulionao. Tumekuwa hatutambui thamani ya tulionao mpaka pale wanapoondoka mikononi mwetu. Tumekuwa watu tusiothamini mioyo na machozi ya wenza wetu kanakwamba sisi ni wanyama.

Kwanini umlize mwanaume aliyekupenda na kukusaidia katika maisha yako? Kwanini umsaliti mwanamke aliyekupa mwili wake na moyo wake pamoja na kukupa thamani kubwa katika maisha yake? Ipi thamani ya machozi yake kwako? Ipi thamani ya mapenzi yake kwako? Kwanini uliache penzi lako lenye furaha na kwenda kwa mtu mwingine ambaye wakati mwingine anaweza asifike hata nusu ya uliyenae?

Kumbukeni mapenzi ni hisia ambayo hukaa ndani kabisa ya moyo, hisia ambazo haziwezi kupuuzwa au kutokuthaminiwa. Hisia ambazo zinauwezo wa kukubadili jina kutoka fulani na kuwa marehemu fulani. Hisia ambazo huumiza zaidi ya kufiwa na ndugu na wakati mwingine hata wazazi wako.mwanamke au mwanaume anapokupenda huwa amekuona wewe na kukuchagua wewe kati ya wengi ambao amewaona.

Amekuchagua wewe kwa kuamini kuwa wewe ni faraja, furaha, liwazo na kumbatio la huba. Hakukupenda ili umsaliti na kuishusha thamani yake.. Hakukupenda ili umpange foleni na kumvunjia heshima, bali amekuoa kwa kuamini wewe ndio kilakitu katika maisha yake. Kama ni hivyo kwanini usimtunzie heshima yake? Kwanini usiipiganie thamani yake? Mwanamke aliyekupenda kweli unaweza ukamuacha akalia? Mwanaume uliyempenda kweli unaweza kumuacha akilia? Ni ipi thamani ya upendo wenu? Ni ipi heshima ya mapenzi yenu?

Mpaka kitu kikutoke mikononi ndio utambue heshima na thamani yake? Kipi ambacho ni kigeni kati ya ulichonacho na unachokifuata? Nani kakwambia papuchi zinautamu tofauti? Nani amekwambia nilichonacho mimi ndicho alichonacho sumbai au kaboom? Au unadhani alichonacho heaven sent ni tofauti na alichonacho badili tabia au madame s

tuondoe ujinga tuthamini tulivyonavyo sio mpaka viondoke mikononi mwetu ndio tugundue thamani zao.

Utamu wa maharage hauwezi kuwa tofauti bali ni upishi wako tu.

Muwe na usiku mwema
very touching words.
 
Tumekuwa wa kuonyesha kutaka kuthamini,kujali na kulinda punde tu tuwapo katika hatua ya kutaka ama kujenga uhusiano au muda mfupi tu tangu uhusiano uanze,tukipata tunasahau sijui huu ugonjwa utapona lini,tukiachwa tunajiwa na kumbukumbu na kuishia kujutia.
Tujaliwe wepesi katika hili.
 
​asalaam aliyekhum wana mmu,

nipo hapa mbele yenu kuwakumbusha kitu kimoja muhimu sana katika maisha yetu ya kila siku hasa yale ya kimahusiano.

Najua wote tunajua thamani ya mapenzi na pia tunafahamu ni jinsi gani mapenzi yanatesa, yanaumiza na wakati mwingine kuua. Wengi tunafahamu jinsi mapenzi yalivyoleta umoja, undugu na urafiki ambao haukutarajiwa katika maisha yetu lakini kutokana na huyu kuoa yule na yule kuolewa na huyu tumejikuta tukiunganishwa na jambo hilo.

Licha ya kujua thamani ya mapenzi na maumivu yake lakini tumeshindwa kuilinda thamani na kuyapuuza maamuvi yake. Tumekuwa wakosaji wakubwa sana kwa wenza wetu tulionao. Tumekuwa hatutambui thamani ya tulionao mpaka pale wanapoondoka mikononi mwetu. Tumekuwa watu tusiothamini mioyo na machozi ya wenza wetu kanakwamba sisi ni wanyama.

Kwanini umlize mwanaume aliyekupenda na kukusaidia katika maisha yako? Kwanini umsaliti mwanamke aliyekupa mwili wake na moyo wake pamoja na kukupa thamani kubwa katika maisha yake? Ipi thamani ya machozi yake kwako? Ipi thamani ya mapenzi yake kwako? Kwanini uliache penzi lako lenye furaha na kwenda kwa mtu mwingine ambaye wakati mwingine anaweza asifike hata nusu ya uliyenae?

Kumbukeni mapenzi ni hisia ambayo hukaa ndani kabisa ya moyo, hisia ambazo haziwezi kupuuzwa au kutokuthaminiwa. Hisia ambazo zinauwezo wa kukubadili jina kutoka fulani na kuwa marehemu fulani. Hisia ambazo huumiza zaidi ya kufiwa na ndugu na wakati mwingine hata wazazi wako.mwanamke au mwanaume anapokupenda huwa amekuona wewe na kukuchagua wewe kati ya wengi ambao amewaona.

Amekuchagua wewe kwa kuamini kuwa wewe ni faraja, furaha, liwazo na kumbatio la huba. Hakukupenda ili umsaliti na kuishusha thamani yake.. Hakukupenda ili umpange foleni na kumvunjia heshima, bali amekuoa kwa kuamini wewe ndio kilakitu katika maisha yake. Kama ni hivyo kwanini usimtunzie heshima yake? Kwanini usiipiganie thamani yake? Mwanamke aliyekupenda kweli unaweza ukamuacha akalia? Mwanaume uliyempenda kweli unaweza kumuacha akilia? Ni ipi thamani ya upendo wenu? Ni ipi heshima ya mapenzi yenu?

Mpaka kitu kikutoke mikononi ndio utambue heshima na thamani yake? Kipi ambacho ni kigeni kati ya ulichonacho na unachokifuata? Nani kakwambia papuchi zinautamu tofauti? Nani amekwambia nilichonacho mimi ndicho alichonacho sumbai au kaboom? Au unadhani alichonacho heaven sent ni tofauti na alichonacho badili tabia au madame s

tuondoe ujinga tuthamini tulivyonavyo sio mpaka viondoke mikononi mwetu ndio tugundue thamani zao.

Utamu wa maharage hauwezi kuwa tofauti bali ni upishi wako tu.

Muwe na usiku mwema
very touching words.
 
Mkuu kuna kitu unatakiwa kuwa nacho.jipe muda,penda maisha yako then kuwa selfish kidogo..ni kupe mfano mdogo mimi mtu aliondoka nikiwa kwenye hard time..masters inatesa,nimetoka kufiwa na uncle ambae alikuwa mshauri mkubwa kwangu then natoka kwenye msiba nafika home mzee anaumwa hatari halafu mtu anakwambia tuachane bila reason...hahahahahaha..wakati mwingine wadada wanashindwa kutambua nini wanataka kwenye mahusiano.mtu mpaka unafikir hivi ningemuacha situation kama hiyo yeye angekuwa vipi unakosa jibu.
Pole sana, ndo walivyo.
Sio kwako tu hutokea kwa watu wengi pia. Kuna jamaa yangu (sala tano) yeye ugomvi wake na mkewe ni kuhusu Pombe, jamaa hataki mkewe anywe Pombe, ila mkewe kwenye Pombe humwambii kitu. Juzi, kamtandika vibao kidogo, Mke kaja juu anatakata taraka yake. Na kwa kujiamini yeye ndiye aliyeleta karatasi na peni eti amwandikie talaka yake waachane. Jamaa akashituka, akalia sana kisha akaondoka. Mpaka leo hajlikani aliko. wanawake hawa, we acha tuuu.
A%20S%2012.gif
 
Sasa hiyo mm sifanyi sjafanya kosa nikuombe radhi hapana asee
KUOMBA Samahani KUNA THAMANI kubwa sana kwenye mahusiano, na hasa kama ikiwa unaona kiukweli kabisa kuwa umemkosea mwenzio.
 
shem ungeingia ndani ya moyo wangu nakujua nilichokibeba nadhani ungenishangaa kwanini naandika haya. Nimepanda Upendo wangu kwenye Mwamba ambao kamwe hakuna mmea ulio na uwezo wa kumelea..

Nikajitia upofu wakutokuona kila nilichotendewa. Niliziba masikio kwa ndugu na marafiki nikiamini kuwa nalinda penzi la mke wangu mtarajiwa lakini sikujua kuwa nilikuwa nikiuingiza Moyo Wangu kwenye moto.. Moto Ambao Umeniunguza na Kuufanya Moyo Wangu upoteze ule Ujasiri Wake..

Nililia sana, nilisimangwa sana, nilitukanawa na kuitwa majina ya kila aina lakini Yote hiyo kwa sababu nilimpenda, nilimjali na Kumthamini.. Sikutaka kumuoma Akilia lakini mimi alinifanya nilie. Sikutaka kumuona akiteseka, lakini akaniacha mimi katika mateso Makali... Hakika kuna mengi ambayo niliwaza mengi lakini sikuwa na thamani tena shem ila Mungu ni Mwema Kwangu..

Bado naishi lakini maisha yenye kumbukumbu mbaya sababu ya Mapenzi....

SIHITAJI KUPENDA TENA WALA KUPENDWA.. HIKI NINACHOPITIA SITAKI NISABABISHE MWINGINE AKIPITIE.. MOYO WANGU
. ibra87. Huwezi kuishi bila mapenzi Ibra, sote tumepitia huko. Unapenda, unaumizwa, unasahau, unapenda, unaumizwa,unasahau, unapenda............ Ndo mzunguko ulivyo. Kikubwa ni kujitambua na kujiuliza ni kwa nini uko kwenye mapenzi na huyo uliyenae sasa? Pamoja na sababu Milioni utakazokuwa nazo, nakushauri usipende kwa 100%, never ever do that. Penda kwa 50% tu, 30% iwe kwa ndugu zako(blood related) na 20% kwa wengineo(jamaa, marafiki, mchepuko n.k). kwa njia hiyo kama mpenzi wako uliyempa 50% atakuumiza, unabaki na other 50% ya kupenda wengine. Hata kama akikukera, utakereka kwa 50&, na utaendelea kuwa salama kwa 50% pia. Nawashauri, mkiingia kwenye mahusiano ili msije kufa kwa pressure na kujiua msipende kwa 100%, pendeni kwa kiwango mabacho akizidi 50%. Mwenye kutaka maelezo zaidi ani-PM
 
kama na wewe yamekugusa mkuu pole sana.. Ni wakati wakuthamini tulionao
Ibra mimi yamenitokea juzi juzi tu, nilichofanya nikachapa makofi mbaya, kisha nikaondoka zangu. Mtu anakukosea, hataki kutoa sababu kwa nini kakukosea na wala haombi msamaha. wewe uliyekosewa ndo unazungumza sana kuliko yeye, Makofi tu ndo dawa yao. Ili hata kama akiondoka, aondoke na kumbukumbu mbaya ili asiende kuwakosea wengine.
 
. ibra87. Huwezi kuishi bila mapenzi Ibra, sote tumepitia huko. Unapenda, unaumizwa, unasahau, unapenda, unaumizwa,unasahau, unapenda............ Ndo mzunguko ulivyo. Kikubwa ni kujitambua na kujiuliza ni kwa nini uko kwenye mapenzi na huyo uliyenae sasa? Pamoja na sababu Milioni utakazokuwa nazo, nakushauri usipende kwa 100%, never ever do that. Penda kwa 50% tu, 30% iwe kwa ndugu zako(blood related) na 20% kwa wengineo(jamaa, marafiki, mchepuko n.k). kwa njia hiyo kama mpenzi wako uliyempa 50% atakuumiza, unabaki na other 50% ya kupenda wengine. Hata kama akikukera, utakereka kwa 50&, na utaendelea kuwa salama kwa 50% pia. Nawashauri, mkiingia kwenye mahusiano ili msije kufa kwa pressure na kujiua msipende kwa 100%, pendeni kwa kiwango mabacho akizidi 50%. Mwenye kutaka maelezo zaidi ani-PM

hakika umenipa mwanga na nitazingatia hilo
 
Sasa sjakosa halafu bado nikuombe radhi hii hapana asee
Mademe, sometime tunafanya hivyo ili mambo yaishe vizuri. Baada ya masiku kupita na hasira za anayehisi kukosewa kwisha , mnaweza yazungumza nakusema your concern.
 
hakika umenipa mwanga na nitazingatia hilo
In additional to that, kama utakasiriswa na kukasirika, make sure that hasira zako zinabadilika na kufanya mambo chanya(Be positive and constructive always). kwa mfano baada ya kuumizwa na kulia, wewe nenda darasani kajisomee(kama ni mwanafunzi), kama ni mkulima nenda shamba kajilimie, kama mfanyabiashara, nenda kwenye biashar zako kazisimamie......................nk. kwa njia hiyo utamsangaza aliyekuumiza na matokeo yake utarudisha maumivu yake.
 
Mademe, sometime tunafanya hivyo ili mambo yaishe vizuri. Baada ya masiku kupita na hasira za anayehisi kukosewa kwisha , mnaweza yazungumza nakusema your concern.

weee nani kasema nimejifunza unajua unaloongea somehow upo sahihi ila unapong'atwa na nyoka ukisikia mtikisiko wa majani lazima ushtuke uhisi inwezekana akawa nyoka tena naomba samahani pale napokosea au kuhisi kumkosea au kumkwaza mtu kwa namna yoyote ile siombi radhi ili kuombwa radhi in return naomba radhi kwa maana kwamba nimejua kosa langu lilipo sijakukosea bado niombe rahi ha ha ha ha hingii akilini hata kidogo na wala sikuekei kinyongo et umenikosea nikukasirikie nehi sipo hivo kabisa na inategemea na makosa pia.
 
ni vigumu kurudia hilo na ni vigumu kuuruhusu Moyo Wangu kupenda.. Nafurahia kuishi hivi kwasasa
. Iko powa, ukibanwa na kikohozi unatafuta sehemu unalipia na kumaliza kikohozi chako na kusonga mbele. Unatengeneza maisha ya hivyo mpaka hapo utakapokuwa umepata chaguo sahii.
 
Back
Top Bottom