It’s official: America is now No. 2

It’s official: America is now No. 2

Wanatapa tapa tu hawa haters wa USA na kujipa faraja hewa.

Kama alivyosema mkuu Mag3 hapo juu, uchumi wa Marekani ukiyumba basi uchumi wa dunia nzima unayumba.

Tumeona majuzi tu hapa 2008.

China bado sana kwa Wamarekani.
Mkuu unachanganya habari sio kwamba uchumi wa US umeyumba bali wa China unakuwa kwa kasi kiasi kwamba wako karibu kuwapita wamarekani. Tofautisha kuyumba na kuzidiwa ni vitu viwili tofauti sana.
 
Mimi naona hata nyinyi mnafanya ushabiki tu. Mimi sina hakika na hizi data lakini kusema Marekani haiwezi kuanguka kama anavyosema "your buddy" hapo juu ni ujuha wa hali ya juu sana. Kwani Marekani ni nani hadi ishindikane kuanguka. Hata China ikimzidi mmarekani it is just a matter of atatokea mwingine akae juu ya China.

Kumbukeni kuwa the only permanent thing is change!!

Who is my buddy?

Kwa nini unilishe maneno yake?

Kama jua litazimika kwa nini Marekani isianguke siku moja?

Hakuna ambacho hakianguki, it is against the second law of thermodynamics.

The devil is in the details.

You probably are going to see Tanzania split asunder before you see the USA do the same.
 
Mkuu unachanganya habari sio kwamba uchumi wa US umeyumba bali wa China unakuwa kwa kasi kiasi kwamba wako karibu kuwapita wamarekani. Tofautisha kuyumba na kuzidiwa ni vitu viwili tofauti sana.

Uchumi wa Marekani ni mkubwa sana hadi hauna tena nafasi kubwa ya kukua.

Sijui kama unaielewa hiyo dhana.
 
Ushawi kuona vijiji vya China?

Mbona huongelei kuhusu watoto omba omba na maskini kuongezeka USA?Na sijui Kama unafahamu most americans are not insured in terms of their healthy.Obamacare ni bomu tu,US citizen wengi wanaenda tu hospital kama akina mimi huku Tanzania unalipia then unaandikiwa prescription because most of them cannot afford the healthy insurance system.U still call that a lasting big economy in the world?Never.

Nearly one in four US children lives in poverty, the highest level in 20 years, with a similar proportion not getting enough food to eat. These were among the findings of an article published last week in the medical journal JAMA Pediatrics, entitled Seen but Not Heard: Children and US Federal Policy on Health and Health Care.

Je mbona huongelei wasio na makazi (homeless) kuongezeka mfano tu Newyork city?
The number of homeless people living on the streets of New York City increased by 23 percent in one year according to an annual survey conducted by the city’s Department of Homeless Services.
 
Mbona huongelei kuhusu watoto omba omba na maskini kuongezeka USA?

Weka takwimu.

Na sijui Kama unafahamu most americans are not insured in terms of their healthy.

Most Americans don't have health insurance? Weka takwimu.

Obamacare ni bomu tu,US citizen wengi wanaenda tu hospital kama akina mimi huku Tanzania unalipia then unaandikiwa prescription because most of them cannot afford the healthy insurance system.U still call that a lasting big economy in the world?Never.

Really? Provide your source(s).

Nearly one in four US children lives in poverty, the highest level in 20 years, with a similar proportion not getting enough food to eat. These were among the findings of an article published last week in the medical journal JAMA Pediatrics, entitled Seen but Not Heard: Children and US Federal Policy on Health and Health Care.

Poverty in the United States is not the same as the poverty in other countries.

Je mbona huongelei wasio na makazi (homeless) kuongezeka mfano tu Newyork city?

Hao wengi wana matatizo yao binafsi tu. Kama mimi Mnyantuzu niliyetokea Ikungulyabashashi ninaishi kwenye gated community nini kinachowashinda hao wengine hata kuishi kwenye Section 8 housing? Marekani social welfare programs zipo nyingi tu hadi kupelekea watu ku-game the system.

The number of homeless people living on the streets of New York City increased by 23 percent in one year according to an annual survey conducted by the city's Department of Homeless Services.

And what is the actual number of those homeless people?
 
Ila mi naona afadhali kwa masikin wa china kuchoma mahindi kuliko masikin wa marekani kucheza video za x.
mimi naona wewe hujawahi safari, unajua huyo mcheza shoo ya x inabidi uumpe mshahara wa manager ili aishi Tanzania
 
Unapewa choice ys passport ya uchina au USA utachagua ipi???? naona mjadala umekwisha
 
Unajua population ya Japan? Ya US?????? Brazil????Russia??????

Unaongelea soko...unawezaje kuuza kwa masikini?

Population mtaji ndio maana EA tunataka tuungane...

Unadhani kwa nini uchumi wa Ethiopia kwa sasa unakua kwa kasi ya ajabu?
Umehoji population ya nchi mbalimbali... hoja yako inasimama wapi katika huko kuhoji? Kama ni kulinganisha na China, hakuna hata moja ambayo population yake imefikia japo robo ya China... afadhali US ndio inakaribi au labda ndo umefika hiyo robo!!

Tukirudi kwenye soko... bahati mzuri mwenyewe umeshasema kwamba "Population mtaji ndio maana EA tunataka tuungane...!" NI kweli, population ni mtaji na ni mtaji wa kuvutia investors sio wa kutajirisha wananchi ndio maana duniani kote, including China kuna suala la birth control kwa ajili ya ku-minimize population growth!! Population is an opportunity for investors but threat for any government!

Unatoa mfano wa Ethiopia kwamba uchumi unakua... unapozungumzia masuala ya kiuchumi tofautisha kati ya Economic Growth na Economic Development! Kinachotokea Ethiopia to date ni economic growth! In the long run, economic growth ndio inaleta economic development but this takes time... couple of decades unless nchi husika igundue raslimali kubwa huku ikiwa na manageable population!

Unahoji unawezaje kuuza kwa maskini... Kwanza naona unataka ku-exaggerate mambo! Hakuna aliyesema China ni maskini nilichosema ni kwamba, ingawaje GDP ya China ni kubwa kuliko US lakini bado itachukua muda, a decade or so, kwa China kuipiku US in terms of economic development na ndio maana nikakupa mfano wa rahisi sana.. pa capita income; kwamba, ingawaje GDP ya China ipo juu kidogo ya ile ya US lakini per capita ya US ni mara nne ya ile ya China! Kutokana na ukweli huo, ndio maana ni nchi za Scandinavia ndizo zinaongoza kwenye ustawi wa jamii coz' population ya zile nchi ni ndogo na sidhani kama kuna any Scandinavian country ambayo population yake ina-exceed 10 million lakini zote si miongoni mwa nchi zenye GDP kubwa duniani!

Kama bado hujaona effect ya population kwenye economic development basi ningekushauri pitia upya makarabrasha yako ya uchumi!!
 
Mchina akipata japo scholarshp za america anashangilia, wanannchi wa china wanamaisha duni sana, bado sana china kufikia level za USA
 
Mbona huongelei kuhusu watoto omba omba na maskini kuongezeka USA?Na sijui Kama unafahamu most americans are not insured in terms of their healthy.Obamacare ni bomu tu,US citizen wengi wanaenda tu hospital kama akina mimi huku Tanzania unalipia then unaandikiwa prescription because most of them cannot afford the healthy insurance system.U still call that a lasting big economy in the world?Never.

Nearly one in four US children lives in poverty, the highest level in 20 years, with a similar proportion not getting enough food to eat. These were among the findings of an article published last week in the medical journal JAMA Pediatrics, entitled Seen but Not Heard: Children and US Federal Policy on Health and Health Care.

Je mbona huongelei wasio na makazi (homeless) kuongezeka mfano tu Newyork city?
The number of homeless people living on the streets of New York City increased by 23 percent in one year according to an annual survey conducted by the city's Department of Homeless Services.
Nafikiri hujaishi US na tukiachana na internal politics za Marekani when it comes down to taking care of themselves America is number ONE. Mengi ya unayoyaongelea ni by choice k.m. mtu anaitwa homeless lakini analala mtaani ndani ya SUV au mtu analala kwenye veranda mtaani lakini nyumba yake kapangisha. Kulala mtaani mara nyingi pia ni by choice; ziko centers unaweza kulala unavyopenda na bila bughdha.

Kulala njaa
Marekani ni by choice, kuna centers unakula hadi unasaza...achana na walioathirika kwa madawa which is also by choice. Hakuna mgonjwa aliyezidiwa akakosa matibabu awe na insurance au asiwe nayo. Nchi gani duniani inawapa huduma zaidi 20 milion illegal immigrants bila kuomba msaada ikiwahudumia kwa chakula, malazi, matibabu n.k.. Amerika ina akiba ya chakula ambacho namna pekee ya kukipunguza ni kutoa misaada kwa nchi zenye njaa. Watanzania wote tunaweza kuhamia US na wasipate mtikisiko.

Amerika ina akiba ya silaha ambayo namna pekee ya kuicontrol ni kutoa misaada kwa wanotaka kuuana au kuzitumia ndani ya nchi zisizotaka amani. Hakuna nchi yenye misukosuko (natural disasters) kama Marekani, ya moto, ya mafuriko, ya tetemeko, ya landslide, ya hali ya hewa you name it, kuliko Marekani lakini hawategemei misaada na badala yake hakuna nchi inayotoa misaada kuliko Marekani na bila kujali itikadi za nchi hizo...hizi ni huduma za jamii tu sijagusa elimu na sayansi and the list goes on.

Marekani ina mipango ya muda mfupi na mrefu hadi wa miaka mia ijayo. Marekani ina akiba ya mafuta na gesi kuliko nchi nyingi...swali ni kwa nini wahangaike kuiharibu environment yao kumbe kuna wajinga wanachimba ovyo mafuta! Wanayo miji chini ya miji, bahari na milima...Je unajua kiasi wanachotumia kupeleka vyombo angani? Unajua kiasi wanachotumia kuwatunza mbwa, paka na wanyama wengine?
 
Uchumi wa Marekani ni mkubwa sana hadi hauna tena nafasi kubwa ya kukua.

Sijui kama unaielewa hiyo dhana.
Kwavile nimesoma Chemistry na Economics, labda niifafanue hiyo dhana ki-chemistry ili wale ambao hawajasoma Economics lakini wamesoma sayansi, Chemistry wapate kuelewa vizuri! Hicho ulichosema ni kile ambacho kipo kwenye makundi ya Unsaturated Solution, Saturated Solution na Super Saturated Solution!!

Ukichukua maji ya kawaida na kuweka kwenye sufuria, kisha ukaweka chumvi kidogo, hii itakuwa unsaturated solution kwavile chumvi itayeyuka! Kadri utakavyoongeza chumvi, chumvi itaendelea kuyeyuka YOTE lakini itafika wakati, kadri unapoongeza, chumvi itayeyuka lakini nyingine itabaki chini bila kuyeyuka! Ikishafikia hii hali, inakuwa saturated salution... kwamba kila kiasi unachoweka, kiasi kinayeyuka na kiasi kinabaki bila kuyeyuka to the point, kiasi kinachoyeyuka kinakuwa kidogo zaidi kuliko kile kinachoyeyuka... na kadri utakavyoongoza, itafika wakati, to any amount unayoongeza, hakuna kitakachoyeyuka na hivyo kuwa Super Saturated Solution!!!

Ingawaje Uchumi wa US bado haujafikia kwenye hiyo state ya super saturated solution lakini umeshapita kwenye unsaturated solution na upo kwenye saturated huku ukiwa unainamia kwenye super saturated na ndio maana utakuta annual growth yake inakuwa below 5%... all factors of economy in US are fully exploited!
 
Mkuu unachanganya habari sio kwamba uchumi wa US umeyumba bali wa China unakuwa kwa kasi kiasi kwamba wako karibu kuwapita wamarekani. Tofautisha kuyumba na kuzidiwa ni vitu viwili tofauti sana.
Unachosema China karibu itaipita Marekani ni GDP... hata ikiwa na GDP kubwa kuliko US lakini bado US ipo juu sana ya China!
 
Hivi hyo 2019 wao USA watakuwa wamelala tu hadi wapitwe?
Nchi yenye watu 300+ million watu wanailinganisha na Billion + people
 
Wachina wanakuja kuuza miili hadi huku bongo nchi masikini!, hii inareflect hali halisi ya kwao
 
Kwa kuwalinda tu wana wa israel kamwe mwenyezi MUNGU hawezi kuicha marakani ianguke
 
China itaizidi tu marekani siku moja...hata india itaizidi marekani....leo hii Brazil imeshaizidi UK kiuchumi....hata japan kuizidi ujerumani ilionekana ni kusadikika...but ni reality now for decades...

Hivi Brazil pesa yao inaitwaje? Nicheke mie .. .... ... khe khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee bora niendelee tu kukaa huku Alaska Brazil wanasingiziwa tu.
 
Back
Top Bottom