Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,208
- 10,965
Ikiwa ni miezi sita kamili tangu vita vianze baina ya Hamas na Israel,na baada ya vifo vingi vya raia na askari wa Israel,na baada ya Israel kuwaudhi washirika wake, hatimae leo jeshi hilo limeamua kurudisha nyuma vikosi vyake kutoka kusini ya Gaza na Rafah.
Baadhi ya taarifa zinaeleza kuwa maelfu ya askari wanaorudi nyuma ni wale ambao wameamua kukimbia vita kurudi nyumbani.
Katika maelezo yake Israel kupitia redio ya channel 2 , imesema inarudisha nyuma jeshi kutokana na kukamilisha majukumu yao na kwamba Gaza nzima imeachwa na brigedi moja tu ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuangalia uzio ambao umewekwa ili kuzuia wapalestina waliokimbilia kusini wasirudi tena kaskazini ya Gaza.
Itakumbukwa kuwa waziri mkuu wa Israel.Benjamin Netanyahu mwanzoni alisema lazima mateka wapatikane kabla ya Ramadhani ama sivyo hakuna kingemzuia kuingia Rafah.Hata hivyo mwezi umeisha na Hamas hakurudisha hata mateka mmoja.
Na vile vile wakati mwezi wa Ramadhani ukikaribia kuisha idadi ya vifo vya askari wa IDF kwenye maeneo yale yale Israel iliyojitangazia ushindi vimekuwa vikiongezeka sana kutokana na kuongezeka kwa mapigano.
Kurudishwa kwa vikosi hivyo kumeleta sherehe kwa wapalestina na pia kuleta kuchanganyikiwa kwa baadhi ya wafuatiliaji wa vita hivyo.
Chanzo: Aljazeera.