Naona unarudia kosa lile lile. Nasubiri majibu ya maswali yangu. Hakuna aya iliyo onyesha ya kuwa Uyahudi si ukafiri katika ulizo weka wewe.Eti unauliza kama nimeshasoma tafsiri yoyote ya Qur'an tukufu!!!?--- kwani hizo tafsiri zimetoka kwa mtume (saw) ??!!.
Qur'an inajitafsiri yenyewe, hebu angalia hizi aya:-
1----- Kila ummati tumewajalia kawaida ya ibada wanayoishikilia basi wasikugombeze katika jambo hili na uite kwa mola wako bila shaka wewe upo juu ya muongozo. (22:67) Qur'an .
2----Hakika walioamini na mayahudi na masabii na wakristo waliomuamini Allah na siku ya mwisho na WAKATENDA MEMA basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
(5:69) Qur'an
3"------ basi hapana shaka zingalivyunjwa nyumba za watawa na MAKANISA na MASINAGOGI na MISIKITI ambamo ndani yake jina la ALLAH linatajwa kwa WINGI.
(22:69) Qur'an .
Hizo aya tatu zinaonyesha kuwa UYAHUDI SIO UKAFIRI lakini hazijasema kwamba Mayahudi hawawezi kuwa makafiri, tofautisha kati ya UYAHUDI na MAYAHUDI.
Sasa wewe onyesha aya inayosema UYAHUDI NI UKAFIRI.
Aya inayokuchanganya ni hii:-
ان الدين عند الله الاسلام Hakika dini mbele ya Allah ni Uisilamu (3:19).
Kwa uwezo wako mdogo wa ufahamu wewe unaona kwamba hiyo aya anapinga ukweli wa dini zingine, Hiyo inashadidia UKWELI NA UZURI WA UISILAMU DHIDI YA DINI ZINGINE ZILIZOLETWA NA MANABII WALIOPITA, YAANI UISILAMU NI DINI ILIYOKAMILIKA KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA YA BINADAMU, Dini zingine hazijakamilika na vitabu vyao vimeishaingizwa mikono na kama atapatika mtu mwema katika dini hizo ALIYEMUAMINI ALLAH na SIKU YA MWISHO na KUTENDA MEMA (5:69) basi hatakuwa na khofu na hatahuzunika, na hii ni pamoja na Waumini (Waisilamu)----- kumbuka yule anayemuamini Allah ni lazima pia atamuamini mtukufu mtume (saw).
Usipokubali jambo hili basi basi utasababisha ikhitilafu katika aya za Qur'an, (aya 5:69 na aya 3:19).
----Unataka kujua maana ya ukafiri na ushirikina----.
Je Kwanza umeelewa tofauti kati ya UYAHUDI na MAYAHUDI ? ??, mbona warukia mada mpya??
Pili,hujajibu maswali yangu na sijatoka nje ya mada.
Tafsiri zinatoka kwa mtume na aya hujifasiri kwa zenyewe ila si kwa namna unayofanya wewe.
Nasubiri majibu ya maswali niliyo kuuliza.