ISRAEL SIO TAIFA TEULE
Natumaini mu wazima wote.
Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kwenye mambo mbalimbali. Leo nyundo yangu itagonga kwenye hii kauli kwamba Israel ni taifa teule na atakayeilaani Israel naye atalaaniwa pia atakaeibariki naye atabarikiwa. Ila kwanza nitoe pongezi zangu kwa Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa nchi yetu. Ninafurahishwa pia kwa hatua kadhaa anazochukua ili kuweka mambo sawa. Kumsimamisha kazi fedhuli Sabaya ni jambo lililonifurahisha kuliko yote yaliyowahi kufanywa na marais wa nchi hii.
Ndugu Sabaya ni mfano halisi wa mtu katili.. wengi wetu ni wahanga wa ukatili wake. Kwa asiyeelewa vizuri kiwango cha ukatili wa Sabaya akatazame movie ya Idd Amin ili kujua kiasi cha ukatili kwasababu hakipishani sana na kina Idd Amin na Malyamungu. Lakini sijafurahi Mheshimiwa Polepole kutolewa kwenye uenezi CCM. Ali-fit sana pale. Anyway, CCM ni kubwa kuliko mtu. Kidumu chama cha mapinduzi! Zidumu fikra za mwenyekiti.
"ISRAEL NI TAIFA TEULE" ni kauli maarufu sana kwenye vinywa vya waumini wengi wa dini ya kikristo. Mimi ni mkristo na ninaamini katika biblia na pia naamini Yesu Kristo ndo masihi aliyetumwa afe kwa ajili yetu tupate kuokoka. Lakini ninapinga kwa nguvu zote kwamba Israel ni taifa teule kwamba atakayalilaani atalaaniwa na atakayelibariki atabarikiwa. Kwangu mimi ni upumbavu uliotukuka kuamini hivyo. Msingi wa hoja ya wakristo wengi katika hili upo kwenye biblia kitabu cha Mwanzo.
Kuna wakati Mungu alimbariki Ibrahim na Yakobo (Israel) na kuwaahidi atabariki hadi vizazi vyao. Hili ni sawa kwasababu Mungu ni mwema na mwenye upendo na hubariki watu wake. Kila binadamu anapozaliwa hupata zawadi ya kipaji fulani kutoka kwa Mungu. Kila mmoja wetu ana kipaji chake. Na ukimcha Mungu hukupa zawadi nyingi zaidi. Kwa kusema hivyo ni kwamba Yakobo ambaye baada ya kupata baraka zake alibadilishwa jina na kuitwa Israel alipata baraka zake kama ilivyo binadamu wote.
Pamoja na baraka za Mungu bado haitufanyi tuwe wateule na wengine wasiwe wateule. Mungu hutupa baraka zake bila kujali kama tutakuja kukiuka maagizo yake au la. Kwahiyo nje ya baraka kuna maisha mengine yanaendelea. Waisrael hawana uteule wowote ni kama walivyo watanzania, wacongo au taifa lolote lile. Ninaandika haya kwa uchungu mno kwasababu ya matendo maovu wanayoyafanya dhidi ya wapalestina halafu mpuuzi mmoja anatetea kwa kusema ni taifa teule.
Hawa viumbe hawana uteule wowote ule. Kwanza kihistoria ni watu wa kutangatanga sana matokeo yake wakajikuta "hawana kwao". Biblia inaonyesha kwamba baba wa Israel aliyekuwa akijulikana kama Yakobo mwanzoni alitenda dhambi ya uongo kwa kuchukua baraka za mzaliwa wa kwanza kihuni ambapo baada ya lile tukio huyu mtu alikuwa wa kutangatanga hadi leo hii. Na kama Israel ni taifa teule ikawaje wakaachwa watawaliwe na warumi na hata karne iliyopita walichomwa moto kikatili na Adolf Hitler. Nimalizie kwa kusema kwamba kinachoendelea GAZA ni ushetani uliovuka mipaka yote ya kistaarabu na wa kulaaniwa.
Haiwezekani wapumbavu fulani katika kivuli cha ukristo wakawa na utetezi dhaifu kwamba taifa teule lina haki ya kuua watu kama nzige kisa mwasisi wao kuna kipindi alibarikiwa. Mungu wetu ni wa upendo na asihusishwe na unyama unaofanywa na wayahudi. Pia wakristo wenye kiherehere cha kuwatetea wayahudi watambue hao ndo walimuua Yesu kikatili.
Pilato aliyekuwa hakimu alitaka kutumia nafasi ya kusamehe mfungwa mmoja ili Yesu asalimike ila hao "Taifa teule" wakaona bora jambazi Baraba aachiwe ili Yesu asulubiwe. Na "taifa teule" sio wakristo hivyo hata wenyewe wanashangaa baadhi yetu tunavyoshoboka.