Israel siyo taifa teule

Israel siyo taifa teule

ISRAEL SIO TAIFA TEULE

Natumaini mu wazima wote.

Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kwenye mambo mbalimbali. Leo nyundo yangu itagonga kwenye hii kauli kwamba Israel ni taifa teule na atakayeilaani Israel naye atalaaniwa pia atakaeibariki naye atabarikiwa. Ila kwanza nitoe pongezi zangu kwa Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa nchi yetu. Ninafurahishwa pia kwa hatua kadhaa anazochukua ili kuweka mambo sawa. Kumsimamisha kazi fedhuli Sabaya ni jambo lililonifurahisha kuliko yote yaliyowahi kufanywa na marais wa nchi hii.

Ndugu Sabaya ni mfano halisi wa mtu katili.. wengi wetu ni wahanga wa ukatili wake. Kwa asiyeelewa vizuri kiwango cha ukatili wa Sabaya akatazame movie ya Idd Amin ili kujua kiasi cha ukatili kwasababu hakipishani sana na kina Idd Amin na Malyamungu. Lakini sijafurahi Mheshimiwa Polepole kutolewa kwenye uenezi CCM. Ali-fit sana pale. Anyway, CCM ni kubwa kuliko mtu. Kidumu chama cha mapinduzi! Zidumu fikra za mwenyekiti.

"ISRAEL NI TAIFA TEULE" ni kauli maarufu sana kwenye vinywa vya waumini wengi wa dini ya kikristo. Mimi ni mkristo na ninaamini katika biblia na pia naamini Yesu Kristo ndo masihi aliyetumwa afe kwa ajili yetu tupate kuokoka. Lakini ninapinga kwa nguvu zote kwamba Israel ni taifa teule kwamba atakayalilaani atalaaniwa na atakayelibariki atabarikiwa. Kwangu mimi ni upumbavu uliotukuka kuamini hivyo. Msingi wa hoja ya wakristo wengi katika hili upo kwenye biblia kitabu cha Mwanzo.

Kuna wakati Mungu alimbariki Ibrahim na Yakobo (Israel) na kuwaahidi atabariki hadi vizazi vyao. Hili ni sawa kwasababu Mungu ni mwema na mwenye upendo na hubariki watu wake. Kila binadamu anapozaliwa hupata zawadi ya kipaji fulani kutoka kwa Mungu. Kila mmoja wetu ana kipaji chake. Na ukimcha Mungu hukupa zawadi nyingi zaidi. Kwa kusema hivyo ni kwamba Yakobo ambaye baada ya kupata baraka zake alibadilishwa jina na kuitwa Israel alipata baraka zake kama ilivyo binadamu wote.

Pamoja na baraka za Mungu bado haitufanyi tuwe wateule na wengine wasiwe wateule. Mungu hutupa baraka zake bila kujali kama tutakuja kukiuka maagizo yake au la. Kwahiyo nje ya baraka kuna maisha mengine yanaendelea. Waisrael hawana uteule wowote ni kama walivyo watanzania, wacongo au taifa lolote lile. Ninaandika haya kwa uchungu mno kwasababu ya matendo maovu wanayoyafanya dhidi ya wapalestina halafu mpuuzi mmoja anatetea kwa kusema ni taifa teule.

Hawa viumbe hawana uteule wowote ule. Kwanza kihistoria ni watu wa kutangatanga sana matokeo yake wakajikuta "hawana kwao". Biblia inaonyesha kwamba baba wa Israel aliyekuwa akijulikana kama Yakobo mwanzoni alitenda dhambi ya uongo kwa kuchukua baraka za mzaliwa wa kwanza kihuni ambapo baada ya lile tukio huyu mtu alikuwa wa kutangatanga hadi leo hii. Na kama Israel ni taifa teule ikawaje wakaachwa watawaliwe na warumi na hata karne iliyopita walichomwa moto kikatili na Adolf Hitler. Nimalizie kwa kusema kwamba kinachoendelea GAZA ni ushetani uliovuka mipaka yote ya kistaarabu na wa kulaaniwa.

Haiwezekani wapumbavu fulani katika kivuli cha ukristo wakawa na utetezi dhaifu kwamba taifa teule lina haki ya kuua watu kama nzige kisa mwasisi wao kuna kipindi alibarikiwa. Mungu wetu ni wa upendo na asihusishwe na unyama unaofanywa na wayahudi. Pia wakristo wenye kiherehere cha kuwatetea wayahudi watambue hao ndo walimuua Yesu kikatili.

Pilato aliyekuwa hakimu alitaka kutumia nafasi ya kusamehe mfungwa mmoja ili Yesu asalimike ila hao "Taifa teule" wakaona bora jambazi Baraba aachiwe ili Yesu asulubiwe. Na "taifa teule" sio wakristo hivyo hata wenyewe wanashangaa baadhi yetu tunavyoshoboka.
100%✓
 
Labda uniambie nikuonyeshe mara ngapi ?

Swali langu hujajibu na najua huwezi kujibu,umemzulia uongo nabii wa Allah Musa kwamba amekuja na Dini ya Uyahudi. Naomba uweke uthibitisho wa hayo uliyo yaandika.

Unaposema Uyahudi ni kama ulivyo kuwa Uislamu ina maana Uyahudi ni usahihi maana yake kama si Ukafiri. Uko wapi na aya ya Allah katika sura ya 5,anasema Allah :

3. ".....Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. " (al-Maaidah : 3)

Uyahudi ni kama Uislamu kwenye nini ? Kama Uyahudi si ukafiri wala si Ushirikina,niambie Uyahudi ni nini hasa ? Sababu hababu hata Ubudha nao ni Dini,je ni Dini ya Allah au ? Usikwepe swali.

Wewe umeishia madrasa ndiyo shida, Judaism ndiyo uyahudi ndiyo dini aliyokuja nayo nabii Musa as na kitabu chake ni Taurati, Taurati ndicho kitabu cha sheria kwa Mayahudi, nyumba zao za ibada ni sinagogi, chukua Mfano huu: Uisilamu uliojengwa katika nguzo tano umeletwa na Nabii Muhammad saw, kitabu chake ni Qur'an na nyumba zake za ibada ni misikiti.

Unang'ang'ania tu ujinga kama mtu usiyeenda shule KABISAAAA !!!

Jifunze mambo mema hata kutoka kwa mtu unayemchukia, Mtume saw alipata kusema "jambo lolote jema ni hazina ya Muisilamu auchukue popote atakapoikuta"--- chukua hazina hii kutoka kwangu japo wanichukia.
 
Hujui kwamba Uyahudi uliletwa na nani??!!, kesho utauliza Ukristo nao uliletwa na nani na ulifundisha nini??.
Nimekuuliza swali hilo ili kuonyesha ujinga wako na uongo wako ulipo,ndiyo maana mpaka muda huu unashindwa kuleta ushahidi ya kuwa nabii Musa ndiyo ameleta Uyahudi.

Ukileta uzushi kama huu pia katika Ukristo lazima nikuulize swali hilo ili kuonyesha ujinga wako,yaani uje kuniambia kwamba nabii Isa ndiyo alileta Ukristo,nikuache hivi hivi. Lazima nikurarue.
Hamna lolote isipokuwa ni midomo myepesi kutusi watu kwa kuwaita "Maqadian" na kuwakufurisha watu wa dini zingine ambazo Allah mwenyewe anakiri baadhi ya wafuasi wao ni watu wema na atawalipa kwa wema wao. Allah mwenyewe anawakiri wafuasi wema wa dini hiyo ya Uyahudi wewe unapinga kwamba dini hizo ni UKAFIRI, sasa kama dini zao ni ukafiri iweje Allah awaahidi malipo siku ya Qiyama???!!, huo wema watakaolipwa nao wamejifunza kupitia mafundisho gani??
Kijana mbona unalalama bila hoja wala ushahidi. Maqadiani ndiyo ni makafiri hili liko wazi tangu zamani. Uyahudi kadhalika na Ukristo nao ni Ukafiri,hawa wameanza kuitwa na Allah mwenyewe mimi nani nisiwaite ?

Sasa kwani mtu akiwa mwema ndiyo si kafiri ? Kijana unauapima vipi haya mambo ? Hapa hoja ni kwamba pamoja na huo wema wao je matendo yao Allah anayakubali ?

Weka aya inayo onyesha kwamba Allah amewaahudi watu pepo,maana haya ndiyo malipo ya wema siku ya Qiyama.
 
Rudi tuition huijui biblia, kama vipi tangua maandiko matakatifu yaliyoandikwa kwenye Biblia.
Bible ililetwa wakati wa ukoloni, wazungu walichukuwa Mali zetu wakaacha mashimo na Bible sisi tukashikilia Bible. Uislamu uliletwa wakati wa utumwa ukaanzia pwani na njia za watumwa walikopitia.
 
ISRAEL SIO TAIFA TEULE

Natumaini mu wazima wote.

Leo tena natumia haki yangu ya kikatiba kutoa maoni yangu kwenye mambo mbalimbali. Leo nyundo yangu itagonga kwenye hii kauli kwamba Israel ni taifa teule na atakayeilaani Israel naye atalaaniwa pia atakaeibariki naye atabarikiwa. Ila kwanza nitoe pongezi zangu kwa Mama Samia Suluhu Hassan kuwa Rais wa nchi yetu. Ninafurahishwa pia kwa hatua kadhaa anazochukua ili kuweka mambo sawa. Kumsimamisha kazi fedhuli Sabaya ni jambo lililonifurahisha kuliko yote yaliyowahi kufanywa na marais wa nchi hii.

Ndugu Sabaya ni mfano halisi wa mtu katili.. wengi wetu ni wahanga wa ukatili wake. Kwa asiyeelewa vizuri kiwango cha ukatili wa Sabaya akatazame movie ya Idd Amin ili kujua kiasi cha ukatili kwasababu hakipishani sana na kina Idd Amin na Malyamungu. Lakini sijafurahi Mheshimiwa Polepole kutolewa kwenye uenezi CCM. Ali-fit sana pale. Anyway, CCM ni kubwa kuliko mtu. Kidumu chama cha mapinduzi! Zidumu fikra za mwenyekiti.

"ISRAEL NI TAIFA TEULE" ni kauli maarufu sana kwenye vinywa vya waumini wengi wa dini ya kikristo. Mimi ni mkristo na ninaamini katika biblia na pia naamini Yesu Kristo ndo masihi aliyetumwa afe kwa ajili yetu tupate kuokoka. Lakini ninapinga kwa nguvu zote kwamba Israel ni taifa teule kwamba atakayalilaani atalaaniwa na atakayelibariki atabarikiwa. Kwangu mimi ni upumbavu uliotukuka kuamini hivyo. Msingi wa hoja ya wakristo wengi katika hili upo kwenye biblia kitabu cha Mwanzo.

Kuna wakati Mungu alimbariki Ibrahim na Yakobo (Israel) na kuwaahidi atabariki hadi vizazi vyao. Hili ni sawa kwasababu Mungu ni mwema na mwenye upendo na hubariki watu wake. Kila binadamu anapozaliwa hupata zawadi ya kipaji fulani kutoka kwa Mungu. Kila mmoja wetu ana kipaji chake. Na ukimcha Mungu hukupa zawadi nyingi zaidi. Kwa kusema hivyo ni kwamba Yakobo ambaye baada ya kupata baraka zake alibadilishwa jina na kuitwa Israel alipata baraka zake kama ilivyo binadamu wote.

Pamoja na baraka za Mungu bado haitufanyi tuwe wateule na wengine wasiwe wateule. Mungu hutupa baraka zake bila kujali kama tutakuja kukiuka maagizo yake au la. Kwahiyo nje ya baraka kuna maisha mengine yanaendelea. Waisrael hawana uteule wowote ni kama walivyo watanzania, wacongo au taifa lolote lile. Ninaandika haya kwa uchungu mno kwasababu ya matendo maovu wanayoyafanya dhidi ya wapalestina halafu mpuuzi mmoja anatetea kwa kusema ni taifa teule.

Hawa viumbe hawana uteule wowote ule. Kwanza kihistoria ni watu wa kutangatanga sana matokeo yake wakajikuta "hawana kwao". Biblia inaonyesha kwamba baba wa Israel aliyekuwa akijulikana kama Yakobo mwanzoni alitenda dhambi ya uongo kwa kuchukua baraka za mzaliwa wa kwanza kihuni ambapo baada ya lile tukio huyu mtu alikuwa wa kutangatanga hadi leo hii. Na kama Israel ni taifa teule ikawaje wakaachwa watawaliwe na warumi na hata karne iliyopita walichomwa moto kikatili na Adolf Hitler. Nimalizie kwa kusema kwamba kinachoendelea GAZA ni ushetani uliovuka mipaka yote ya kistaarabu na wa kulaaniwa.

Haiwezekani wapumbavu fulani katika kivuli cha ukristo wakawa na utetezi dhaifu kwamba taifa teule lina haki ya kuua watu kama nzige kisa mwasisi wao kuna kipindi alibarikiwa. Mungu wetu ni wa upendo na asihusishwe na unyama unaofanywa na wayahudi. Pia wakristo wenye kiherehere cha kuwatetea wayahudi watambue hao ndo walimuua Yesu kikatili.

Pilato aliyekuwa hakimu alitaka kutumia nafasi ya kusamehe mfungwa mmoja ili Yesu asalimike ila hao "Taifa teule" wakaona bora jambazi Baraba aachiwe ili Yesu asulubiwe. Na "taifa teule" sio wakristo hivyo hata wenyewe wanashangaa baadhi yetu tunavyoshoboka.
Huyo mparastina anaejitoa muhanga daily ndio taifa la Mungu?
 
Wewe umeishia madrasa ndiyo shida, Judaism ndiyo uyahudi ndiyo dini aliyokuja nayo nabii Musa as na kitabu chake ni Taurati, Taurati ndicho kitabu cha sheria kwa Mayahudi, nyumba zao za ibada ni sinagogi, chukua Mfano huu: Uisilamu uliojengwa katika nguzo tano umeletwa na Nabii Muhammad saw, kitabu chake ni Qur'an na nyumba zake za ibada ni misikiti.
Weka ushahidi huo na unionyeshe ya kuwa kipindi cha nabii Musa Uyahudi ulikuwepo.

Kijana unakwama wapi. Kipindi ambacho mnapindisha maana za aya wenzenu wanafanya utafiti na kusoma. Weka ushahidi huo.

Aya ya 69 katika sura ya 5, inaongelea ya kuwa endapo hao Mayahudi na Wakristo wakimuaani Allah na yale aliyokuja nayo Mtume na wakafanya mema basi watalipwa pepo. Maana yake hao wanakuwa ni Wafuasi wa mtume sasa yaani Waislamu. Rejea Tafsiri ya Ibn Kathiri.
 
Unang'ang'ania tu ujinga kama mtu usiyeenda shule KABISAAAA !!!

Jifunze mambo mema hata kutoka kwa mtu unayemchukia, Mtume saw alipata kusema "jambo lolote jema ni hazina ya Muisilamu auchukue popote atakapoikuta"--- chukua hazina hii kutoka kwangu japo wanichukia.
Nasubiri majibu ya maswali niliyo kuuliza.

Hizi nyingine ni porojo tu,hazibadilishi ukweli.
 
"------- Na lau kama Allah hakuwakinga watu kwa watu, basi hapana shaka zingalivunjwa nyumba za watawa na MAKANISA, na MASINAGOGI, na MISIKITI ambamo ndani yake jina la ALLAH linatajwa kwa wingi". (Qur'an 22:40)

Haya hebu niambie humo ndani ya MASINAGOGI ambamo jina la Allah linatajwa kwa wingi ni watu gani hao hulitaja jina la Allah kwa wingi???, tunawajua watu wanaotumia maKanisa na msiktini ndanimo kutaja jina la Allah.
Sasa hoja yako hapo iko wapi kijana,kuwakinga maana yake ndiyo kuwalipa pepo au ? Jikite kwenye hoja.
 
Aya ya 69 katika sura ya 5, inaongelea ya kuwa endapo hao Mayahudi na Wakristo wakimuaani Allah na yale aliyokuja nayo Mtume na wakafanya mema basi watalipwa pepo. Maana yake hao wanakuwa ni Wafuasi wa mtume sasa yaani Waislamu. Rejea Tafsiri ya Ibn Kathiri.

Aya ya 5:69 inasema:

"Hakika wale walioamini NA Mayahudi NA Masabii NA Wakristo--- atakaye muamini Allah na siku ya mwisho na kufanya vitendo vizuri basi hao hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika".

Hapo yametajwa makundi manne

1-----الزين امنو
2-----الزين هادو
3----اصبءن
4----النصر

1 --- wale walioamini ambao ndio Waisilamu , 2 Mayahudi, 3Masabii 4 Wakristo.

Sasa wewe unataka kudanganya hapa eti wote hao ni kundi namba moja???!!-----labda utamdanganya kipofu asiyejua Qur'an.
 
Sasa hoja yako hapo iko wapi kijana,kuwakinga maana yake ndiyo kuwalipa pepo au ? Jikite kwenye hoja.

Maana yangu ni hii ndugu kwamba Allah anatambua nyumba za ibada za mayahudi ambazo ni Sinagogi ndanimo jina lake linatajwa kwa wingi (katika ibada zao), wewe unapinga kwamba na kusema uyahudi na mayahudi ni makafiri, hiyo ndiyo point yangu.

Aya hii ya Qur'an inasapoti aya hiyo:

Kila ummati tumewajaalia kawaida ya ibada WANAYOISHIKILIA, basi wasikugombeze katika jambo hili; na uite kwa mola wako; bila shaka wewe upo juu ya mwongozo ulio sawa.
22:67 Qur'an.

Unganisha na aya hizi hapa:-

5:69, 2:62.

Msipokuwa waangalifu mtawakurusha watu ambao Allah anawatambua kwa wema wao.

Ni hivi; Uisilamu ndiyo dini pekee iliyokuwa kamili na inayoweza kumuinua mtu kiimani kuliko dini zingine ambazo nyingi kati ya hizo mafundisho yake yameishatiwa mikono lakini juu ya hayo kuna baadhi ya waumini wachache wa dini hizo ni watu wema na hawatendi maovu bali wanamkubali mtume mtukufu Muhammad saw kwamba ni mtume mkweli wa Allah, waumini hao ndio waliotajwa na ALLAH katika aya ya 5:69 na 2:62.

Sasa kama Allah kawataja na kuwakubali wewe nani ujitie ulingoni kuwakufurisha???--- hicho kibri.
 
Aya ya 5:69 inasema:

"Hakika wale walioamini NA Mayahudi NA Masabii NA Wakristo--- atakaye muamini Allah na siku ya mwisho na kufanya vitendo vizuri basi hao hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika".

Hapo yametajwa makundi manne

1-----الزين امنو
2-----الزين هادو
3----اصبءن
4----النصر

1 --- wale walioamini ambao ndio Waisilamu , 2 Mayahudi, 3Masabii 4 Wakristo.

Sasa wewe unataka kudanganya hapa eti wote hao ni kundi namba moja???!!-----labda utamdanganya kipofu asiyejua Qur'an.
Hivi ushawahi kusoma tafsiri yoyote ya Wur'aan ?

Aya iko wazi maana yake hapi aya inaonyesha ya kuwa Uyahudi na Ukristo ni kufru na ushirikina mpaka pale walio itwa Wakristo wafate mwenendo wa mtume,yaani wamuamini Allah na kuamini siku ya mwisho na kutenda wema,maana yake hapo hawawi tena Wayahudi wala Wakristo ndiyo maana watalipwa pepo. Sasa wangekuwa wapo katika usahihi hizo "na" zisingekuwepo.

Bado nasubiri ushahidi unaonyesha ya kuwa Uyahudi na Ukristo si ukafiri.

Kisha hujaniambia maana ya Ukafiri na maana ya Ushirikina.
 
Maana yangu ni hii ndugu kwamba Allah anatambua nyumba za ibada za mayahudi ambazo ni Sinagogi ndanimo jina lake linatajwa kwa wingi (katika ibada zao), wewe unapinga kwamba na kusema uyahudi na mayahudi ni makafiri, hiyo ndiyo point yangu.

Aya hii ya Qur'an inasapoti aya hiyo:

Kila ummati tumewajaalia kawaida ya ibada WANAYOISHIKILIA, basi wasikugombeze katika jambo hili; na uite kwa mola wako; bila shaka wewe upo juu ya mwongozo ulio sawa.
22:67 Qur'an.

Unganisha na aya hizi hapa:-

5:69, 2:62.

Msipokuwa waangalifu mtawakurusha watu ambao Allah anawatambua kwa wema wao.

Ni hivi; Uisilamu ndiyo dini pekee iliyokuwa kamili na inayoweza kumuinua mtu kiimani kuliko dini zingine ambazo nyingi kati ya hizo mafundisho yake yameishatiwa mikono lakini juu ya hayo kuna baadhi ya waumini wachache wa dini hizo ni watu wema na hawatendi maovu bali wanamkubali mtume mtukufu Muhammad saw kwamba ni mtume mkweli wa Allah, waumini hao ndio waliotajwa na ALLAH katika aya ya 5:69 na 2:62.

Sasa kama Allah kawataja na kuwakubali wewe nani ujitie ulingoni kuwakufurisha???--- hicho kibri.
Nasubiri majibu ya maswali niliyo kuuliza,usirudie maneno yale yale pasi na ushahidi.
 
Waafrika ni wajinga na ni brain washed. Wanaacha dini za mababu zao wanafata dini za watu wengine
 
Kasome Biblia

Kuna wakati Mungu anawatuma Waisrael waende kuua maadui wanaomdharau na kutaka kulitesa Taifa lake kuanzia,

Watoto
Wake
Waume
Wazee
Vibibi
Mbuz
Kuku
Bata
Kondoo
Kila kituuu yaan wauwe kila kitu.

Mungu mwenyewe aliua wazawa wakwanza wakila familia ya wamisiri. Akaua Mtoto wa farao.

Kwa ufupi, Mungu aliyekuumba, anayohaki ya kukufanya anavyotaka
Yanii Mwenyezimungu anauwa?...hivi ni kiswahili tunapishana au ufahamu wako mdogo wa kidini?
 
Hivi ushawahi kusoma tafsiri yoyote ya Wur'aan ?

Aya iko wazi maana yake hapi aya inaonyesha ya kuwa Uyahudi na Ukristo ni kufru na ushirikina mpaka pale walio itwa Wakristo wafate mwenendo wa mtume,yaani wamuamini Allah na kuamini siku ya mwisho na kutenda wema,maana yake hapo hawawi tena Wayahudi wala Wakristo ndiyo maana watalipwa pepo. Sasa wangekuwa wapo katika usahihi hizo "na" zisingekuwepo.

Bado nasubiri ushahidi unaonyesha ya kuwa Uyahudi na Ukristo si ukafiri.

Kisha hujaniambia maana ya Ukafiri na maana ya Ushirikina.

Eti unauliza kama nimeshasoma tafsiri yoyote ya Qur'an tukufu!!!?--- kwani hizo tafsiri zimetoka kwa mtume (saw) ??!!.

Qur'an inajitafsiri yenyewe, hebu angalia hizi aya:-

1----- Kila ummati tumewajalia kawaida ya ibada wanayoishikilia basi wasikugombeze katika jambo hili na uite kwa mola wako bila shaka wewe upo juu ya muongozo. (22:67) Qur'an .

2----Hakika walioamini na mayahudi na masabii na wakristo waliomuamini Allah na siku ya mwisho na WAKATENDA MEMA basi hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
(5:69) Qur'an

3"------ basi hapana shaka zingalivyunjwa nyumba za watawa na MAKANISA na MASINAGOGI na MISIKITI ambamo ndani yake jina la ALLAH linatajwa kwa WINGI.
(22:69) Qur'an .

Hizo aya tatu zinaonyesha kuwa UYAHUDI SIO UKAFIRI lakini hazijasema kwamba Mayahudi hawawezi kuwa makafiri, tofautisha kati ya UYAHUDI na MAYAHUDI.

Sasa wewe onyesha aya inayosema UYAHUDI NI UKAFIRI.

Aya inayokuchanganya ni hii:-

ان الدين عند الله الاسلام Hakika dini mbele ya Allah ni Uisilamu (3:19).

Kwa uwezo wako mdogo wa ufahamu wewe unaona kwamba hiyo aya anapinga ukweli wa dini zingine, Hiyo inashadidia UKWELI NA UZURI WA UISILAMU DHIDI YA DINI ZINGINE ZILIZOLETWA NA MANABII WALIOPITA, YAANI UISILAMU NI DINI ILIYOKAMILIKA KATIKA NYANJA ZOTE ZA MAISHA YA BINADAMU, Dini zingine hazijakamilika na vitabu vyao vimeishaingizwa mikono na kama atapatika mtu mwema katika dini hizo ALIYEMUAMINI ALLAH na SIKU YA MWISHO na KUTENDA MEMA (5:69) basi hatakuwa na khofu na hatahuzunika, na hii ni pamoja na Waumini (Waisilamu)----- kumbuka yule anayemuamini Allah ni lazima pia atamuamini mtukufu mtume (saw).

Usipokubali jambo hili basi basi utasababisha ikhitilafu katika aya za Qur'an, (aya 5:69 na aya 3:19).

----Unataka kujua maana ya ukafiri na ushirikina----.

Je Kwanza umeelewa tofauti kati ya UYAHUDI na MAYAHUDI ? ??, mbona warukia mada mpya??
 
Uko sahihi lakini umeonyesha hisia za kulichukia Taifa hilo!
Kimsingi kwa sasa katika Agano Jipya siyo Taifa Teule,Taifa Teule ni KANISA LA MUNGU ulimwenguni,(1Petro 2:9-10),(Ufunuo1:6).
Kila aliyemwamini Yesu Kristo na kuokolewa bila kujali ni Myahudi au Myunani au Msukuma,nk anakuwa raia wa TAIFA TEULE (Kanisa) na anakuwa mtoto wa Ibrahimu,(Wagalatia3:27-29)
Hii ni kwa sababu Wayahudi waliukataa Wokovu na Mungu kuwageukia Mataifa,(Matendo 13:46-48) na (Matendo28:26-28)
Hata hivyo kwa sababu ya ahadi za Mungu kwa Mababu zao Ibrahimu,Isaka na Yakobo,(Warumi9:4-5),Mungu hajawaacha,mara baada ya Mlango wa Wokovu kwa Mataifa kufungwa na Kanisa kunyakuliwa watapewa nafasi nyingine ya kumwamini Kristo na kwa atakayeamini sasa atapewa uraia katika Taifa Teule (Kanisa)-Warumi11:25-27
Mwisho,bado Mungu analilinda Taifa hilo,na jicho lake liko kwenye Taifa hilo bila kujali hawamwamini Yesu Kristo,kwa sababu Karama za Mungu hazina majuto! Kwa hiyo ukiligusa unagusa jicho la Mungu,jitihada za Waarabu na Wapalestina kutaka kuwaondoa kwenye ardhi yao waliyopewa mababa zao Ibrahimu,Isaka na Israeli ni haziwezi kuzaa Matunda!
 
Back
Top Bottom