Hujanipa ushahidi wa kuonyesha ya kuwa Uyahudi si ukafiri wala hujanipa ushahidi wa kuonyesha ya kuwa mtume Musa amekuja na Uyahudi.
Soma katika Qur'aan kuanzia surat al Fat'ha mpaka surat an Nas hakuna sehemu ambayo Allah ameutaja Uyahudi na Mayahudi kwa sifa nzuri.
Mimi masheikh wangu hapa wanahusika sababu narejea kwao,wewe kadhalika Gulamu anahusika sababu yeye ndiyo kiongozi wenu.
Niambie Uyahudi ni Dini na inafundisha nini na uniambie nani amekwambia ya kuwa nabii Musa amekuja na dini ya UYAHUDI.
Wewe ndio unayetakiwa kuonyesha kwamba UYAHUDI ni UKAFIRI.
Mimi nimekuonyesha kwamba Kafiri au asiyekuwa kafiri ni Myahudi/Wayahudi na sio Uyahudi, Tofautisha kati ya UYAHUDI na MYAHUDI/MAYAHUDI, Uyahudi ni dini kama ilivyokuwa dini ya Uisilamu au Ukristo au Usabii nk, kama jinsi katika Uisilamu na Ukristo kuna watu wema na wabaya ni hivyohivyo kwenye Uyahudi kuna watu wema na wabaya, katika hali hiyo huwezi kuhukumu UYAHUDI kama dini kwa makosa ya wafuasi wake, -----hili nimeishalieleza hapo mwanzo, yaani mfano huwezi kuhukumu Uisilamu kwa makosa ya kigaidi ya Waisilamu.
Eti unauliza: Uyahudi ni dini inayofundisha nini na nani kasema Nabii Musa (as) alikuja na dini ya Uyahudi??!!----- Halafu maswali kama hayo bado unataka kujiita wewe ni Muisilamu safi mwenye elimu ya dini kupambana na "wenye elimu???
Hujui kwamba Uyahudi uliletwa na nani??!!, kesho utauliza Ukristo nao uliletwa na nani na ulifundisha nini??. Hamna lolote isipokuwa ni midomo myepesi kutusi watu kwa kuwaita "Maqadian" na kuwakufurisha watu wa dini zingine ambazo Allah mwenyewe anakiri baadhi ya wafuasi wao ni watu wema na atawalipa kwa wema wao. Allah mwenyewe anawakiri wafuasi wema wa dini hiyo ya Uyahudi wewe unapinga kwamba dini hizo ni UKAFIRI, sasa kama dini zao ni ukafiri iweje Allah awaahidi malipo siku ya Qiyama???!!, huo wema watakaolipwa nao wamejifunza kupitia mafundisho gani??
"------- Na lau kama Allah hakuwakinga watu kwa watu, basi hapana shaka zingalivunjwa nyumba za watawa na MAKANISA, na MASINAGOGI, na MISIKITI ambamo ndani yake jina la ALLAH linatajwa kwa wingi". (Qur'an 22:40)
Haya hebu niambie humo ndani ya MASINAGOGI ambamo jina la Allah linatajwa kwa wingi ni watu gani hao hulitaja jina la Allah kwa wingi???, tunawajua watu wanaotumia maKanisa na msiktini ndanimo kutaja jina la Allah.