Israel siyo taifa teule

Israel siyo taifa teule

Taifa la asili la Israeli SIYO TAIFA TEULE LA MUNGU kwa sababu zifuatazo:
1. Taifa la Israeli la asili liliacha kuwa taifa teule la Mungu wakati lilipomkataa Masihi, ambaye ni Mwana wa Mungu. Masihi mwenyewe alisema hivi: “Yerusalemu, Yerusalemu, muuaji wa manabii na ambaye huwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwake Tazama! Nyumba yenu mmeachiwa katika hali ya ukiwa.” - Mathayo 23:37,38.

2. Pia “Yesu mwenyewe akamwambia, ‘Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.’”—Yohana 14:6, Union Version. Hivyo hawa wanaoitwa na wengine kuwa wateule walimkana Yesu mpaka wakamuua. Hakuna hata sehemu moja kwenye biblia inayoonesha kama wayahudi walimpenda Yesu au hata kufuata mafundisho yake. Bali tunaona wayahudi waliazimia kumpinga na kuwa wapinzani madhubuti kumuelekea Yesu. Walipinga kila kitu, mpaka wakasema kuwa ana mapepo. Sasa kwa msingi wa maneno hayo ya kwenye Yohana je wanaweza kusadikisha wengine kwamba wayahudi ni taifa teule la Mungu, ilhali hawakuikubali njia ya kuwapeleka kwa Mungu?
 
Back
Top Bottom