Yah naungana na wewe. Hii kiu tuiweke kwenye business then tuanze kujadli facts.Hii yote ni katika kuvutia kundi la wateja waliokuwa nje ya wigo wao; its puely a business strategy na sioni kama kuna siasa zozote hapa.
Mods ningeomba hii ipelekwe kwenye ukumbi wa business forums.
Banks huwa inadesign product zao kutokana na aina ya customers waliopo km ilivyo biashara nyingine. Akili ya kung'an'ania Islamic banking ni ubaguzi hii ni akili ya kijima na imepitwa na wakati. Bank zinahitaji kuongeza share za market yao na ndio maana KCB walikuwa wajanja na wakaanzisha hiyo huduma miaka takribani miwili iliyopita. Na wengine wameona kuna faida na wao wakawa attracted.
Tukiungumzia upande wa katiba. Katiba ipo wazi kabisa juu ya hili. Katiba inaruhusu mtu kuabudu dini yoyote pasi na kuingiliwa ktk imani ikiwa havunji kanuni na taratibu za nchi zilizoweka. Ndio maana ukiachana na Taasisi za fedha, utakuta sekta nyingi za huduma km elimu na afya zipo zinaotolewa na Taasisi za dini na nyingine kufuata misingi ya dini husika.
Kwa hiyo uwepo wa Islamic banking Tanzania unafaida kwa taasisi zenyewe yaani benki na pia kwa taifa maana wale ambao wasingewezeka kuwekeza nchini kwa hofu ya riba sasa wanaweza kuja kuwekeza. Pia ni katika harakati zilezile za kukamilisha utaratibu wa kikatiba wa haki ya kuabudu.