Akiruhusu tu kugawanywa na baadhi ya wilaya hasa za kanda ya ziwa, basi itakuwa chaos. Kuna watu wanataka mikoa yao igawanywe. Morogoro kusini wanataka mkoa wa Kilombero, Ruvuma kaskazini mashariki wanataka mkoa wa Tunduru, Tabora kaskazini wanataka mkoa wa Nzega. Kuna miji midogo inataka kupandishwa hadhi kuwa mamlaka ya mji yenye kuunda halmashauri. Mfano ni Tukuyu mkoani Mbeya, Ngaramtoni mkoani Arusha, Karatu Mkoani Arusha, Mbalizi mkoani Mbeya etc. Kama hatuko tayari kugharamia maeneo mapya ya kiutawala basi tuwe uniform. Sio tunakataza Kaskazini na Nyanda za Juu Kusini lakini tunaruhusu Kanda ya Ziwa. Mimi sioni kama tuko tayari kugharamia maeneo mapya ya utawala. Tuache tuone serikali ya awamu ya 6 itakuwaje.
Lakini pia serikali inatakiwa kufuata ushauri wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Wizara ya fedha, Mamlaka ya mapato na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Sio tunaanzisha tu wilaya au mkoa just kwa maombi ya mabaraza ya madiwani au migogoro. Serikali ifuate ushauri wa kitaalam wa Taasisi zake.