Protector
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 423
- 903
Habari wanaJF,
Nimeona nilete kwenu hii ishu inayoendelea ya Uanzishwaji wa Wilaya mpya ya Kisesa. Kuna wilaya tatu zimeathirika moja kwa moja ambazo ni Ilemela, Magu na Misungwi. Mapendekezo ya makao Makuu ya wilaya yatakuwa Fella ambapo ndo itajengwa station ya SGR.
Ni ukweli usiopingika kuwa wakazi wa Kisesa na Usagara wanasafiri Muda mrefu sana na kwa gharama kufuata huduma katika makao makuu ya wilaya zao.
Kutokana na usemi kwamba kuanzishwa kwa Wilaya hii itasogeza huduma kwa wananchi na kupunguza umbali wa kuzifuata, katika kuwaza kwangu nikaona kama ni kusogeza huduma mbona wakazi wa Ilemela ambao kata zao zimemegwa za Sangabuye, Kayenze na Nyamhongolo watakuwa wamepelekwa mbali zaidi kuliko ilivyo sasa hivi.
Kutoka Kayenze/Sangabuye mpaka Ilemela ni kilomita kama 20 hivi na kutoka Kayenze/Sangabuye mpaka Fella ni km zaidi ya 40 tena barabara inapita palepele makao makuu ya Ilemela.
Kwa nini Kata za Ilemela zisiachwe badala yake wachukue kata kutoka Nyamagana kati ya Buhongwa na Kishiri ziunde Wilaya mpya ziungane na kata za Magu na Misungwi?
Au kama lengo ni kusogeza huduma basi wachukue Kisesa waiongeza Ilemela na wachukue Usagara waiongeze Nyamagana (Jiji).
Haya ni moni yangu binafsi, karibuni kwa hoja.