Is Vodacom, Caspian facilitating mauaji?

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,185
307
Jamani nimeshitusha na habari zilizoko kwenye gazeti la Mwanahalisi la leo kuwa wauaji watarajiwa wa Dr Mwakyembe walisafirishwa na magari ya polisi, Vodacom, Caspian na serikali???

Jamani ina maana Vodacom wanatumiwa kuhujumu usalama wa taifa??? Je JK anasemaje kuhusu tuhuma hizi nzito za waziri wake, je huyu waziri kweli anaweza kufanya kazi yake kwa ufanisi katika mazingira haya ya hofu?

Naomba wasije wakanikong'oli na mimi kwa umbeya huu... lakini wakifanya hivyo Mungu wa Ibrahim ninayemwamini atawaadhibu kwa pigo ambalo hawatalisahau

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika
 
Ni taarifa ya kutisha lakini sidhani kama tutasikia lolote kutoka kwa mkuu wa kaya kwa sababu tuhuma zinawahusu maswahiba wake. Sijawahi kumsikia akitamka neno 'mafisadi' kwa sababu anajua msamiati huo utamgombanisha na rafiki zake.
 
Inavyoonesha jamaa anajitafutia umaarufu tu, sioni sababu ya wauwaji kupanda magari yote hayo< kwenda kwa mganga wa tunguli, wamfate Dodoma.

Hivi huyu jamaa naona ana ma-"hallucination". Wauaji hasa wa maana, mpaka Al Shabab, wafanye yote hayo aliyoyaandika? upuuzi usio niingia akilini.

Anahitaji maombi.
 
Ukishangaa ya Mwakyembe na Polisi utaonyeshwa na Polisi na mtoto wa Mengi kuhusu madawa ya kulevya na jinsi tume ya Said Mwema ilivyokula pozi bila kuueleza umma ukweli! Hii ndiyo Bongoland
 
Mkuu kwani mwisho ni magari mangapi ili mauaji yafanyike? Magari machache ni mangapi? Moja, mbili, tatu, kumi, ishirini? Na kwanini iwe idadi unayofikiria?
 
Inavyoonesha jamaa anajitafutia umaarufu tu, sioni sababu ya wauwaji kupanda magari yote hayo< kwenda kwa mganga wa tunguli, wamfate Dodoma.

Hivi huyu jamaa naona ana ma-"hallucination". Wauaji hasa wa maana, mpaka Al Shabab, wafanye yote hayo aliyoyaandika? upuuzi usio niingia akilini.

Anahitaji maombi.

Kwa nini usitie mashaka juu ya akili yako isiyoona upuuzi mwingi wa serikali hii. Hebu angalia wapangaji wa mipango hiyo. Kuna akili ya kupanga mbinu za maana. CCM hiyo! Hukusikia Meya wa Mwanza kuleta muuaji toka kigoma na baada ya kutenda hayo akakimbilia ziwani? Yes Ziwani! CCM hiyo
 
Jamani nimeshitusha na habari zilizoko kwenye gazeti la Mwanahalisi la leo kuwa wauaji watarajiwa wa Dr Mwakyembe walisafirishwa na magari ya polisi, Vodacom, Caspian na serikali???

Jamani ina maana Vodacom wanatumiwa kuhujumu usalama wa taifa??? Je JK anasemaje kuhusu tuhuma hizi nzito za waziri wake, je huyu waziri kweli anaweza kufanya kazi yake kwa ufanisi katika mazingira haya ya hofu?

Naomba wasije wakanikong'oli na mimi kwa umbeya huu... lakini wakifanya hivyo Mungu wa Ibrahim ninayemwamini atawaadhibu kwa pigo ambalo hawatalisahau

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika

Anaogopa kivuli chake.
Pole sana
 
Ukishangaa ya Mwakyembe na Polisi utaonyeshwa na Polisi na mtoto wa Mengi kuhusu madawa ya kulevya na jinsi tume ya Said Mwema ilivyokula pozi bila kuueleza umma ukweli! Hii ndiyo Bongoland

Tanzania kila kitu kinawezekana. Tuhuma kama hizi (ya madawa ya kulevya ya mtoto wa Mengi na ya mauaji ya Mwakyembe) ni tuhuma nzito, kama polisi kweli wanafanya uchunguzi wanatakiwa kuujulisha umma, kukaa kimya maana yake ni kwamba ama polisi wamepuuza au wamedharau na hii ikiwa ni precedence basi twahwelela!
 
Sio kuwa huyu jamaa anahitaji umaarufu. Kuna hali fulani hapa Tz sasa inafanya nijue kuwa tumevamiwa na viongozi wanaopenda kula damu za wengine
 
Msemo "Lisemwalo lipo na kama halipo linakuja" unaweza kuthibitika kwani haya mambo ambayo Mwanahalisi wameibua sio ya mchezo. Watanzania wenzangu ninahisi umafia umeingia humu nchini. Angalia yule Profesa alieuwawa nyumbani kwake misezi michache iliopita - ingawa uchunguzi haujawekwa wazi yeye alikuwa ni mahiri katika kesi za Rwanda wakamtumia watu wakamwua. Iweje leo mambo mazito yaliokwishafanyika hapa TZ yanayowagusa mafisadi moja kwa moja wayaache? Sitashangaa hayo yasemwayo kutokea. Mungu atusuru na watu wabaya hawa.
 
Inavyoonesha jamaa anajitafutia umaarufu tu, sioni sababu ya wauwaji kupanda magari yote hayo< kwenda kwa mganga wa tunguli, wamfate Dodoma.

Hivi huyu jamaa naona ana ma-"hallucination". Wauaji hasa wa maana, mpaka Al Shabab, wafanye yote hayo aliyoyaandika? upuuzi usio niingia akilini.

Anahitaji maombi.

Umaarufu alipata siku nyingi sana, yaelekea hujui historia ya Tanzania...

Kama anatafuta umaarufu mbona hawamuondoi basi serikalini
 
Kampuni zilizotajwa ni za mtu ambaye watanzania wote wanajua kuwa ni fisadi isipokuwa mkuu wa kaya, Nashawishika kuamini maneno ya N/waziri kuwa wanataka kujisafishia njia kwa ajili ya 2015 ili wasiwe na wapinzani.
 
Tangu nilivyojua vodacom na RA ndio wale wale, ka-line kao nikakatupilia mbali.
 
MTEMI KAZWILE USIHOFU hao wa wauaji ........Watakufa kabla ya kuua wengine....!

Nashukuru kwa kunitia nguvu, tawala dhalimu (hii ya kwetu inaonyesha kila dalili ya tawala za namna hii kwa kutowawajibisha wakosaji na badala yake inawasakama wanaopigia kelele juu ya udhalimu unaofanywa) zina historia ya kunyamazisha sauti zinazoipinga au kuwapinga washirika wa watawala.. who knows?
 
Tangu nilivyojua vodacom na RA ndio wale wale, ka-line kao nikakatupilia mbali.

Mkuu tatizo ni kwamba wameshikilia mpini.. ukitaka kumtumia ndugu yako mpunga kiasi akiwa kijijini lazima uwaone (M-PESA), Tigo sijui ni akina nani lakini uwezekana wa kuwa wanafanana kwa matendo ni mkubwa
 
Ni taarifa ya kutisha lakini sidhani kama tutasikia lolote kutoka kwa mkuu wa kaya kwa sababu tuhuma zinawahusu maswahiba wake. Sijawahi kumsikia akitamka neno 'mafisadi' kwa sababu anajua msamiati huo utamgombanisha na rafiki zake.

Heshima kwako MzeePunch,

Mkuu jeshi letu la polisi lilishaoza siku nyingi ukitaka kuthibitisha soma taarifa ya mauaji ya waandamanaji mjini Arusha.Hawana lolote kazi yao kuwapigia salute mafisadi.

Inavyoonesha jamaa anajitafutia umaarufu tu, sioni sababu ya wauwaji kupanda magari yote hayo< kwenda kwa mganga wa tunguli, wamfate Dodoma.

Hivi huyu jamaa naona ana ma-"hallucination". Wauaji hasa wa maana, mpaka Al Shabab, wafanye yote hayo aliyoyaandika? upuuzi usio niingia akilini.

Anahitaji maombi.

Heshima kwako Majimshindo,

Dr H Mwakyembe alishapata umaarufu siku nyingi tangu enzi akiwa board member NBC na baadaye kamati teule ya kale kaulaji RICHMOND.Vipi kweli wewe upo Tanzania au umetumwa kuchafua hali ya hewa. nenda kwenye jukwaa lako la dini hapa hapakufai.

Ukishangaa ya Mwakyembe na Polisi utaonyeshwa na Polisi na mtoto wa Mengi kuhusu madawa ya kulevya na jinsi tume ya Said Mwema ilivyokula pozi bila kuueleza umma ukweli! Hii ndiyo Bongoland

Haswaa polisi walishajivunjia heshima siku nyingi.

Anaogopa kivuli chake.

Pole sana

Yamkini wewe ndiyo unaogopa kivuli chako.

Mimi nadhani maelezo ya polisi yatatupunguzia mgongano wa hisia

Hakuna kitu kama hicho sasa hivi polisi wanapanga mkakati wa kupindisha hoja na kudanganya wananchi.

Msemo "Lisemwalo lipo na kama halipo linakuja" unaweza kuthibitika kwani haya mambo ambayo Mwanahalisi wameibua sio ya mchezo. Watanzania wenzangu ninahisi umafia umeingia humu nchini. Angalia yule Profesa alieuwawa nyumbani kwake misezi michache iliopita - ingawa uchunguzi haujawekwa wazi yeye alikuwa ni mahiri katika kesi za Rwanda wakamtumia watu wakamwua. Iweje leo mambo mazito yaliokwishafanyika hapa TZ yanayowagusa mafisadi moja kwa moja wayaache? Sitashangaa hayo yasemwayo kutokea. Mungu atusuru na watu wabaya hawa.

Mkuu umafia upo Tanzania siku nyingi unajua tena serekali ya mkwere !!!!!!.

Tangu nilivyojua vodacom na RA ndio wale wale, ka-line kao nikakatupilia mbali.

Mkuu tuko pamoja nilishatupilia mbali kaline ka voda
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom