Kama ilivyo siasa za Tanzania hasa kwenye kambi ya upinzani,huibuka vyama venye nguvu na baada ya muda hupotea.
mimi nilijijengea imani kuwa CDM kuwa si chama cha mpito lakini sasa naona ni walewale tu.
Hii ni kutokana na siasa za undugu na ubaguzi zinazoibuka sasa,viongozi wa CDM wanatuhumiana pia wanapishana kauli,hapa sitapanzungumzia sana ila nieleze wasiwasi wangu mkubwa juu za tuhuma wanazopewa viongozi wa CDM.
1.Tuhuma zinazotolewa na wanachama wanaihama cdm na kueleza madudu yaliyo ndani ya cdm.unaweza kupuunza kwa kusema wanaponda kwasababu wametoka lakini hasha! mbona yanajirudia?.hapa tutafakari tuhuma ya Mke wa Dr Slaa kutuhumiwa kuhujumu chama lakini pia kutengeneza mtandao wa wabunge wa viti maalum anaowataka yeye uchaguzi ujao na kubagua wengine,lakini pia tuhuma za matumizi mabaya ya pesa ndani ya chama,mbaya zaidi mama huyu anatuhumiwa kuamrisha viongozi wa chama Taifa kuhidhinisha malipo kazi ambayo si yake ni ya katibu wa chama Dr Slaa anakwenda mbali zaidi pale anapokua mara kwa mara anadai pesa za mume wake wakati yeye hupo ata kama ni haki yake.HOJA ZOTE HIZI CHAMA HAKIJATOA MAJIBU,ni ishara tosha huu ni ukweli.
2.Tuhuma zinazotolewa na CCM kuwa CDM wanapanga mauwaji ya raia,mbona hawajibu viongozi wa CDM inamaana ni kweli kama ni kweli si kweli kama cdm wamepoteza dira na umaarufu wake sasa unashuka na hatimaye kufa kama ilvyokufa NCCR MAGEZI ya Mrema?.
3.CDM tunajua kilianza kama chama cha kufa na kuzikana cha wachaga,kwangu si shida kwani sasa kimesajiliwa kwa chama cha kisiasa lakini shida hapa ni tuhuma za kuendeleza dhana ya kufa na kuzikina na hapo ndipo utakuta viongozi wake ni wale wale akibadilika wanampa mkwe wao na mtu ambaye si mchaga kama kabwe akionesha niya tayari anaitwa CCM au Usalama, huu ni ushaidi wa tuhuma za kuendeleza dhana ya kufa na kuzikana. na hapa huwa ninamkumbuka sana marehemu CHACHA WANGWE ambaye amekufa kifo cha kutatanisha na cdm hata siku moja sijawai kusikia wakimkumbuka kwa lolote wakati kwangu mimi nilimwona kama mwanaharakati wa kweli.
najua mtatukana sana na kuniita CCM ila nitafurahi mkinita Mtanzania maana mi si mwamini wa vyama ila ni Mtanzania Ambaye si shabiki kama wengi walivyo na ushabiki ambao leo nawatabiria kutafuta chama kingine cha kushabikia maana CDM inakufa.
Ushauri wangu vijana wenye upeo na muona wa dhati wa kusaidia taifa fungueni macho muone kuwa nchi hii ina ombwe la chama cha kisiasa chenye sura halisi ya taifa la Tanzania wa sasa si watanzania wale wa ukoloni.tuungane tuanzishe chama chenye sura ya kitaifa na ambacho katiba yake itakuwa wazi kukemea uwepo wa mabepari ndani ya chama ambao mara zote ndiyo adui wa siasa za Tanzania, ebu chukua mfano cdm wakiamua leo kuwa wanamiliki mahotel wapandishiwe kodi Mbowe atakubali hoja hiyo wakati anajua zile protea,akina aishi hotel, amani beach na wakina Bill hali itakuwa mbaya.TUFUNGUKE WATANZANIA TUACHE USHABIKI.Tutaendelea kuhama vyama mpaka lini? ona sasa cdm hiyo inaporomoka kwa kasi kubwa kisa tu sheji ama ametumwa ama kwa akili zake anatuburuza! Mti wenye matunda ukipigwa mawe sana huku haupuputishi matunda mwisho hufa kwa majeraha ya mawe