Is this the end of CHADEMA?

Is this the end of CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Kama ilivyokuwa kwa NCCR mageuzi baada ya uchaguzi wa 1995 chama kinachojiita cha demokrasia chadema kimekumbwa na migogoro isiyokwisha
Kila kukicha hapa utasikia ngumi zimezuka kona fulani
Mara ooh Saa nane kamuanika Zito
Mara ooh Zito msaliti
Mara ooh Sshibuda anadhamini wasaliti
Mara ooih CCM wanaingiza mapandikizi,
Mara ooh juliana kafanya vilee
Mara ooh sijui nani kafanya vile, yaani imekuwa kero sasa kwani kila siku sasa ukiingia jamii forums au kusoma magazeti hukosi vichwa vya habari vya chadema wakinyoosheana vidole na kutimuana kama kuku bila kufuata katiba wanayodai kuwa ndiyo ya kidemokrasia.
Hiki chama mie nimeanza kukitilia mashaka kuwa kinaweza kuja kuleta maafa kwa nchi yetu kwani wao hawahubiri amani bali wanaeneza machafuko kama vile uamsho tu hakuna tofauti yoyote.
Hebu fikiria suala la gesi watu na akili zao wanashinikiza maandamano gesi ibakli mtwara. haya yangesemwa huko zenji ingekuwa balaa hapa. huu si uchonganishi huu, unaposhinikiza hayo maandamano hujui sie wahehe, wanyakyusa, wakurya, waha, wafipa, wahaya, wachaga nk pia tunahitaji kuona faida ya hiyo gesi.
Uliwahisikia wasukuma wakiandamana kudai mapato ya dhahabu na almasi au minofu yawe kwa ajili ya mwanza tu?
Au uliwahi sikia umeme unaotengenezwa mtera wahehe na wagogo wakasema ubaki iringa na dodoma tu taifa libaki kiza?
What about gesi itakayopatikana lake rukwa? lake tanganyika? selous?
Chadema mie kwa sasa nawafananisha na Kundi la mbwa mwitu waliokosa mawindo kwani wana hasira kali na matokeo yake wamepoteza muelekeo wanaanza kuumana wenyewe kwa wenyewe
1.1276530557.wild-dogs-fighting.jpg

Mara oh Ba.b.a yako kamtimua ma.m.a yako kama ku.ku
 
chilsosi ccm wamekuahidi kukupa tender london ,nazani inabidi utuache sisi chadema tujenge chama chetu wewe dili na tenda uliyopewa na ccm,na ujue hao jamaa watakutumia alafu watakutimua utabaki kama hao fisi kwenye picha....
we dont need you mr lukosi,tuachie tujenge chama chetu
 
- Chadema wamekuwa wakifanya kosa moja kubwa sana na kwa muda mrefu sana, kuzuia challenge from within the party, ambayo kwa maana nyingine ni kuficha ugonjwa sasa wanafichuliwa na maradhi, hawatakufa kama chama hapana isipokuwa wataishia kuwa na vyama viwili baada ya 2015, kwa sababu hawatashinda Urais na watapoteza viti vingi sana vya ubunge,

- Ndani ya Chadema kuna udikteta sana tena wa kutisha sana, nimewasikia mara nyingi sana wale walio ndani ya Chadema wakilalamika kwa siri, na siku zote wana walalamikia Slaa na Mkewe sana, wengi wao wanamuogopa sana Mbowe, so ndani ya Chadema kuna Kundi la Slaa, Mbowe na Zitto, Kundi lenye matatizo makubwa nia la Slaa kwa sababu halipendwi na wengi walio ndani ya Chadema, lakini linakubalika sana na walio nje ya Chadema na hasa wasio wanachama, halafu Chadema inajiumiza sana mara kwa mara inapotegemea sana ideas za hapa JF, makundi ya Zitto na Mbowe hayako mbali sana kiitikadi na yanaweza kuelewana, lakini la Slaa haliwezi kuelewana na yoyote hapa ni lazima kila mmoja awasikilize wao.

- Ujumbe wangu kwa Chadema ni kwamba kama kweli mnataka kusimama na kuwa one thing kabla ya cuhaguzi ujao ni lazima sasa hivi huko kwenu ufanyike uchaguzi wa kihalali tu, ndio kitakachowafikisha 2015 mkiwa na nguvu japo kidogo, otherwise huu mzimu unaowatesa sasa hivi hauondoki soon, na ninaomba kuwakumbusha CCM kwamba sio our interest Chadema kuvunjika sasa hivi kama kuvunjika wavunjike baada ya uchaguzi wa 2015, so ni muhimu sana tukawasaidia wasivunjike.

KIDUMU CCM!!

LE MUTUZ
 
Mkuu nikusahihishe jambo hapo tafadhali
Chadema hakuna uchaguzi wa haki au halali, huo ushauri utakufanya utukanwe hapa,
Hawa jamaa wanaongozwa kidikteta lakini kwa sababu wanawategemea sana wanaowaongoza hawawezi kukemea kitu
Hebu angalia wanavyovunja katiba yao yenyewe, hawa kweli ndio wataweza kuiongoza nchi kwa staili hii?
Wao wakiona chopa limepita hewani tuu basi wameridhika ndio maana kuna kipindi niliwawekea picha ya chopa hapa walinigongea like 1000 within ten minutes hahahah LOL!
 
Kama ilivyokuwa kwa NCCR mageuzi baada ya uchaguzi wa 1995 chama kinachojiita cha demokrasia chadema kimekumbwa na migogoro isiyokwisha
Kila kukicha hapa utasikia ngumi zimezuka kona fulani
Mara ooh Saa nane kamuanika Zito
Mara ooh Zito msaliti
Mara ooh Sshibuda anadhamini wasaliti
Mara ooih CCM wanaingiza mapandikizi,
Mara ooh juliana kafanya vilee
Mara ooh sijui nani kafanya vile, yaani imekuwa kero sasa kwani kila siku sasa ukiingia jamii forums au kusoma magazeti hukosi vichwa vya habari vya chadema wakinyoosheana vidole na kutimuana kama kuku bila kufuata katiba wanayodai kuwa ndiyo ya kidemokrasia.
Hiki chama mie nimeanza kukitilia mashaka kuwa kinaweza kuja kuleta maafa kwa nchi yetu kwani wao hawahubiri amani bali wanaeneza machafuko kama vile uamsho tu hakuna tofauti yoyote.
Hebu fikiria suala la gesi watu na akili zao wanashinikiza maandamano gesi ibakli mtwara. haya yangesemwa huko zenji ingekuwa balaa hapa. huu si uchonganishi huu, unaposhinikiza hayo maandamano hujui sie wahehe, wanyakyusa, wakurya, waha, wafipa, wahaya, wachaga nk pia tunahitaji kuona faida ya hiyo gesi.
Uliwahisikia wasukuma wakiandamana kudai mapato ya dhahabu na almasi au minofu yawe kwa ajili ya mwanza tu?
Au uliwahi sikia umeme unaotengenezwa mtera wahehe na wagogo wakasema ubaki iringa na dodoma tu taifa libaki kiza?
What about gesi itakayopatikana lake rukwa? lake tanganyika? selous?
Chadema mie kwa sasa nawafananisha na Kundi la mbwa mwitu waliokosa mawindo kwani wana hasira kali na matokeo yake wamepoteza muelekeo wanaanza kuumana wenyewe kwa wenyewe
1.1276530557.wild-dogs-fighting.jpg

INawezekana mkuu mawazo yako ni sahii kabisa kwani nakumbuka wakati tunaanza siasa za vyama vingi mwaka 1995 NCCR mageuzi kilikuwa ni chama chenye nguvu sana kiliungwa mkono na kila mtu hasa wasomi Mrema ambaye alikuwa mwenyekiti wa chama hicho alikuwa na mvuto wa aina yake kwa wakati ule na kila mmoja aliamini kuwa mrema alistahili kuwa raisi lakini baada ya uchaguzi na kushindwa kwa NCCR matatizo makubwa ya kiuongozi yakatokea ndani ya chama kile moja ikiwa ni migogoro iliyosababishwa na swala la posho lakini hata mamluki pia walikuwepo ndani ya NCCR na walichangia sana kukiua chama. Laiti kama si migogoro ya kiuongozi yamkini leo hii NCCR ingekuwa imeshashika dola lakini ndio imekuwa hivyo. CDM inapaswa kuwa makini sana na kutambua kuwa CCM isingetamani kuona hata siku moja chama cha upinzani kikashika nchi kwa hiyo itafanya kila njia kuhakikisha vyama vyote imara vinasambaratika. Baada ya uchaguzi 2005 na 2010 CDM imeonekana kuwa chama chenye nguvu na ambacho watu wengi walitarajia labda 2015 kingeweza kuchukua madaraka ya nchi au kingetoa upidhani mkali zaidi kwa CCM kwa kuongeza idadi ya wabunge na madiwani. Ilichotakiwa kufanya CDM baada ya uchaguzi 2010 ni kuzidi kujiimarisha kwa kuongeza wanachama na kufungua matawi mengi ya chama sehemu mbalimbali kuhakikisha kuwa kinafahamika vizuri za katika maeneo ambayo kilikuwa hakitambuliki au hakina wanachama kama tanga, morogoro, njombe, zanzibar na pemba n.k. Kwa kuingia kwenye migogoro ya wenyewe kwa wenyewe ni jambo la hatari zaidi ambalo litafanya wananchi wapoteze imani na chama hiki kwa hiyo kisishangae kikishindwa kufurukuta tena 2015. Inawezekana migogoro hiyo ikawa ni mbinu chafu za CCM kwa kuwa japo CCM iliruhusu mfumo wa vyama vingi lakini haikuwa kwa ridhaa yake na haitamani kuona vyama hivyo vikiwa na afya au vikiwa hai kwa kuwa kustawi kwa upinzani ni hatari kwa CCM.
 
We jamaa uwezo wako wa ufahamu na kuchanganua mambo mdogo sana na ndiyo maana uliamua kujiondoa mwenyewe CDM, Hivi kwa huo mfano wako hapo kwenye RED,
1. Unapozungumzia Dhahabu inachimbwa wapi na akina nani walioajiliwa huko, Ingawa bado serikali ya chama unachokiabudu sasa inachukua 3% ya thamani ya dhahabu inayovunwa.

2. Unapozungumzia Samaki wavuvi ni akina nani na wanaouza ni akina nani?
3. Usiwe na akili finyu watu wa Mtwala wanahitaji mitambo yoye juu ya uzalishaji wa hiyo Gesi ichengwe huko na wao wapate ajira na mapato na mikoa mingine itanufaika kwa gesi hiyo kusafilishwa na kuuzwa huko, hakuna mwananchi wa Mtwala aliyesema gesi ibaki huko na kutumika huko, hizo ni mbinu mnazofanya kupotosha ukweli kwani CCM kwa sababu ni Chama Cha Mapinduzi basi kimezoea kupindua ukweli na kuwa uwongo.[/QU ni kwasababu sijui tu umri wako mana ngekupa la kukutoa mawe humo kichwani kubaki na ubongo, kasome vyema tarifa ya serikali then ujione, watu wa mtwara wanaweza kuwa na madai sahihi ila cyo hayo unayoyasema ww mana ingekuwa hvyo kila mtu angewaunga mkono.
 
chilisosi nimeamini wewe ni msosi(chakula) coz ukishakuwa menu uwezo wa kufikiri unakuwa= 0. Tutafanyaje sasa hamna jinsi tena
 
chilisosi nimeamini wewe ni msosi(chakula) coz ukishakuwa menu uwezo wa kufikiri unakuwa= 0. Tutafanyaje sasa hamna jinsi tena

Polisi waliosambaratisha Chadema mkoani Iringa wadai posho zao
Share bookmark Print Email Rating

Polisi wakiwa wanamshambulia aliyekuwa mwandishi wa Channel 10,Daudi Mwangosi
Na Hakimu Mwafongo, Iringa (email the author)

Posted Jumatatu,Januari7 2013 saa 9:31 AM

Kwa ufupi

“Tulikaa Iringa kwa siku kumi, hivyo kila askari aliyekwenda kwenye operesheni ile, alipaswa kulipwa Sh450,000. Lakini bahati mbaya sana, baada ya kutokea mauaji yale hakuna mtu aliyelipwa mpaka sasa. Vocha zimeendikwa lakini hazijatolewa.”
SHARE THIS STORY
0
inShare

ASKARI walioshiriki katika operesheni ya kusambaratisha mkutano wa Chadema mkoani Iringa na kusababisha kifo cha mwandishi wa habari wa Kituo cha Channel Ten, Daud Mwangosi, wanalalamika kwamba hawajalipwa posho zao zinazofikia Sh12,150,000.

Habari zilizolifikia gazeti hili jana, zilisema kiasi hicho cha fedha kilipaswa kulipwa kwa askari 27 waliotokea mkoani Dodoma kwa malipo ya Sh45,000 kwa siku kwa kila askari. Askari hao walikaa Iringa kwa muda wa siku kumi. Mmoja wa askari hao alisema hadi kufikia jana askari wote waliotoka mkoani Dodoma, walikuwa hawajalipwa posho zao za operesheni hiyo iliyofanyika Septemba mwaka jana. “Kutoka hapa tulienda (Iringa) askari 27, askari wa kawaida 24, masajenti wawili na inspekta mmoja. Wakati tunaondoka tuliambiwa kwamba posho zetu ambazo ni Sh45,000 kwa siku wangetutumia,” alisema askari huyo na kuongeza;

“Tulikaa Iringa kwa siku kumi, hivyo kila askari aliyekwenda kwenye operesheni ile, alipaswa kulipwa Sh450,000. Lakini bahati mbaya sana, baada ya kutokea mauaji yale hakuna mtu aliyelipwa mpaka sasa. Vocha zimeendikwa lakini hazijatolewa.”

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema hana taarifa kuhusu malipo hayo hasa ikizingatiwa kuwa yeye ni mgeni mkoani humo.

“Hapa Dodoma mimi nimekuja siku za hivi karibuni na hilo suala la askari kutolipwa posho zao silijui na sifahamu kama kweli walikwenda huko ulikosema,” alisema Kamanda huyo na kuongeza: “ Naomba nipe muda zaidi nifuatilie ili kujua ukweli wake. Lakini pia nikuombe uwasiliane na mwandishi mwenzako aliyeko hapa Dodoma ili iwe rahisi mie kuwasiliana naye kuliko kuzungumza kwa simu tu.”

Mwangosi aliuawa kwa bomu Septemba 2, mwaka jana wakati polisi hao waliodaiwa pia kutoka Mikoa ya Morogoro na Mbeya, wakiwatawanya wafuasi wa Chadema, waliokuwa kwenye mkutano wa ndani katika Kijiji cha Nyololo mkoani Iringa.
Askari hao walikwenda mkoani Iringa kushirikiana na wenzao katika kudhibiti, mikutano ya Chadema.

Mwangosi aliuawa kwa bomu alipokuwa akiwajibika katika kazi zake za kutafuta habari wakati wa ufunguzi wa matawi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na kufanya mikutano ya ndani ya kuimarisha chama.

Ripoti ya kamati iliyoundwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuchunguza kifo hicho, ilisema Mwangosi aliuawa kwa makusudi na polisi chini ya usimamizi wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda.

CHRIS MKOSI unaikumbuka hiii? MAAKE WE MTAALAM WAKUTUMIA MAKAMASI KUFIKIRI, SASA NAANZA KUKUBALI WE MUUZA POWDER! MAANA HATA MANENO YAKO YA MUUZA POWDER!, NA KALE KATABIA KAKO KA KU....KA NASIKIA KIDOGO KAVUNJE NDOA!!!TEHE!
 
Malecela akoleza moto sakata la gesi
Share bookmark Print Email Rating

Waziri Mkuu Mstaafu na Mwanasiasa Mkongwe nchini, John Malecela
Na Raymond Kaminyoge Dar na Abdallah Bakari, Mtwara (email the author)

Posted Jumatatu,Januari7 2013 saa 8:43 AM
Kwa ufupi
ASEMA LICHA YA KUSTAHILI KUWANUFAISHA WATANZANIA WOTE,UKIWA KARIBU NA WARIDI UNATAKIWA KUNUKIA
SHARE THIS STORY
0
inShare
WAZIRI Mkuu Mstaafu na Mwanasiasa Mkongwe nchini, John Malecela, ametoa wosia kuhusu mgogoro wa gesi akiiomba Serikali kufanya kila iwezalo ili kuhakikisha kuwa wakazi wa Mtwara wananufaika kwanza na rasilimali hiyo.
Malecela alitoa kauli hiyo jana alipotakiwa na gazeti hili kutoa maoni yake kuhusu mgogoro wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam unaoendelea kushika kasi katika siku za hivi karibuni.
"Ukiwa karibu na waridi unatakiwa kunukia waridi. Wakazi wa Mtwara nao wanatakiwa wanukie waridi," alisema.
Malecela alisema, pamoja na ukweli kwamba rasilimali inayopatikana nchini ni kwa ajili ya watanzania wote, ukweli kwamba wakazi wa eneo inakopatikana rasiliamali hiyo wanapaswa kunufaika nayo, haukwepeki.
"Hatutakiwi kuwaacha hivi hivi wana-Mtwara eti kwa sababu hii ni rasilimali ya Watanzania wote. Ni lazima wanufaike zaidi, wao kuliko wengine kwa kuwa wako karibu na waridi," alisema Malecela.
Alisema licha ya gesi hiyo kuwa ya watanzania wote, Serikali inatakiwa kuandaa utaratibu ili kuhakikisha kuwa wananchi wa Mtwara wananufaika zaidi na rasilimali hiyo.
Malecela alieleza kuwa umaskini uliokithiri katika baadhi ya mikoa nchini ukiwamo mkoa wa Mtwara, ndio unaosababisha watu waanze kudai rasilimali zinazotoka katika maeneo yao wakiamini kuwa ndio mwanzo wa ukombozi wao.
"Serikali iyaangalie kwa umakini maeneo yanayotoa utajiri na rasilimali, ni lazima wapewe upendeleo ili wafurahie matunda mali asili yao," alisema Malecela.
Kuhusu gesi kutoka Mtwara
Malecela alisema anaunga mkono gesi kusafirishwa mahali popote palipo na soko kubwa ili iweze kuwanufaisha Watanzania lakini, lazima kuwe na mkakati wa kuwanufaisha pia wakazi wa eneo husika.
"Mnaweza kuisafirisha gesi kwenda mahali popote palipo na soko kubwa, lakini mkaangalia namna mnavyoweza kuwanufaisha wakazi wa Mtwara," alisema na kuendelea;
"Rasilimali inayogundulika popote ndani ya Tanzania ni mali ya watanzania wote, hivyo hata gesi ya Mtwara si ya wakazi wa Mtwara peke yao."
"Kama ilivyo kwa bwawa lililopo katika Jimbo la Mtera linalozalisha umeme na kuingizwa katika gridi ya taifa kwa ajili ya watanzania wote, gesi nayo inatakiwa kuwanufaisha watanzania wote,"
Mkazi Mtwara atishia gesi kutoonekana
Katika hatua nyingine Kikongwe Somoe Issa (90) ambaye ni mkuu wa kaya ya Msimbati, kijiji ambacho gesi asilia inavunwa ameionya Serikali kutoendelea na mpango wake wa kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam na kwamba iwapo itapinga bomba hilo litasafirisha maji badala ya gesi.
Kikongwe huyo ambaye haoni wala kusikia alisema hayupo tayari kuona gesi hiyo ambayo imepatikana katika kijiji hicho ikiondoka mkoani Mtwara.
"Atakayejaribu kuondoa gesi hii kitakachomkuta atakijua yeye mweyewe…ninasema gesi isiende kokote…iwapo atabisha inawezekana akasafirisha maji tu na isiwe gesi yenyewe" alisema bibi huyo kupitia kwa mkalimani wake Asha Hamis
Aliongeza kuwa,"mwaka walioanza kuchimba (2005) walifika hapa bila kubisha hodi, wanajua kilichowakuta…bomba lilikuwa haliendi chini wala kurudi juu…walinifuata hapa nikaenda kufanya tambiko"
Bibi huyo alilazimika kutumia lugha ya kimakonde kwa maelezo ndiyo anayoifahamu vizuri, alisema wakati wa tambiko hilo wazungu waliokuwa katika mradi huo walilazimika kunywa maji kwa kutumia kifuu cha nazi ambapo mmoja wao alikataa.
"Yule aliyekataa niliwaambia aondoke, wale wenzake walimsafirisha na baada ya hapo waliaza kuchimba na gesi ikapatika…leo wanasema gesi inaondoka, hilo sikubali…mimi ndiye mwenye eneo hili, nilifanya tambiko gesi ipatikane na sasa nitafanya tambiko isiondoke" alisisitiza kikongwe huyo ambaye hajui mwaka aliozaliwa.
Kauli ya Kikongwe huyo kupinga gesi kwenda Dar es Salaam na kutishia kusafirishwa kwa maji badala ya gesi iwapo serikali itapuuza madai ya wananchi inarejesha historia ya vita ya Majimaji iliyoasisiwa wilayani Kilwa, mkoani Lindi mwaka 1905-7.
Katika vita hiyo viongozi wa kimila walisema kuwa bunduki za wazungu zitatoa maji badala ya risasi, jambo ambalo lilihamsisha wananchi wengi kupigana vita hivyo.
Kwa kauli hiyo ya mkuu huyo wa kaya anaungana na wakazi wengi wa Mkoa wa Mtwara wanaopinga mradi huo, wakiwemo wanasiasa, viongozi wa dini, mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnain Murji na CCM wilaya ya Mtwara mjini.
Katika salamu zake za mwaka mpya, Rais Kikwete, alisema gesi ni mali ya Watanzania lakini akasema Serikali itahakikisha inaandaa utaratibu kwa wananchi wa Mtwara kunufaika zaidi na gesi hiyo.
Hivi karibuni wananchi wa Mtwara waliandaa maandamano kupinga usafirishaji wa gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
Sakata hilo lilizikidi kuchukua sura mpya baada ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Manispaa ya Mikindani, Mtwara, Ali Chinkawene na Mbunge wa Mtwara Mjini (CCM) Hasnain Murji kumpinga Rais Kikwete wakitaka gesi isisafirishwe kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam.
 
Huyu Babu yuko more in touch na current affairs kuliko we mfano wa binadamu ambae umbo kubwa akili zero! Kazi kudisplay gwanad la Graduation as if you are the only ever graduant, but it is another evidence of how much you are in politics as an attempt to compansate for your failures and unserachievements in the other more prominent areas. As a matter of fact, wewe isingelikuwa kutumia jina la huyu Babu ndani Ufisadini, irrespective of his shortcomings, Ungelikuwa kwenye MI. Hoja muhimu ya Kitaifa ni Issue ya Gesi , siyo upuuzi wenu na huyu muuza Powder!
 
Mkuu nikusahihishe jambo
hapo tafadhali
Chadema hakuna uchaguzi wa haki au halali, huo ushauri utakufanya
utukanwe hapa,
Hawa jamaa wanaongozwa kidikteta lakini kwa sababu wanawategemea sana
wanaowaongoza hawawezi kukemea kitu
Hebu angalia wanavyovunja katiba yao yenyewe, hawa kweli ndio wataweza
kuiongoza nchi kwa staili hii?
Wao wakiona chopa limepita hewani tuu basi wameridhika ndio maana kuna
kipindi niliwawekea picha ya chopa hapa walinigongea like 1000 within
ten minutes hahahah LOL!

Mkuu umenena kama ni mpezi wa likes, andika CDM kuzoa majimbo yote ya DSM, watu watakusapoti bila tafakuri yeyote ndivyo anavyowafanyia Pasco
 
Haya ona sasa,
Kila mtu akiwakosoa katumwa na Zito
Mie ni chilisosi na situmwi, I am my own boss
By the way mie natuma situmwi

Inakuuma nini kuhusu chadema? wewe siyo member! wasiasi wako ni nini? kama wewe ni member acha ushabiki take action. Nina uhakika chama ni imara sana na unajua hilo ndiyo maana unaanza propaganda just to confirm your fear. Nenda kasikitikie CCM.:evil:
 
CDM haifi,we subiri 2015 utaona tu wabunge zaidi ya 100 wanaingia mjengoni,ccm itakuwa ndio chama cha upinzani hyo Dec 2015...
Mkuu, kuna kipindi I was sympathetic to CDM, wana ideas nzuri sana. But they are not a team.
nimeona demokrasia wanayo itaka CCM itumie, wenyewe hawaitumii ndani ya chama chao.
Sipati picha ya Tanzania ikiongozwa the way CDM inavoongozwa sasa hivi... that's me.
Chama cha upinzani ila kina matatizo ya uongozi kuliko hata chama kilicho madarakani!
 
muda unaandika hii post ulikuwa umekula kweli???make hujawaza vizuri kulingana na uhalisia ulivyo wa hari ya kitanzania na maendeleo yake.JIPANGE KWANZA NDO UPOST ONCE AGAIN.
:confused2::confused2::confused2::confused2:
 
Mkuu nikusahihishe jambo hapo tafadhali
Chadema hakuna uchaguzi wa haki au halali, huo ushauri utakufanya utukanwe hapa,
Hawa jamaa wanaongozwa kidikteta lakini kwa sababu wanawategemea sana wanaowaongoza hawawezi kukemea kitu
Hebu angalia wanavyovunja katiba yao yenyewe, hawa kweli ndio wataweza kuiongoza nchi kwa staili hii?
Wao wakiona chopa limepita hewani tuu basi wameridhika ndio maana kuna kipindi niliwawekea picha ya chopa hapa walinigongea like 1000 within ten minutes hahahah LOL!
Ni Kweli tumeshuhudia upo CCM ambapo mwenyekiti anaingiza wajumbe waliopita bila kupingwa kwenye NEC Mkewe-Salma Kikwete,Mwanawe Ridhiwani Kikwete,Mdogoye MOhamed KIkwete,Mwanawe -Halfani Kikwete,Shangazie Tatu Kikwete,Mkwewe Mrs Ridhiwani Kikwete ,mmh unaonaje uchaguzi ulivyo huru na haki huko
Haitoshi anabadili katiba ya CCM akikaa mezani anasema wajumbe wa NEC watatoka wilayani bila kubadili katiba au Kanuni ya CCM unaonaje mmh
 
Mkuu, kuna kipindi I was sympathetic to CDM, wana ideas nzuri sana. But they are not a team.
nimeona demokrasia wanayo itaka CCM itumie, wenyewe hawaitumii ndani ya chama chao.
Sipati picha ya Tanzania ikiongozwa the way CDM inavoongozwa sasa hivi... that's me.
Chama cha upinzani ila kina matatizo ya uongozi kuliko hata chama kilicho madarakani!

Ungekuwa una qoute basi unatuambiya lini kikao kipi na uchaguzi upi vinginevyo hii ni conflict of interest unashuhudia uwongo kwa namna ya kujilidhisha
 
Sasa wewe Chilisosi wasi wasi wako ni nini? vita vya panzi si ndio furaha ya kunguru? mimi naona mnahofu jinsi Chadema inavyogundua mbinu zenu chafu mapema ndio maana mnaa wasi wasi na hofu kubwa, mimi nilitegemea ufurahie mnyukano huo ambao wewe unauona upo ingawa kiukweli haupo bali ni masalia tu.

Wewe ni ccm kwa mujibu wa maelezo yako, jaribu kuimarisha chama chako ili mpate wagombea bila rushwa hapo 2015. maana hata ndugu yetu Sumaye amethibitisha rushwa hutembea kipande hiyo ili mtu uweze kuchaguliwa kuwa kiongozi.
 
Chris ulijidhalilisha na sababu zako za kurudi CCM eti Tanzania kumeendelea. Watu walio UK wanajua unafiki wako na kupenda sifa kwako. Nani hajui ulirudi CCM eti upate hiyo tenda ya kuchagua magari. Kama kuna wanafiki wewe ni nambari One. Ya Chadema hayakuusu tena jaribu kutafuta mada zingine.

Kaka achana na "WASAKA TONGE"
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom