OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,206
- 103,769
Kamusi ya TUKI imetafsiri maana ya neno Civilization. Imetafsiri kuwa ni ustaarabu; hali bora ya kuishi, Hali ya kuwa mstaarabu na kuheshimiana
Mimi ni mmoja kati ya watu wanaomini serikali hii inaongozwa mtu mwenye mapenzi na hofu ya Mungu na mwenye roho ya upendo kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa. Kiongozi na viongozi ni watu wastaarabu. Lakini nimeanza kuingiwa na mashaka ya kushindwa kujua kama tutafika salama, Nitatoa mfano kwa machache
1. Kujivuna ushindi wa kumpiga adui aliyefungwa miguu na mikono
Hili linatudhalilisha sana sio ndani tu bali hata nje ya nchi. Viongozi wa CCM wamekuwa wakijitapa huku na kule kufanikiwa kuiangamaiza UKAWA lakini ajabu ni kwamba wakati CCM ikiwa huru kufanya siasa za wazi na vikao vya ndani, wapinzani hususani CHADEMA wanakamatwa hata wanapofanya vikao vya ndani. CHADEMA wamekuwa wapole na kuachana na siasa za majukwani na kubaki na vikao vya ndani, lakini bado hata huko wanafuatwa na kuwekwa ndani. Huu ni ustaarabu gani jamani.
2. Zoezi la ukaguzi wa vyeti wafanyakazi wa umma kufanywa kisiasa
Zoezi la vyeti kwa watumishi ni zoezi lililofanywa kwa mihemko ya kisiasa kama sio kutaka kiki kwa pikipiki. Kitaalam zoezi kama hilo lingefanywa kwa weledi na shirikishi badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kudhalilisha watu wasio husika.
Kiweledi zoezi hili lilitakiwa lifanyike kwa kina na kuwa na mawasiliano ya karibu kati ya kamati na wakurugenzi. Mawasiliano ya ndani kati ya kamati ya wataalam na wakurugenzi ingesaidia sana kupembua kwa umakini wote wasiohusika na kubaki na wale ‘’pure’’ tu, ndipo majina yangekabidhiwa kwa rais na kutolewa kwa umma. Kurudiwa-rudiwa kwa zoezi hili na baadhi ya watu kuingizwa kimakosa ni dhahiri kwamba kulikuwa na siasa nyuma ya kamati ya wataalam. Mmedhalilisha sana watu wasiohusika wakati kulikuwa na namna ya kuepuka yote haya.
3. Matukio ya mauaji Kibiti kuhusishwa na milengo ya kisiasa
Kauli zimetolewa na wakubwa kuanzia Dr.John, PM Majaliwa na waziri Mwigulu kwamba mbona wanaouliwa ni wa chama kimoja tu. Kiukweli mauaji ya Kibiti yanaumiza sana, lakini iweje kauli kama hizi za kutugawa zinatokana na viongozi. Picha gani inataka kuletwa na viongozi. Kauli kama hizi zinatonesha kidonda cha mgawanyiko uliopo kati ya watu wenye ideology tofauti.
4. Kauli za kibabe na kukataza mawazo kinzani.
Hili lihitaji kulizungumzia, lakini jambo nili sio la kistaarabu kabisa na bahati mbaya zaidi hata Rais aliposhauriwa kumfukuza kazi RC Makonda mnajua majibu aliyoyatoa
Nauli tena kwa mara nyingine, Is government of ‘’Awamu ya 5’’ uncivilized?
Naomba majibu

- Nilistajabishwa sana na kauli kupiga marufuku kupinga agizo la rais kuhusu wanafunzi wanaopata mimba. Nchi hii sio ya kidikteta ni ya kidemokrasia. Hata kama rais yupo sahihi lakini ni kweli tumefikia kiwango cha kukatazana kutoa mawazo tofauti na rais?
- Ile kauli baada ya Lowasa kutaka mashehe wa Zanzibar wapelekwe mahakamani. Kwamba polisi wasiangalie sura wala mwendo wa mtu ''mchochezi''........Mwendo??Mwendo wa Lowasa unaosababishwa na maradhi??!!!!
- Ile kauli ya rais kuwakaripia wabunge waliomtembelea Kamanda Lema akiwa gerezani ni wasaliti, haitatuacha salama
- Matusi makubwa makubwa aliyotukana Rais Mstaafu Mkapa wakati wa kampeni na ambayo hata juzi ameendelea kutukana watanzania wenye mawazo tofauti kwamba ni Wapumbavu na Malofa