Is the Fifth Phase Government uncivilized? | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is the Fifth Phase Government uncivilized?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OKW BOBAN SUNZU, Jul 16, 2017.

 1. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2017
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 23,471
  Likes Received: 19,612
  Trophy Points: 280
  Kamusi ya TUKI imetafsiri maana ya neno Civilization. Imetafsiri kuwa ni ustaarabu; hali bora ya kuishi, Hali ya kuwa mstaarabu na kuheshimiana

  Mimi ni mmoja kati ya watu wanaomini serikali hii inaongozwa mtu mwenye mapenzi na hofu ya Mungu na mwenye roho ya upendo kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa. Kiongozi na viongozi ni watu wastaarabu. Lakini nimeanza kuingiwa na mashaka ya kushindwa kujua kama tutafika salama, Nitatoa mfano kwa machache
  1. Kujivuna ushindi wa kumpiga adui aliyefungwa miguu na mikono
  Hili linatudhalilisha sana sio ndani tu bali hata nje ya nchi. Viongozi wa CCM wamekuwa wakijitapa huku na kule kufanikiwa kuiangamaiza UKAWA lakini ajabu ni kwamba wakati CCM ikiwa huru kufanya siasa za wazi na vikao vya ndani, wapinzani hususani CHADEMA wanakamatwa hata wanapofanya vikao vya ndani. CHADEMA wamekuwa wapole na kuachana na siasa za majukwani na kubaki na vikao vya ndani, lakini bado hata huko wanafuatwa na kuwekwa ndani. Huu ni ustaarabu gani jamani.

  2. Zoezi la ukaguzi wa vyeti wafanyakazi wa umma kufanywa kisiasa

  Zoezi la vyeti kwa watumishi ni zoezi lililofanywa kwa mihemko ya kisiasa kama sio kutaka kiki kwa pikipiki. Kitaalam zoezi kama hilo lingefanywa kwa weledi na shirikishi badala ya kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kudhalilisha watu wasio husika.
  Kiweledi zoezi hili lilitakiwa lifanyike kwa kina na kuwa na mawasiliano ya karibu kati ya kamati na wakurugenzi. Mawasiliano ya ndani kati ya kamati ya wataalam na wakurugenzi ingesaidia sana kupembua kwa umakini wote wasiohusika na kubaki na wale ‘’pure’’ tu, ndipo majina yangekabidhiwa kwa rais na kutolewa kwa umma. Kurudiwa-rudiwa kwa zoezi hili na baadhi ya watu kuingizwa kimakosa ni dhahiri kwamba kulikuwa na siasa nyuma ya kamati ya wataalam. Mmedhalilisha sana watu wasiohusika wakati kulikuwa na namna ya kuepuka yote haya.
  3. Matukio ya mauaji Kibiti kuhusishwa na milengo ya kisiasa
  Kauli zimetolewa na wakubwa kuanzia Dr.John, PM Majaliwa na waziri Mwigulu kwamba mbona wanaouliwa ni wa chama kimoja tu. Kiukweli mauaji ya Kibiti yanaumiza sana, lakini iweje kauli kama hizi za kutugawa zinatokana na viongozi. Picha gani inataka kuletwa na viongozi. Kauli kama hizi zinatonesha kidonda cha mgawanyiko uliopo kati ya watu wenye ideology tofauti.
  4. Kauli za kibabe na kukataza mawazo kinzani.
  • Nilistajabishwa sana na kauli kupiga marufuku kupinga agizo la rais kuhusu wanafunzi wanaopata mimba. Nchi hii sio ya kidikteta ni ya kidemokrasia. Hata kama rais yupo sahihi lakini ni kweli tumefikia kiwango cha kukatazana kutoa mawazo tofauti na rais?
  • Ile kauli baada ya Lowasa kutaka mashehe wa Zanzibar wapelekwe mahakamani. Kwamba polisi wasiangalie sura wala mwendo wa mtu ''mchochezi''........Mwendo??Mwendo wa Lowasa unaosababishwa na maradhi??!!!!
  • Ile kauli ya rais kuwakaripia wabunge waliomtembelea Kamanda Lema akiwa gerezani ni wasaliti, haitatuacha salama
  • Matusi makubwa makubwa aliyotukana Rais Mstaafu Mkapa wakati wa kampeni na ambayo hata juzi ameendelea kutukana watanzania wenye mawazo tofauti kwamba ni Wapumbavu na Malofa
  5. Uvamizi wa Kituo cha Habari cha Clouds Media
  Hili lihitaji kulizungumzia, lakini jambo nili sio la kistaarabu kabisa na bahati mbaya zaidi hata Rais aliposhauriwa kumfukuza kazi RC Makonda mnajua majibu aliyoyatoa
  Nauli tena kwa mara nyingine, Is government of ‘’Awamu ya 5’’ uncivilized?
  Naomba majibu
   
 2. Erythrocyte

  Erythrocyte JF-Expert Member

  #21
  Jul 16, 2017
  Joined: Nov 6, 2012
  Messages: 46,836
  Likes Received: 29,206
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha sana !
   
 3. c

  chabusalu JF-Expert Member

  #22
  Jul 16, 2017
  Joined: Apr 29, 2016
  Messages: 6,132
  Likes Received: 3,539
  Trophy Points: 280
  Ni vigumu kuwa na matarajio ya kufika salama penye chuki na visasi!
   
 4. M

  Mama Obama JF-Expert Member

  #23
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 5, 2016
  Messages: 1,550
  Likes Received: 1,027
  Trophy Points: 280
  Rais Magufuli ameingia serikalini na nia nzuri sana. Alitupa hope Watanzania wengi. Amefanya vitendo vya kutetea haki zetu na Mali zetu Wakati MARAIS waliopita walishindwa. Kitu kinachomuangusha bado ana nawazo ya kizamani na ya kishamba ya kutawala na amri na siyo kwa kushauriana. Rais Magufuli hafuati sheria ya katiba ya nchi na sheria za ulimwengu, Tanzania ni nchi ambao ni member ya mashirika mbali mbali duniani, lazima aelewe sheria tulizoahidi haswa za kuchunga haki za binaadamu. Tanzania ni ya Watanzania wote, lazima asikilize maoni ya Watanzania Ndiyo maana tukawa na bunge. Kama atalipuuza bunge kwa kuwa yeye ni Rais basi bunge lifungwe. Yeye kusimama na kusema hawezi kuwaruhusu watoto waliopata ujauzito kuendelea na masomo Wakati bunge limepitisha huo sio ustaarabu, kuweka kid on da chumvi kufumbia macho Viongozi wanaotowa amri ya kuwaweka watu ndani kinyume. Kweli yeye ni `Rais aheshimiwe, lakini heshima hutoka pande zote mbili. Yeye mwenyewe alipokuwa kwenye serikali ya Kikwete vitu vingi vilikuwa vikimuuzi na hata akageuziwa kesi ya samaki ikawa yeye ni mshitakiwa ingawaje alikuwa akitenda haki ya Watanzania je alipenda?

  Na kwa nini anataka kuwaziba Watanzania midomo kutetea haki zao na sheria ambazo Tanzania imepitisha, kama sio ushamba na kutokuwa na ustaarabu ni nini basi? Hii inaonyesha wazi kabisa elimu yake ya kimawazo ni ndogo sana na yakishamba, otherwise he could be the best leader.
   
 5. areafiftyone

  areafiftyone JF-Expert Member

  #24
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 4, 2017
  Messages: 3,178
  Likes Received: 1,850
  Trophy Points: 280
  Tanzania katika nchi za dunia 196 is ranked 186th kwa ujinga wa watu wake.Katika nchi ya watu wa namna hii mama Obama,ungetegemea rais aweje.WaTz ni watu wa ajabu sana.

  Furthermore kwa mahali katika ujinga wetu tulipokuwa tumefika,nadhani tunahitaji Rais wa calibre ya Magufuli,ngoja atunyooshe kidogo.Mambo mengi yanayotokea katika nchi yetu ni out of shear stupidity.
   
 6. M

  Mama Obama JF-Expert Member

  #25
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 5, 2016
  Messages: 1,550
  Likes Received: 1,027
  Trophy Points: 280
  Basi atunyooshe huku anatupa elimu, otherwise na ujinga na kunyooshwa bila ya elimu tutakuwaje?
   
 7. m

  mliberali JF-Expert Member

  #26
  Jul 16, 2017
  Joined: Jul 13, 2012
  Messages: 3,248
  Likes Received: 1,915
  Trophy Points: 280
  mi nilishangaa MTU mwenye PHD kukomalia issue ya vitoto vinavyodanganywa na mibaba yenye mifedha vikabeba ujauzito.
  mi kama raisi na msomi wa PhD ningekuja na Sera ya kuwaprotect wasichana wall katika mazingira hatarishi kwa kuwajengea mabweni nchi nzima. wakae shule na kuwe na ulinzi.

  ngosha mshamba sana
   
 8. realoctopus

  realoctopus JF-Expert Member

  #27
  Jul 16, 2017
  Joined: May 11, 2014
  Messages: 3,152
  Likes Received: 1,845
  Trophy Points: 280
  Imekuuma hiyo
   
 9. N

  Nyamanoro JF-Expert Member

  #28
  Jul 16, 2017
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 599
  Likes Received: 264
  Trophy Points: 80
  Huyo yumo kwenye government inayozungumziwa ndiyo maana ameonyesha dhahiri kuwa naye ni "Uncivilized"
   
 10. areafiftyone

  areafiftyone JF-Expert Member

  #29
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 4, 2017
  Messages: 3,178
  Likes Received: 1,850
  Trophy Points: 280
  Katika kunyooshwa huko huko tunajifunza mama Obama.Unaona kwamba kumbe hili halikupaswa kuwa hivi,linapaswa kuwa hivi.

  Namhurumia Magufuli sana,ana kazi ngumu.Ni vigumu sana kuwaongoza watu ambao hawajui kwamba wana matatizo,lakini pia ambao hata wakionyoshwa matatizo yao, hawa-appreciate kwamba hayo kweli ndio matatizo yao na kwamba yanahitaji ufumbuzi,and day in and day out they continue bending corners.He has real hard time.
   
 11. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #30
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,579
  Trophy Points: 280
  Majibu ni "He is Uncivilised" Na wala hana hofu ya Mungu ana act tu,ila anayo hofu ya mungu maana hata ikawa anaohofu ya upinzani pia.
   
 12. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #31
  Jul 16, 2017
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 26,400
  Likes Received: 17,579
  Trophy Points: 280
  Tatizo JPM mwenyewe haelewi anafanya mini.Kwa maana hana vission wala mission.
   
 13. H

  HEKIMA KWANZA JF-Expert Member

  #32
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 31, 2015
  Messages: 2,471
  Likes Received: 2,897
  Trophy Points: 280
  Usipate shida mkuu, kijana kapewa MB za bure na memo, kazi yake ni kupost tu, wala hajui nini kapost. Tatizo la ukosefu wa ajira ni kubwa sana.
   
 14. Lobapula

  Lobapula JF-Expert Member

  #33
  Jul 16, 2017
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 2,270
  Likes Received: 1,435
  Trophy Points: 280
  wahaya kaombeni msaada tff si mmejazana huko
   
 15. b

  bababikko JF-Expert Member

  #34
  Jul 16, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,135
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280
  Ngosha mshamba sana pamoja na kukaa mjini muda mrefu haijamsaidia
   
 16. Al-Watan

  Al-Watan JF-Expert Member

  #35
  Jul 16, 2017
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,981
  Likes Received: 14,078
  Trophy Points: 280
  Kwa akili zako fupi za one track mimi kuandika hivyo ushaniona Muhaya.

  No wonder unatetea mjinga mwenzako.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #36
  Jul 16, 2017
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 78,670
  Likes Received: 110,435
  Trophy Points: 280
  Serikali za kidhalimu ndivyo zilivyo!
   
 18. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #37
  Jul 16, 2017
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 24,687
  Likes Received: 24,773
  Trophy Points: 280
  Na ushamba katika ulimwengu wa sasa ni tatizo kubwa sana na hasa ikiwa ni kwa kiongozi. Ushamba kisha unampa madaraka mtu? Tegemea matatizo tuu.
   
 19. d

  don xxx JF-Expert Member

  #38
  Jul 16, 2017
  Joined: Aug 14, 2013
  Messages: 1,116
  Likes Received: 898
  Trophy Points: 280
  Umenena vyema
   
 20. b

  bababikko JF-Expert Member

  #39
  Jul 16, 2017
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,135
  Likes Received: 1,238
  Trophy Points: 280
  uncivilized mag fooooooool
   
 21. Auz

  Auz JF-Expert Member

  #40
  Jul 16, 2017
  Joined: Apr 6, 2016
  Messages: 2,976
  Likes Received: 1,854
  Trophy Points: 280
  Usiamini chochote juu ua mwanadamu mwenzako, na hasa mwanasiasa. Kama ni mhofia mungu wake, basi huyo mungu (shetani) ndie anayejua, na ya familia yake hali kadhalika. Ila unayoyaona (kushuhudia) kama ulivyoorodhesha, huo ndio uhalisia wa mambo

  Post sent using JamiiForums mobile app
   
Loading...