Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,244
- 113,628
Unapoona viongozi wa nchi wanatoa kauli kama ‘Rais Samia ameruhusu maandamano’ au ‘Rais Samia ameruhusu vyama vya upinzani vifanye mikutano ya kisiasa’, wewe Mtanzania uliye mwerevu na uliye na ufahamu wa msingi wa elimu ya uraia, unajisikiaje? Unaonaje?
Huoni kwamba, ama tunaongozwa na viongozi wajinga wasio na ufahamu hata ule wa msingi tu wa elimu ya uraia na jinsi ambavyo nchi inapaswa kuongozwa kwa kufuata katiba ya nchi, au, tunaongozwa na viongozi wasiojali kabisa kufuata katiba ya nchi na sheria zingine za nchi?
Lipi ni lipi hapo?
This country is a hot steaming mess!