Is the Fifth Phase Government uncivilized?

Barbarism nilianza kuiongela hapa JF baada ya watu kuingiliwa kwenye shughuli za misiba/mazishi.
 
wewe unayemtetea mwenye akili mwenzako Luwasa mmefika nae wapi zaidi ya kuchafua jukwaa tu Geita
Umekaa kisiasa sana ilhali watu wanajadili mambo ya muhimu... Mara wahaya wakaombe misaada tff et huko ndipo walipojazana na kwani michango iliyotolewa ilipelekwa tff

Apart from ccm , there's nothing exists within your skull than an empty space
 
Katika kunyooshwa huko huko tunajifunza mama Obama.Unaona kwamba kumbe hili halikupaswa kuwa hivi,linapaswa kuwa hivi.

Namhurumia Magufuli sana, kwa kazi ngumu.Ni vigumu sana kuwaongoza watu ambao hawajui kwamba wana matatizo,lakini pia ambao hata wakionyoshwa matatizo yao, hawa-appreciate kwamba hayo kweli ndio matatizo yao na kwamba yanahitaji ufumbuzi,and day in and day out they continue bending corners.He has real hard time.

Rais Magufuli ana kazi ngumu sana nakubaliana na wewe, kwa uchafu mwingi alioukuta. Na kazi anayoifanya imemuletea maadui wengi sana, lakini kazi yake anaifanya kuwa ngumu zaidi kwa yeye mwenyewe kuvunja sheria kwa kuziba watu midomo na kauri zake anazozitowa za ukatiri. Binaadamu yeyote hajakamilika, lazima akikosea akiambiwa asikie maoni ya watu na azungumuze na watu. Anapovunja sheria na kulipinga bunge, bunge linalowawakilisha Watanzania anajiletea chuki kati ya wananchi wanaompenda na yeye, na hii ina inawafurahisha adui zake, na anaifanya kazi yake iwe ngumu sana.

Statement ambazo anazitowa saa nyingine ni za kikatiri, tofauti na mambo aliyojitolea kufanya ya kupigania haki za Watanzania kwa kupigana na mafisadi ikiwa na wavunjaji wa sheria. Bado nina imani kuwa atakaa ajifikikilie ya kuwa Tanzania ni ya Watanzania wote, asifanye vitendo ambavyo vitaonyesha waliotoka walikuwa afadhari kuliko yeye. Mimi najuwa anafanya kazi ngumu, kuliko waliomtangulia, na angeifanya kazi hii huku anaheshimu sheria ya nchi na za ulimwengu, Rais Magufuli angekuwa star wa Viongozi wa Afrika, lakini badala yake sifa zinaanza kushuka na watu wameanza kumuweka kwenye kundi la Viongozi wa Afrika ambao wengi wao wametoka madarakani na sifa za kutumia vibaya madaraka yao kwa wizi wa Mali za wengi Na kwa kuwakandamiza watu wao (dictator), Hii inawavunja moyo Watanzania wengi ambao wameteseka kwa miaka mingi kwa uongozi mbaya na ubinafsi wa Viongozi waliopita, hofu inatuijia ya kurudi kule kule tulikotoka.
Kupigana na ufisadi pekee huku ananyanyasa wananchi kunamuongezea maadui, na hii vita ni vigumu kupigana peke yake anahitaji Watanzania wawe nyuma yake. Kauli anazozitowa haswa kwa watu wa kawaida wakipata maafa zinaonyesha hana huruma na watu anaosema
anawapigania.
 
Nadhani unataka kutuambia kwamba Rais Magufuli sio civilized, ingawa naona Mkapa naye kaunganishwa.Hata hivyo umeshindwa ku-connect vizuri mawazo yako, ili hatimaye uweze kupata mtiririko mzuri.Kwa jinsi hiyo bandiko lako lingeweza kueleweka vizuri zaidi.

Kwa sehemu nakubaliana na wewe kwamba Mkapa sio civilized,hasa ukizingatia matamshi yake dhidi ya Watanzania kwa ujumla wetu, ambayo yamekuwa na utata mwingi.Hata hivyo sikubaliani na wewe kuhusu Rais Magufuli.Frankly he does not deserve to be called uncivilized. Sioni baya mno alilolifanya mpaka aonekane kwamba ni uncivilized.

At most he should be praised for his efforts.Mengi anayofanya ni mazuri, na yana lengo la kuhakisha kwamba tunafika salama, tofauti na wewe unavyodhani, hata kama kwa sasa hili haliko wazi,labda kwa sababu ya agenda zetu za siri au ufahamu wako mdogo.To me, hizi ni juhudi za makusudi za kumkatisha tamaa Rais.
Mkulu wa kaya kiukweli ana kaulimbukeni na hilo halipingiki. Kuna mambo anafanya vizuri au anaonyesha dhamira ya dhati kuyafanya vizuri. Ila kuna mambo ambayo mengine sio ya muhimu sana lakini anayatolea mapovu kwelikweli, kwa mfano suala la kuzuia mikutano ya vyama pinzani halikuwa na umuhimu wowote bali ni ushamba, ubabe na kupenda sifa. Ukiwa kiongozi na ukawa unavunja katiba huwezi kueleweka kwa watu wenye akili zao timamu, pia kutelekeza mchakato wa katiba mpya kunatia shaka sana kama kweli ana dhamira ya dhati na hili halihitaji itikadi za kisiasa hata kwa mimi wa chama chake.
 
Kitu kinachomufethesha Rais Magufuli ni ushamba, kisomo pekee hakitoshi. Rais Magufuli anatakiwa ajichanganye na Viongozi wengine pia kabula ya uongozi wake angesafiri nchi mbali mbali na kujifunza ustaarabu na sheria za dunia. Hii ndiyo maana wanafunzi wa nchi za Ulaya wakimaliza masomo yao ya vyuo vikuu wanasafiri (back packers) kujifunza kwa kuiona dunia na nazingara yake. Hawasafiri kifahari kama vile alivyokuwa akisafiri Rais wetu Kikwet, wanasafiri kimasikini, na hata wanaishi na wenyji na kukaa kwenye vi hotels vidovidogo, hata siku moja wakiwa wakubwa wa nchi wanaijuwa vizuri dunia na mazingara yake. Rais wetu hayuko exposed, hajui sheria, kauri yake ndiyo sheria anasahau kabisa nchi hii ina Katiba, , ingawaje nia yake nzuri. Maamuzi yake anayofanya yanamuharibia jina, na anaonekana hana tofauti ya mtu asiyesoma. Uamuzi wake wa vyeti, uamuzi wake wa watoto wadogo wanaopata mimba kuwanyima kuendelea na elimu Wakati bunge limepitisha na kadharika, vinaonyesha ya kuwa elimu yake ya nawazo ni ndogo na Hanoi mbali.

Wananchi wamemunga mkono kwa juhudi zake za kupigana na wezi wa Mali zetu, lakini uamuzi wake mwingine unaletwa chuki, sio tu kwa Watanzania na kwa jamii ulimwenguni. Ukiwashambulia watoto na wakinamama , umewashambulia watoto na wakiwa mama duniani kote. Na kwa kuwa Watanzania tuna Uwoga wa kijinga, hata walio karibu naye wanaogopa kumwambia ingawaje vitendo vyake vinauzi, ni kama yeye alipokuwa kwenye serikali ya nne mambo mengi yalikuwa yakimuuzi sana lakini hakudhubutu kufunguwa mudomo mpaka aliposhika madaraka. Lazima serikali ikubali kuambiwa, na sio ikiambiwa ukweli, iweke watu ndani kinyume cha sheria. Tanzania siyo ya mtu binafsi ni yetu wote.
Mkuu mbona unaandika kwa typing errors nyingi kiasi hicho, yaani mpaka mtu anaishiwa hamu ya kusoma, kwa nini usiandike taratibu then ukapitia ulichoandika kabla ya kupost? Tuwe makini kwa kweli sio uandishi wa mtu aliye makini hata kidogo makosa mia kidogo.
 
Elimu yangu mbovu niliyoipata Tanzania. Samahani. Ni wapi hujaelewa niifafanishe?
 
Elimu yangu mbovu niliyoipata Tanzania. Samahani. Ni wapi hujaelewa niifafanishe?
Mkuu sikumaanisha elimu bali makosa ya kiuandishi yanayoepukika, sorry kama nimekukwaza ila nimehisi wewe si mbongo kwa kuzaliwa. Hilo neno niifafanishe sio common hapa bongo, ila lengo langu lilikuwa kuepusha hizo typing errors na si vinginevyo.
 
Mkulu wa kaya kiukweli ana kaulimbukeni na hilo halipingiki. Kuna mambo anafanya vizuri au anaonyesha dhamira ya dhati kuyafanya vizuri. Ila kuna mambo ambayo mengine sio ya muhimu sana lakini anayatolea mapovu kwelikweli, kwa mfano suala la kuzuia mikutano ya vyama pinzani halikuwa na umuhimu wowote bali ni ushamba, ubabe na kupenda sifa. Ukiwa kiongozi na ukawa unavunja katiba huwezi kueleweka kwa watu wenye akili zao timamu, pia kutelekeza mchakato wa katiba mpya kunatia shaka sana kama kweli ana dhamira ya dhati na hili halihitaji itikadi za kisiasa hata kwa mimi wa chama chake.
Mkuu tuko pamoja,ila wakati mwingine watu wa vyama vya upinzani wana udhi.Watu hawa hata pale ambapo hawapashwi kupinga wanapinga tu,for the sake of it,ili wa-justify their precense,bila kujua kwamba wanajidhalilisha kwa wananchi.Tabia za namna hii ni za kitoto sana.Mkuu Rais Magufuli sio malaika, kwa hiyo wakati mwingine atakosea katika maamuzi yake in trying to contain this childish behaviour of the oposition.To me overall he is doing fine,na kama ningeambiwa nimfanyie assessment, ningempa 75%.Jamani tuchukuliane nae,after all he is not a politician.Kwa tabia za Watanzania zilivyo, we need a President of the calibre of Magufuli.Ngoja atunyooshe kwanza tulizidi.
 
Mkuu sikumaanisha elimu bali makosa ya kiuandishi yanayoepukika, sorry kama nimekukwaza ila nimehisi wewe si mbongo kwa kuzaliwa. Hilo neno niifafanishe sio common hapa bongo, ila lengo langu lilikuwa kuepusha hizo typing errors na si vinginevyo.

Bila ya samahani, kuelezana ukweli ndiyo maendeleo. kiswahili bado hakiko chote kwenye mitandao, Wakati mwingine unaandika kitu sentence na inajibadilisha. .. Nifafanishe , nilikuwa na maana nifafanue. Hata hivyo Kiswahili changu sio kizuri sana, unajuwa tena watu wa Usambilo, sijui kama unapafahamu.
 
Nadhani unataka kutuambia kwamba Rais Magufuli sio civilized, ingawa naona Mkapa naye kaunganishwa.Hata hivyo umeshindwa ku-connect vizuri mawazo yako, ili hatimaye uweze kupata mtiririko mzuri.Kwa jinsi hiyo bandiko lako lingeweza kueleweka vizuri zaidi.

Kwa sehemu nakubaliana na wewe kwamba Mkapa sio civilized,hasa ukizingatia matamshi yake dhidi ya Watanzania kwa ujumla wetu, ambayo yamekuwa na utata mwingi.Hata hivyo sikubaliani na wewe kuhusu Rais Magufuli.Frankly he does not deserve to be called uncivilized. Sioni baya mno alilolifanya mpaka aonekane kwamba ni uncivilized.

At most he should be praised for his efforts.Mengi anayofanya ni mazuri, na yana lengo la kuhakisha kwamba tunafika salama, tofauti na wewe unavyodhani, hata kama kwa sasa hili haliko wazi,labda kwa sababu ya agenda zetu za siri au ufahamu wako mdogo.To me, hizi ni juhudi za makusudi za kumkatisha tamaa Rais.
Ame piga bann upande wa pili, hilo ni tatizo namba moja.
 
Ame piga bann upande wa pili, hilo ni tatizo namba moja.
Sawa amepiga ban mkuu,lakini nimeendelea kusisitiza kwamba upinzani hawana sababu za msingi kwa sasa ya kufanya mikutano kwa kuwa hawaongozi nchi.Upinzani wafanye mikutano kwa sababu gani na ili iweje?CCM wanafanya mikutano kwa kuwa ndio wanao ongoza nchi na wanafanya mikutano ili kutoa maelekezo ya kiutendaji,kuonyesha dira,na kuhamasisha wananchi katika shuhuli za maendeleo.Upinzani hawana sababu hizi.Sana sana wakiruhusiwa kwa jinsi tunavyowajua wataanza criticisms zao ambazo sio constructive,ku-discourage wananchi kushiriki kwenye maendeleo,kuidhalilisha institution ya Urais na matamshi mengine tata yenye nia ovu,badala ya wote kushirikiana kuijenga nchi.

Upinzani wanadai kwamba katiba imeruhusu kila chama kufanya mikutano,ni sawa.Hata hivyo katiba haijasema mikutano hiyo ifanywe lini.Wapinzani waelewe kwamba serikali haijakataza vyama kufanya mikatano,serikali inachosema ni kwamba mikutano hiyo kwa vyama ambavyo haviongozi dola ifanywe wakati muafaka,wakati wa campaign.Lazima tukumbuke kwamba campaign zimeisha na sasa ni wakati wa kufanya kazi.Hawa wasubiri 2020 wakati wa campaign au watakapo pata nafasi ya kuingia Ikulu.
 
Irejee sheria ya vyama vya siasa, alafu ruzuku ni za kazi gani?
 
Irejee sheria ya vyama vya siasa, alafu ruzuku ni za kazi gani?
Ruzuku ni kwa ajili ya mambo yafuatayo:-
1.Shuhuli za chama,ziko nyingi.Shuhuli sio mikutano tu.
2.Mikutano ya campaign katika wakati muafaka.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom