Is Lowassa still relevant? - I would say "No" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Is Lowassa still relevant? - I would say "No"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Nov 22, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Nov 22, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Naweza kupendekeza kuwa Lowassa alikuwa na nafasi ya kujijenga upya baada ya kujiuzulu katika kashfa ya Richmond. Wakati ule alipojiuzulu alikuwa bado na umaarufu wa aina yake na umaarufu ambao ulilazimisha watu kugawanyika pande mbili kumhusu yeye. Nakumbuka walikuwepo watu ambao waliamini kabisa kuwa ni Lowassa aliyemjenga Kikwete na kuwa ni yeye kweli aliyekuwa mashine ya serikali. Maamuzi mbalimbali ambayo yalichukuliwa na serikali kati ya 2006 na 2008 yalimhusisha sana Lowassa kiasi kwamba haikuwa haki kumpa pongezi Kikwete bila kumpa pongezi waziri wake mkuu.

  Anguko lake lilikuja kwenye suala la Richmond kama wengi tunavyojua. Nimerudi kuangalia mara kwa mara maelezo yake kwenye mahojiano yake na TVT (yanapatikana kwenye mwanakijiji's Channel - YouTube) na kumsikiliza zaidi ya mara hamsini sasa. Jinsi alivyolishughulikia suala lile hata kama ilikuwa ni kwa nia nzuri kiasi gani isingeweza kukubalika kwani alijipa madaraka ambayo hakuwa nayo. Na zaidi ni uamuzi wake wa kujiuzulu (kuzira) Uwaziri Mkuu kwa mtindo alioufanya ambao kwa kweli wengine japo tulitarajia lakini tulitarajia uwe ni kujiuzulu kwa kuwajibika siyo kwa kuzira.

  Sasa kuanzia wakati ule wa kujiuzulu naamini umekuwa ni wakati wa majuto kwani yumkini amebakia kufikiria mara 1001 jinsi ambavyo angeweza kujitetea pale Bungeni bila kulazimika kujiuzulu. Siwezi kushangaa kuwa kama kuna majuto aliyonayo Lowassa ni jinsi alivyojiuzulu kwa haraka ili kuwapata kile alichokiita "a wish" ambayo wabaya walikuwa wanataka yaani "uwaziri mkuu". Nakumbuka maneno yake kuwa "I'm going to grant it".

  Sasa, aliamua siyo tu kuzira lakini kuzira kabisa na mambo mengine. Ni wazi aliumizwa sana na tukio lile na watu waliokuwa karibu yake nao waliumia pamoja naye. Na wengi wameendelea kuonesha uaminifu kwake. Wamesimama naye na wameenda naye jangwani na hatimaye wamekuwa na matarajio kuwa wanaweza kurudi naye kwenye nchi imiminikayo maziwa na asali.

  Tatizo ni kuwa Lowassa hawezi kurudia utukufu uliokwisha ondolewa. Alikuwa na nafasi ya kuurudia kama angefanya maamuzi sahihi baadaye. Na atakuwa na wakati mgumu zaidi kama atajikuta anachukuliwa hatua yoyote na Chama chake. Usalama wake ni kuweza kuzuia mashambulizi na kurudisha mashambulizi. Lakini endapo atajikuta anapewa "karipio kali" au uamuzi wowote adverse dhidi yake utakuwa ni mwisho wa nyota ya kisiasa ya Lowassa. Sidhani kama atakuwa na nafasi yoyote ya maana nje ya CCM. Isipokuwa kama ataweza kuondoka kweli na wabunge wengine ndani ya CCM ambao wanamtii na hivyo kusababisha a semi-parliamentary election.

  Could Lowassa be a "come back kid"? I don't think so. Could he be a reckoning force? labda ndani ya CCM. Is he relevant for the political future of the country. AN EMPHATIC NO.
   
 2. Dickson Mpemba

  Dickson Mpemba JF-Expert Member

  #2
  Nov 22, 2011
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 330
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Watch him!!!
   
 3. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Katika Tanzania kila kitu kinawezekana mkuu!
   
 4. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Alisahau ule msemo usemao "wewe ukisusa, wenzio twala!"
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Tatizo sio Lowassa kuwa relevant au hapana....
  tatizo ni mfumo wa mizengwe,mbinu,hila na wa kimafia wa CCM
  unaowafanya watanzania wawe na hofu na yeyote wasio mpenda ambae anataka kuwa Rais....

  Tungekuwa na mfumo clean na wa kuaminika wa kuchagua kwanza wagombea kwenye vyama..
  halafu uchaguzi huru na wa haki.....hakuna mtu angekuwa na hofu na Lowassa..
  hata yeye mwenyewe asingejisumbua na siasa tena....

  lakini anajua 'akiweza kufanya mazingaombwe' anaweza jikuta yuko Ikulu....
  na wengi tunajua nchi hii 'mazingaombwe' yapo meengi mno....
   
 6. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  MM, ni wewe ulimsafisha Lowasa baada ya makala ile iliyokuwa inasubiriwa sana ya NIPASHE, watu wakifikiri itammaliza kumbe ilimsafisha. Gazeti lile liliandika ukweli jinsi alivyowashauri akina Msabaha wawe makini katika ufuatiliaji wa mchakato mzima wa Richmond na ninakumbuka aliandika katika moja ya memo zake kwenda kwa Msabaha kwamba "mjiridhishe kwanza" kama Richmond inafaa. Kilichomuuza Lowasa ni ufuatiliaji kwamba kitu kimeishaamuliwa, urasimu wa nini?

  Lowassa anasifa mbili,
  - sio muoga wa maamuzi na anafuatilia maamuzi yake i.e mchapakazi, exactly what TANZANIA needs.
  - mdokoaji.
  Given those two qualifiacations i will vote for him anyday.
  Kwa sababu tunaweza kuzuia udokoaji wake, lakini ni vigumu kupata uchapakazi wake kwa akina Membe, Mwandosya, Mwinyi na wengine wote wanaotajwa tajwa ambao nina uhakika nao ni wala rushwa pia.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  i think EL is fighting this hard just to cover for somethings he did... as for "come back kid".... we are crap when it comes to rational thinking
   
 8. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Kinachoshindikana kwenye real world, kwenye political world kinawezekana!! Kwanza alianza na advrtise ya kwenda Israel kuhiji almost three years ago. Akaja na la mke wake kuandika kitabu (n'shasahau kinahusu nini)....likaja la kuwa Fund Raising Manager wa Makanisa!! kote huko, anaenda ama ku-prove his innocense au kuonesha kwamba "u'll never br free of mistakes while u're still alive" na hivyo kuamua kujutia yote yaliyopita na kuamua kurudi kundini na kujiweka karibu na mungu. Anatoa ujumbe wa kwamba yeye ni kijana mzuri pamoja na yote yaliyomkuta hivyo hakuna sababu ni kwanini asiaminiwe na watanzania!
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Niliuliza huko nyuma who is CHADEMA' sasa nitauliza tena who is 'Lowassa'? Ni huyu mheshimiwa toka Monduli aliyewahi kuwa Waziri mkuu? Kikwete anajua Lowassa sio 'mtu' na ndio maana anabuni dawa za kichinachina ili ku-prolong maisha ya CCM. Kama kweli tatizo la CCM ni mtu anayeitwa Lowassa kwanini washindwe kumdhibiti?
   
 10. BONGE BONGE

  BONGE BONGE JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 3,399
  Likes Received: 1,524
  Trophy Points: 280
  ......mkuu naomba nitofautiane (sijui kama ni kidogo au sana) kuhusu relevance ya huyu jamaa, kwa maoni yangu, Lowassa is not only still relevant but also can deliver; udokozi imekuwa kama ka-utamaduni kakibongo, ndio maana kila kukicha utasikia mchwa wa local govt wakizifanyia kweli asilimia 23 ya trilion 13 (keki ya taifa) ili hali 77% ya hizo trilion zikifanyiwa kweli kule central govt(huku ni kimya kimya hamna kelele), kwa kifupi kautamaduni ka kula kulingana na urefu wa kamba, kamekithiri.... kiongozi aina ya Lowassa(sio lazima yeye) ndiye tunayemhitaji, kiongozi anayeweza kusema kitu kikafanyika, sio balaa la akina Membe, Mwandosya, Mwinyi (kwa maoni yangu) wataendeleza shida za mkuu wa kaya tuliyenaye
   
 11. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Ntachanganua upya then ntarudi! Inanitatiza sana thread hii!
   
 12. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Is there any proof kwamba alijiuzuru kwa "kususa" uwaziri mkuu? so far so good mi namkubali kama mtu mweyne uthubutu,, achilia mbali anaotajwa kuwa nao ambao basically ndo hulka ya wote ccm kama BONGE BONGE alivojaribu kuainisha hapo!
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Naona ameshaanza kukutuma kuwaandaa wafuasi wa chadema kumkaribisha rasmi kwenye chama..

  Mtakula mapishi yenu, just wait n see
   
 14. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Kama watanzania wataendelea kuwa makondoo,basi Lowassa anawafaa.
   
 15. Kitaja

  Kitaja JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 2,665
  Likes Received: 703
  Trophy Points: 280
  Ninasikitikitika sana kuona jinsi baadhi ya watu wanavyoendelea kuamini na kuaminisha watu wengine kuwa EL pekee ndiye atakaemudu nafasi ya ukuu wa kaya kwa mhula ujao.Hayo ni mawazo potofu sana kwa nchi yenye watu zaidi ya milioni 45 kwani naamini na kuna ushahidi wa wazi wa watanzania wengi tu tena waadilifu wanaoweza kumudu nafasi hiyo . kwa ndugu yetu EL akikalia kiti bila ajizi ataanza kulipa kisasi kwa watu anaohisi walihusika kumjeruhi kitu ambacho ni hatari kwa usalama na maendeleo ya nchi.
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Mkuu akisimama EL na akashinda,basi watanzania deserves him,however CCM wakishindwa pia ni vyema,hivyo binafsi naamini EL akisimama,matokeo ya either or kama tutakuwa na katiba mpya basi siyo mbaya.
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu alofanya Lowassa ni maamuzi mazuri sana kuliko kila kitu. Kama angethubutu kukubali kuanikwa bungeni leo hii watu mngemtemea mate na pengine ubunge pia angeupoteza kwa sababu ingefikia kuwa kesi na mshtakiwa mahakamani..

  Ushahidi ulokusanywa ulikuwa mkubwa sana dhidi yake na shukuruni hamkupata kuusikia kwa undani lakini INATISHA....
  Hivyo, mwacheni ale kuku zake kwa wakati akijutia Uroho wa fedha na madaraka huku akiwa na maadui wengi...

  Richmond ni moja ya mikataba mibovu zaidi ya 100 ya Tanzania iloingia lakini kwa nini mkataba huu ndio pekee ulikomaliwa na wanasiasa?... Utajaza.
   
 18. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Mkuu nadhani umesahau kulikuwepo na ripoti mbili hizo za kuhusu RICHMOND, shida ni Mwakyembe mgonjwa.
   
 19. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Well said The Boss

  Uchaguzi wa kupata rais wa Tanzania unaaminika na wengi kwa 99% kuwa una stages kuu tatu, ukizipita hizo wewe ni Rais mteule unasubiri RUBBER STAMP ya GENERAL ELECTION in uapishwe kuwa Rais. Stage hizo ni
  1. Kamati kuu ya CCM (CC): ukiweza kufanikisha kuwashawishi wajumbe ili jina lako lipite kwenda stage ya pili basi hiyo ni development tosha towards presidency.
  2. HALMASHAURI KUU YA CCM. Hawa kazi yao ni kusikiliza na kupigia majina matatu yatakayoweza kupitishwa kwenda stage ya mwisho ya kumpata Rais wa Jamhuri ya muungano wa CCM wa Tanganyika na visiwani. Ukivuka hapa probability ya kuingia ikulu ni 0.33. ni hatua kubwa sana maana iwe isiwe unakuwa umehakikishiwa ulaji wa namna moja ama ingine ili kukupoza kama utatupwa nje. Katika stage hii vitu kama ahadi za vyeo na nani utamlinda ni muhimu sana ili uvuke.
  3. Stage ya mwisho ni MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM. Hapa pia inategemea sana na mtandao ulioujenga mikoani, wajumbe wa mikoa wanakuja na agenda zao na kila mkoa unaangalia masilahi yake, lakini pamoja na hilo inategemea pia uwepo wa short term incentives kama bahasha pia na ahadi ya kuhakikishiwa ulaji wajumbe wenye ushawishi ili kuwapindua mawazo wafuata upepo na posho ambao ni wengi mno. Stage hii ni sawa na uchaguzi mkuu wa rais, hivyo basi ukipitishwa tu kama mgombea wewe ni PRESIDENT ELECT unasubiri PAPER WORK za TUME YA UCHAGUZI Kama CERTIFICATE ili uweze kupata INTERNATIONAL LEGITIMACY.
  Uchaguzi utakaofanyika October ni wa kuwadanganya wananchi kuwa wanachagua rais wao, ukweli ukiwa hilo zoezi zima ni PREDETERMINED Na kila aina ya mbinu itafanywa ku-deceive wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA CCM WA TANGANYIKA NA VISIWANI NDIYO HUYO WA TANZANIA.

  Kwa process hiyo niliyoitaja ni DHAHIRI KUWA LOWASA BADO NI RELEVANT KWENYE SIASA ZA CCM JAPO SI LOLOTE SI CHOCHOTE MBELE YA WATANZANIA KAMA WATAPEWA VETO POWER YA KUKATAA MAAMUZI YA MKUTANO MKUU MAALUM WA CCM.

  Ingekuwa Wananchi ndiyo wenye maamuzi ya mwisho ni dhahiri kuwa domino effect ingeenda mpaka ndani ya CCM kuwa kumchagua Lowassa kama Rais wao ni kuchagua VETO ya wananchi. Hivyo They should compromise with real voters to avoid their VETO Threat.

  MPAKA PALE WANANCHI WATAKAPOSEMA SASA BASI, CCM ITAENDELEA KUTUTIA VIDOLE VYA MACHO NA KUTULISHA VIBUDU KAMA VIONGOZI WETU TULIOWACHAGUA.
   
 20. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,935
  Trophy Points: 280
  Na kwa maana hiyo EL is still very relevant!
   
Loading...