Mkuu MM, ulichokiandika kita-hold water endapo serikali yetu ingekuwa muumini mzuri wa utawala bora.....lakini bahati mbaya sana sivyo ilivyo!!! Kama ujuavyo, serikali ya CCM imejikabidhi yote kwa matajiri ambao sasa wakikohoa tu chama chote kinatikisika. Pengine hii ndio inampa ugumu Kikwete wa kufanya maamuzi magumu ndani ya chama. Kwa sasa chama *cha CCM kinaendeshwa kwa mfumo wa kamari (mfumo wa liwalo na liwe), no objectivity, no integrity, no ethics!!!
Katika mazingira kama haya bado LOWASA ana chances za kucheza karata zake vyema and possibility of*re-bouncing*back still exists!!!
Katika mazingira kama haya bado LOWASA ana chances za kucheza karata zake vyema and possibility of*re-bouncing*back still exists!!!
Naweza kupendekeza kuwa Lowassa alikuwa na nafasi ya kujijenga upya baada ya kujiuzulu katika kashfa ya Richmond. Wakati ule alipojiuzulu alikuwa bado na umaarufu wa aina yake na umaarufu ambao ulilazimisha watu kugawanyika pande mbili kumhusu yeye. Nakumbuka walikuwepo watu ambao waliamini kabisa kuwa ni Lowassa aliyemjenga Kikwete na kuwa ni yeye kweli aliyekuwa mashine ya serikali. Maamuzi mbalimbali ambayo yalichukuliwa na serikali kati ya 2006 na 2008 yalimhusisha sana Lowassa kiasi kwamba haikuwa haki kumpa pongezi Kikwete bila kumpa pongezi waziri wake mkuu.
Anguko lake lilikuja kwenye suala la Richmond kama wengi tunavyojua. Nimerudi kuangalia mara kwa mara maelezo yake kwenye mahojiano yake na TVT (yanapatikana kwenye mwanakijiji's Channel - YouTube) na kumsikiliza zaidi ya mara hamsini sasa. Jinsi alivyolishughulikia suala lile hata kama ilikuwa ni kwa nia nzuri kiasi gani isingeweza kukubalika kwani alijipa madaraka ambayo hakuwa nayo. Na zaidi ni uamuzi wake wa kujiuzulu (kuzira) Uwaziri Mkuu kwa mtindo alioufanya ambao kwa kweli wengine japo tulitarajia lakini tulitarajia uwe ni kujiuzulu kwa kuwajibika siyo kwa kuzira.
Sasa kuanzia wakati ule wa kujiuzulu naamini umekuwa ni wakati wa majuto kwani yumkini amebakia kufikiria mara 1001 jinsi ambavyo angeweza kujitetea pale Bungeni bila kulazimika kujiuzulu. Siwezi kushangaa kuwa kama kuna majuto aliyonayo Lowassa ni jinsi alivyojiuzulu kwa haraka ili kuwapata kile alichokiita "a wish" ambayo wabaya walikuwa wanataka yaani "uwaziri mkuu". Nakumbuka maneno yake kuwa "I'm going to grant it".
Sasa, aliamua siyo tu kuzira lakini kuzira kabisa na mambo mengine. Ni wazi aliumizwa sana na tukio lile na watu waliokuwa karibu yake nao waliumia pamoja naye. Na wengi wameendelea kuonesha uaminifu kwake. Wamesimama naye na wameenda naye jangwani na hatimaye wamekuwa na matarajio kuwa wanaweza kurudi naye kwenye nchi imiminikayo maziwa na asali.
Tatizo ni kuwa Lowassa hawezi kurudia utukufu uliokwisha ondolewa. Alikuwa na nafasi ya kuurudia kama angefanya maamuzi sahihi baadaye. Na atakuwa na wakati mgumu zaidi kama atajikuta anachukuliwa hatua yoyote na Chama chake. Usalama wake ni kuweza kuzuia mashambulizi na kurudisha mashambulizi. Lakini endapo atajikuta anapewa "karipio kali" au uamuzi wowote adverse dhidi yake utakuwa ni mwisho wa nyota ya kisiasa ya Lowassa. Sidhani kama atakuwa na nafasi yoyote ya maana nje ya CCM. Isipokuwa kama ataweza kuondoka kweli na wabunge wengine ndani ya CCM ambao wanamtii na hivyo kusababisha a semi-parliamentary election.
Could Lowassa be a "come back kid"? I don't think so. Could he be a reckoning force? labda ndani ya CCM. Is he relevant for the political future of the country. AN EMPHATIC NO.