Hapana! best disscussion forum in Africa inaweza kuwa Nairand ya wanaigeria! Lakini nina hakika Jamiiforums inaweza kuwa ya pili baaada ya Nairanda...! Uzuri Mimi hizi mbili nazijua vizuri!
Ukiangalia kwenye umakini wa wanachama Nairand wana wanachama wengi makini ukilinganisha na Jf maana ni mara chache ukakuta matusi na utani ambapo hapa husiki!
Muonekano/mpangilio/ wa majukwaa! Katika hili Jamiiforums is the best ukilinganisha na Nairand..
Nairand hawana mpangilio mzuri kabisa wa forums kiasi kwamba unaweza kuchukua muda mrefu kutafuta jukwaa unalo liihitaji kifupi majukwaa yao wame yarundika kama nyanya hivyo mtu mgeni anaweza kupata shida pakuanzia . katika hili nitawawekea picha!
Uzuri wa application kati ya Nairandforum na Jamii forums...na hapa bado Jf inaongoza kwa kuwa application nzuri na yenye mvuto ambayo utafurahia na majukwaa yote lakini katika hili Nairandforum pamoja na kuwa na wametupita kwenye technology still wameshindwa kuipatia Nairandforum application nzuri...application walionayo haina tofauti na mtu kutumia browser kwa hiyo katika kipengele hiki tumewapiga bao!
Upole/Ukali wa moderators! Hakika moderators wa kule ni wakali ukifanya kosa ukapigwa ban hairuhusiwi kufungua id nyingine labda wasikubaini ..lakini hapa Jf tuna moderators wapole na wanao vumilia sana..kule ukifungua thread utakutana na sheria mwanzoni wana sahihisha hadi lugha..kuandika kitoto ni kosa ..ku chit-chat kwenye thread ni kosa ..nafikiri ukali wao ndio unafanya Nairand kuwa the best ukilinganisha na Jf!
Uzalendo kwa nchi yao! Duu hawa wenzetu ni wazalendo sana kwa nchi yao ukilinganisha nasisi hata ukipitia disscussion zao zote wao ni Nigeria kwanza!
Siasa za majitaka kwenye forum! Hawa jamaa pamoja na kuwa na mikwaruzano kati ya wana siasa na wana siasa lakini siasa zao hazijafikia za kwetu kabisa ...sisi huwa tuna dhalilishana sana.ukipitia jukwaa lao la siasa unakutana na mada za siasa za msingi na zenye tija tuu ..pengine ni sababu ya sheria zao kali kwenye forum.
Wanachama wanavyo changamkia thread! Nairand pamoja na kuwa na member wengi sana lakini uchangamkiaji wa thread si mkubwa sana ukilinganisha na Jf ..Jf watu wanajua kushambulia sana thread..na comment zinapanda kwa kasi ukilinganisha na Nairand forums ambapo inategemea ni jukwaa gani labda sports au political..
Fikra za wanachama..kuhusu siasa! Hata kule Nairand kama ilivyo Jf kuna watu wana amini kabisa kuwa kuna watu ni vibaraka wa watu na wanalipwa kuwasifu au kuwatetea watu fulani..
Ubinafsi na utaifa! Kule Nairand wakijua wewe si Mnigeria wanachama wanachukia unapo comment kwenye mambo yanayo ihusu Nigeria....
Urahisi wa kuwasiliana na moderators ! Kule Nairand ni rahisi sana kuwasiliana na moderators maana kila jukwaa kuna sehemu juu ya kuwasiliana na moderator wa jukwaa husika kama una maoni au ushauri..kuna sehemu pa kumuandikia Email kirahisi kabisa..ni tofauti na kitufe cha report abuse..hiki kipo separate..katika hili wametushinda bila shaka
Invisible na timu yake wanaweza lifanyia kazi!
Idadi ya wanachama wanao kuwa hewani or on line...katika hili pamoja na Nairand kuwa na wanachama wengi sana lakini ni wanachama wachache wanaweza kuwa on line kwa wakati mmoja..hata kama kuna issue nyeti wanachama huwa hawazidi 2000 tofauti na Jf japo siku hizi hawaonekani!
Kuhusu Matangazo..hakika kama ni hela mmiliki wa Nairand anapata hela nyingi kupitia matangazo maana wana matangazo mengi hadi.... nafikiri hili linachangiwa na kujitangaza na pia wanaigeria wengi wana uelewa mkubwa wa matumizi ya internet na umuhimu wake hivyo ni rahisi watu kupekeka matangazo wakijua yata wafikia watu wengi...
Mada kuandikwa kwa umakini! Kule wanachama wengi wanajua kuandika mada zao vizuri hawakuachi mwanachama unajiuliza! Wanaandika kwa undani kabisa sio vipisi..ukienda kwenye habari za uchunguzi ndio utapenda kabisa!
Ni kweli tuna Mengi ya kujifunza kutoka Nairand na wao wana ya kujifunza kutoka kwetu hasa mpangilio wa thread na muonekano wa jukwaa sisi tuko bora!
Nairand forums is the best though