Irrigation system maji ya visima virefu yenye chumvi

Silicon Valley

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
1,092
1,116
Naomba kujua changamoto za irrigation system source ya maji ni kisima kirefu 100 mtrs.

Ukimwagilia maji shambani kwa mpira wa kawaida baada ya km mwezi pakikauka panapauka inaiona chumvi chumvi juu ya udongo lakini hayo maji kwa kunywa huisikii kbs chumvi na tunayanywa kama kawaida.

Je, ni nini madhara yake km migomba na parachichi?

Je, unaweza kuimalizaje hiyo changamoto?
 
Hapo bado sijaelewa, yaani hayo maji ukiyanywa hayana chumvi lakini yakikauka unaona chumvi chumvi?

Hebu jaribu kuwaona wataalamu waliangalie hilo eneo huwenda ni ardhi.

Kwa sababu kwa maji ilikuoneka athari yake baada ya kukauka ingebidi chumvi yake iwe Kali sana, sasa iweje uwe uihisi unapoyanywa kunywa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwezi mmoja ni mrefu sana kwenye mmea kufahamu kama kuna madhara ama la,nilifikiri wewe ungeleta ushauri kwani mpaka sasa umefanya kwa vitendo,tueleze umeona nini kwenye mmea baada yakumwagilia maji ya chumvi?
 
Chumvi siyo nzuri kwa mimea ila kwa binadamu nzuri
shukran madam
Mwezi mmoja ni mrefu sana kwenye mmea kufahamu kama kuna madhara ama la,nilifikiri wewe ungeleta ushauri kwani mpaka sasa umefanya kwa vitendo,tueleze umeona nini kwenye mmea baada yakumwagilia maji ya chumvi?
Shukran sana hadi sasa sijaona tofauti yeyote ya direct kwenye mimea ila nimeweza gundua mvua zikianza kunyesha mimea inakua haraka na kuchanua vizuri zaidi kuliko kipindi cha kiangazi natunamwagilia hayo maji,
 
Hapo bado sijaelewa, yaani hayo maji ukiyanywa hayana chumvi lakini yakikauka unaona chumvi chumvi?

Hebu jaribu kuwaona wataalamu waliangalie hilo eneo huwenda ni ardhi.

Kwa sababu kwa maji ilikuoneka athari yake baada ya kukauka ingebidi chumvi yake iwe Kali sana, sasa iweje uwe uihisi unapoyanywa kunywa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah teste ya hayo maji husikii chumvi, na kama ipo (tegemea na mtu) ni kwa mbaali sana ambayo haimzuii mtu kunywa maji km wanavyosema maji ya kilimanjaoro wapo wanaodai yana chumvi

Lakini ukimwagilia kama mwezi na pakakauka unauona unga mweupe km chumvi wazi kabisa nahisi inaweza kuwa ni madini mengine aidha chokaa au mchanganyiko
 
Tunasubiri majibu ya maabara

PH
7.0
Conductivity
1724(2500)
Turbidity
22(25)
Hardness
252(300)
Calcium
181(150)
Magnesium
17(100)
Potassium
NA(50)
Sodium
128(200)
Chloride
200(250)
Flouride
0.5(1.5)
Salphate
331(400)
Nitrate
1.5(45)
 
Chukua hayo maji na ndani ya masaa 6 yawe yamefika chuo cha maji wakupimie. Watakupa madini yote kwenye hayo maji na kama yanafaa kwa kilimo au matumizi ya binadamu
 
Inawezekana vumbi la ardhini au mwamba unaweza kuhisi ni chumvi mkojo na chumvi yake haionekani kamwe ukiimwaga chini zaidi ya madhara na harufu
 
Hata pale Arusha Technical wanayo lab ya maji kwa ajili ya irrigation n.k. watamsaidia vizuri tu. Cha msingi aende akaulizie kwanza bei zao.
Na kama hajui namna ya kufanya sampling pia aombe wamuelekeze ili kupunguza gharama.
 
Ila hiyo chumvi huenda ni ya kwenye maji mkuu. Maana kwenye udongo kuna chumvi, huwa ukimwagilia maji mara nyingi chumvi yake hushuka chini kwenye siol profile yake (tunaita flushing).
So kwa maelezo yake huenda ni chumvi ya kwenye maji. Wewe na wenyeji wengine mnaweza kuona sio chumvi kali sababu miili yenu imezoea maji hayo.
Kwa ufupi, chukua sampuli za maji na udongo peleka lab.
Pia ili kupunguza gharama, kuna watu huwa wanavyo vipimo vidogo sana havihitaji umeme, wanaweza kukuuzia u kufanya hiyo kazi hapo hapo shambani kama unajua utaalam huo. Then ukafanya interpretation ya data zako. Kama hujui, basi tafuta wataalam.
 
Nawashuku sana wote, tayari maji tumeshayapeleka maabara tunasubiri majibu ndani ya siku 10
 
Tunashukuru majibu ya Maabara yanasema Maji ni salama kwa matumizi ya binadamu na kilimo pia
baadae nikipata muda nitayaweka hapa matokeo ya vipimo vyote

Nawashukuru sana wote kwa ushauri wenu, Tuendelee kushirikiana kwa ajili ya maendeleo yetu sote
 
Back
Top Bottom