Iringa: Watoto wawili wafariki nyumba ikiungua moto

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,120
Watoto Rehema Masanga wa miaka 7 na Amos Masanga mwenye miaka 5 wamekutwa wakiwa wamekumbatiana baada kushindwa kujiokoa kutokana na kufungiwa ndani na mama yao.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mafifi, Rabi Mgata amesema chanzo cha moto ni mshumaa ulioshika Godoro na kuunguza nyumba wakati mama wa watoto akidaiwa kwenda kunywa Pombe.

Kamanda wa Zimamoto Isabela Bwago amesema “Ni uzembe wa mzazi aliyendoka akiwa amewafungia watoto wake. Taarifa ya moto tulipewa kwa kuchelewa na hata ingekuja mapema gari isingeweza kufika eneo la tukio kulingana na miundombinu mibovu,”.
1666622162943.png

==============================

Watoto wawili wamefariki dunia kwa kuungua baada ya nyumba waliyokuwemo kuteketea kwa moto katika Mtaa wa Mfifi, Kata ya Kihesa mkoani Iringa.

Inadaiwa watoto hao, Rehema Masanga (7) na Amos Masanga (5) ambao walikuwa wakiwa wamekumbatiana, walishindwa kujiokoa baada ya mama yao, Skolastika Mgombewa kufunga mlango kwa nje akiwaacha peke yao kisha kuondoka nyumbani.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mafifi, Rabi Mgata amedai kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa ambao ulishika godoro kisha kuunguza nyumba yote.

“Mama yao aliwafungia watoto ndani akaenda kunywa pombe kwa hiyo moto ulivyokuwa unaendelea kuwaka walishindwa kujiokoa, mama alirudi baadaye wakati tayari tumeshazima moto na kugundua watoto wamekufa,” amesema Mgata.

Mgata amesema baada ya kuzima moto walibomoa mlango na kukuta watoto wawili waliokufa huku wakiwa wamekumbatiana kwenye kona moja ya nyumba.

Kwa upande wao baadhi ya majirani wamesema awali walianza kuona moshi ukifuka lakini, wengine walidhani ni wa matairi.

Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Iringa, Isabela Bwago amekiri kuwa chanzo cha tukio hilo ni mshumaa ambao ulishika godoro kisha kuunguza nyumba yote bila kuokoa kitu chochote.

“Ni uzembe wa mzazi ambao aliondoka akiwa amewafungia watoto wake kwa nje. Taarifa ya moto tulipewa kwa kuchelewa na hata ingekuja mapema gari isingeweza kufika eneo la tukio kulingana na miundombinu mibovu,” amesema Bwango.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Issa Juma amesema wakati majirani wanahangaika kuzima moto huo hawakujua kama ndani kuna watoto.

Ameitaka jamii kuwa kuwa makini na matumizi ya mishumaa, vibatari, taa na kuwa walinzi wa familia zao hasa watoto.

MWANANCHI
 
Rest In Peace little Angels 🙏🙏

Hiyo mama angekuwa mke wangu sijui angenibebea mbeleko gani
 
Huyo mama atandikwe kifungo Cha maisha liwe fundisho Kwa wengine. Tunao lewa ovyo hovyo.
huyu mama ni mzembe sana na si mala ya kwanza miaka ya nyuma pia alishawahi kuchoma hiyo nyumba alimanusula amchome mwanae mkubwa ,hata hii ishu ya jana karudi saa saba usiku kalewa haelewi chochote yaani kakutana na police na majilani washazima moto muda mrefu
 
Watoto Rehema Masanga wa miaka 7 na Amos Masanga mwenye miaka 5 wamekutwa wakiwa wamekumbatiana baada kushindwa kujiokoa kutokana na kufungiwa ndani na mama yao.
very very painful
giphy.gif
 
Watoto Rehema Masanga wa miaka 7 na Amos Masanga mwenye miaka 5 wamekutwa wakiwa wamekumbatiana baada kushindwa kujiokoa kutokana na kufungiwa ndani na mama yao.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mafifi, Rabi Mgata amesema chanzo cha moto ni mshumaa ulioshika Godoro na kuunguza nyumba wakati mama wa watoto akidaiwa kwenda kunywa Pombe.

Kamanda wa Zimamoto Isabela Bwago amesema “Ni uzembe wa mzazi aliyendoka akiwa amewafungia watoto wake. Taarifa ya moto tulipewa kwa kuchelewa na hata ingekuja mapema gari isingeweza kufika eneo la tukio kulingana na miundombinu mibovu,”.
View attachment 2396636
==============================

Watoto wawili wamefariki dunia kwa kuungua baada ya nyumba waliyokuwemo kuteketea kwa moto katika Mtaa wa Mfifi, Kata ya Kihesa mkoani Iringa.

Inadaiwa watoto hao, Rehema Masanga (7) na Amos Masanga (5) ambao walikuwa wakiwa wamekumbatiana, walishindwa kujiokoa baada ya mama yao, Skolastika Mgombewa kufunga mlango kwa nje akiwaacha peke yao kisha kuondoka nyumbani.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mafifi, Rabi Mgata amedai kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa ambao ulishika godoro kisha kuunguza nyumba yote.

“Mama yao aliwafungia watoto ndani akaenda kunywa pombe kwa hiyo moto ulivyokuwa unaendelea kuwaka walishindwa kujiokoa, mama alirudi baadaye wakati tayari tumeshazima moto na kugundua watoto wamekufa,” amesema Mgata.

Mgata amesema baada ya kuzima moto walibomoa mlango na kukuta watoto wawili waliokufa huku wakiwa wamekumbatiana kwenye kona moja ya nyumba.

Kwa upande wao baadhi ya majirani wamesema awali walianza kuona moshi ukifuka lakini, wengine walidhani ni wa matairi.

Kamanda wa Zimamoto Mkoa wa Iringa, Isabela Bwago amekiri kuwa chanzo cha tukio hilo ni mshumaa ambao ulishika godoro kisha kuunguza nyumba yote bila kuokoa kitu chochote.

“Ni uzembe wa mzazi ambao aliondoka akiwa amewafungia watoto wake kwa nje. Taarifa ya moto tulipewa kwa kuchelewa na hata ingekuja mapema gari isingeweza kufika eneo la tukio kulingana na miundombinu mibovu,” amesema Bwango.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Issa Juma amesema wakati majirani wanahangaika kuzima moto huo hawakujua kama ndani kuna watoto.

Ameitaka jamii kuwa kuwa makini na matumizi ya mishumaa, vibatari, taa na kuwa walinzi wa familia zao hasa watoto.

MWANANCHI
🙆🙆
 
Umasikini ni gharama!
 
So sad,nimeshindwa Hadi kumalizia story nimesisimkwaa mmmh tuwalinde watoto wetu jmn.
 
Daaah...! Kwa jinsi watu wengine wanavyotafuta hao watoto wakikesha makanisani, kwa waganga wa kienyeji afu wazazi wengine wanawapoteza kizembe hivi duuuh...!
 
Unamwachia dogo wa miaka 7 alinde nyumba amuangalie na dogo wa miaka 5.
Hizi akili watu wengi sana wanazo, huwa wanataka mtoto awe na akili ya mtu mzima. Dogo akianza kuongea tu wanaanza kumtreat kama jitu zima.
Yale matendo ya kitoto hawataki ayafanye bali afanye yale mazuri machache sana wanayofanya wao na yale mabaya ambayo ndo asilimia kubwa anawaona wakiyafanya ndo asiyafanye kwakua ni mtoto bado.
 
Huyo mama ni zwazwa sana yaani ana acha watoto wadogo kisa kwenda kunywa mataputapu na kushikwa mattyakko yake?
Afungwe jela na akatwe sehemu zake asiwe na hamu tena ya kunyanduliwa maisha yake yote.
 
Back
Top Bottom