TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

ITV wametangaza kuwa kauwawa muandishi,kamanda wa polisi kapigiwa simu kuulizwa kadai yuko safarini network ni mbovu,baadae kadai hana taarifa hiyo akakata simu
 
CCM lazima wawe makini kwa haya matukio vinginevyo wanakoelekea siko. Ziko njia nyingi za kuzuia mihadhara lakini kwa mtindo huu, wanajiondoa madarakani kwa mbinu zao wenyewe.
 
Sasa amani ya nchi imetoweka!.

taarifa nilizonazo ni kwamba huyu mwandishi kafumuliwa tumbo na utumbo kutoka, na kufariki dunia palepale.
Source: Itv breaking news.

My take: Hawa polisi wanatekeleza amri ya chama tawala. Juzi pale msamvu walidai yule kijana alipigwa na kitu kizito! Leo watasemaje ili hali mwandishi alikuwa kazini?? Inasikitisha sana ndg zangu watanzania! Nani atakaeiwajibisha hii serikali dhalimu namna??
 
nyie lazimisheni maandamano lakini hayo maandamano ndio mnatafuta kutoweka kwenye ramani ya vyama vya siasa, iko wapi cuf ngunguri, wapi Nccr , kimsingi hiyo huruma mnayotaka kutoka kwa wananchi hamtaipata kwa staili ya maandamano

You are simply stupid trying to divert the discussion
 
Radio one: Anaulizwa Michael Kamwanda RPC anasema hawezi kuongea yupo barabarani!
 
Mkuu tupe tàarifa ilinyooka walipigwa kwenye mazingira gani?

Ni taarifa za uhakika kabisa

Mwandishi alikuwa natimiza wajibu wake wa kuchukua habari (movie) kwenye mkutano, kapigwa risasi na kufa hapo hapo.
Source; mtu alieoko kwenye tukio.
 
Mwili mzima ganzi!Kweli jamaa mshipa wao wa aibu wameukata!Hivi Police wanamaisha mazuri sana?Au posho huwa inaongezeka baada yakitu kama hicho?Eee Mungu angalia machozi yawategemezi wake aliwaacha hapa duniani.
 
Jamani tunakwenda wapi mtu akikataa kuesabiwa maana kila anapo Taka aki yake Ana jinsi hii nchi ya democracy why tunaishi Kama atuna Huru
 
Natoa pole kwa wafiwa. Ila nawashangaeni mno,nyie sindio juzi juzi mmeiona serikali ni sikivu kwenye suala la sensa?mkawatukana waislam kadri mlivyoweza na tena mkawa mnashangilia kila mnaposikia police wanawavamia waislam majumbani mwao na kuvunja milango kisa wamegomea sensa. Sasa leo nadhani mnajisifu ujinga kuwa mnakuwa upande wa serikali pindi serikali inapokuwa inawadhulumu waislam ila inapowageuzia mchezo mnalalamika. Jifunzeni kusema ukweli siku zote. Jana police kwa waislam mlishangilia leo imekuwa tofauti.
 
Back
Top Bottom