Iringa: Jela maisha kwa kubaka na kumpa mtoto Ukimwi

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,830
Mahakama ya Wilaya ya Iringa imemuhukumu kifungo cha maisha mara mbili Mzee Selemani Gwabuga maarufu Msabato, sambamba na kulipa fidia ya shilingi milioni 25, kulipa faini shilingi milion 5 na kuchapwa viboko 11 baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka Mtoto wa miaka 11 na kumuambukiza virusi vya UKIMWI.

Mahakama imesema Mzee Msabato mwenye umri wa miaka 78 alikuwa akiishi kitongoji cha Idodi , Isimani Mkoani Iringa na alikuwa jirani na Mtoto huyo na mara kadhaa alikuwa akihubiri Injili.

Hukumu imetolewa baada ya kukutwa na hatia ya makosa matatu ikiwemo la kubaka Mtoto mwenye umri wa miaka 11 na kumuambukiza virusi vya UKIMWI kwa makusudi huku akijua yeye ni Mwathirika na anatumia dawa za kufubaza UKIMWI (ARVs) na kosa la tatu ni kujaribu kubaka Mtoto huyo wa miaka 11 aliyekuwa akisoma darasa la tano hivyo kosa la kwanza amehukumiwa jela maisha na kosa la pili akahukumiwa tena jela maisha.

“Siku ya kwanza baaada ya kumbaka Mtoto alimpa shilingi 200 na kumuambia asiseme kwa Mtu yeyote na katika tukio jingine Mtuhumiwa alikutana na Mtoto huyo mtoni na alipojaribu kumlazimisha Mtoto huyo Mama wa Mtoto alitokea na Mzee alikimbia na taratibu za kumkamata zikafanyika”

Kesi hiyo imesimamiwa na Waendesha mashtaka wa Serikali Nashon Saimon pamoja na Balton Mayage na ilikuwa na Mashahidi wanne akiwemo Daktari aliyethibitisha Mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na kuambukizwa UKIMWI.
 
Huyo si wamuhukumu kunyongwa ata siku ya kesho tuu kama ushahidi umejitosheleza hakuna haja ya kuendelea kukaa humo gerezani, wanyongaji kama hakuna tuende China tukawakodi au mtangaze nafasi za kazi hiyo.

Majitu mengine hayapaswi kuwekwa gerezani ni kuyafuta tuu.
 
Hili lizee linatakiwa lipigwe mapanga likatwe katwe

Kwa kikurya tunaita kughecha ghecha mpaka libaki mishikaki
 
Dah!Wamemuonea sana mzee m-nini sijui!Ilipaswa apewe adhabu nyepesinyepesi tu:-

1-Afilisiwe kila kitu ifute kidogo machozi ya waathirika.Naamini atakuwa na mashamba kule Ismani.Ni sehemu ya barabarani na potential.

2-Anapigishwa magoti na lingetumika jambia/panga lililonolewa vizuri mbele ya umma,kichwa chake kinafyekwa mara moja,

3-Mwili wa huyo mzee punguani,ungerudishwa mahakamani na kuhukumiwa kifungo cha milele.
Anaenda kula tu ugali bure na kufuga chawa makwapani.
 
Duh! Sasa kama unajua una ukimwi ya nini kula asiye na ukimwi wakati wenye ukimwi wapo tele tena wamenona? Haya wale wanaopenda kusafisha mitaro huko jela moto huo unawakuta, wakijichanganya kuzibua mtaro huo ngoma itawahusu na wakimaliza kifungo tayari watakuwa wana maambukizi watatoka nayo kuja uraiani kuishi kwa mashaka tena. Mbaya kala mtoto kamharibia utengenezaji wa familia safi yenye afya bora
 
Adhabu hii ingekua nzuri kama angekua bado kijana,
Apate mda wa kujutia...

Huyo mtoto sijui saikolojia yake wataifanyaje, anapaswa kupata wataalamu haswa haswaa
Ikibidi abadilishiwe mazingira kabisa, shuleni, nyumbani mtaani hatakua na utulivu,
Imagine mzazi mwanao anafanyiwa hivi?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom